Polisi wachukua simu ya Zitto, ofisi za ACT Wazalendo kupekuliwa kutafuta nyaraka za kusinyaa kwa uchumi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Zitto Aachiwa, Polisi Wachukua Simu Yake, Ofisi za ACT Wazalendo Kupekuliwa Kutafuta Nyaraka za Kusinyaa kwa Uchumi



Leo Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto aliripoti Kituo cha Polisi Kamata jijini Dar es salaam kama alivyotakiwa awali na jeshi hilo. Jeshi la Polisi limechukua simu ya ndugu Zitto kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao, na wameahidi kuwa watairudisha kwake kesho jioni, na ametakiwa kurudi kituoni hapo Novemba 21, 2017.

Pia Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo, kwa Lengo la kufanya upekuzi wa Ofisi hizo wakitafuta nyaraka zilizotumika na Chama kufanya Uchambuzi wa Takwimu za Serikali ambao unaonyesha Uchumi wa Nchi yetu "UNASINYAA".

Ado Shaibu
Katibu - Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma
ACT Wazalendo
Novemba 7, 2017
Dar es salaam

=====
DAR: Jeshi la Polisi limemaliza upekuzi katika Ofisi za ACT-Wazalendo
> Wameondoka na baadhi ya vitu vikiwemo Flashdisk na Laptop
 
Tatizo la ngosha hakuandaliwa kushika uraisi sie wananchi tutazamie vituko zaidi kwenye uongozi wake
 
Ofisini na Nyumbani kwa hao viongozi wa ACT wangeenda kimya kimya, wasinge tangaza

Vitu kama Laptops, Tablets, Desktops na CPU zake, Flash disk, CD watavikosa

Watuhumiwa watavitoa na kuvificha kwingine

Vyombo vya usalama hapa wamekosea sana

 
Hapo wanataka kuvictimize watumishi wa uma ambao namba zao zitakutwa humo, ubazazi wa hali ya juu!
 
Na mkikuta wame delete vitu, pelekene kwa ITs wa ukweli vitarudishwa vyote
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom