Polisi wachukua simu ya Zitto, ofisi za ACT Wazalendo kupekuliwa kutafuta nyaraka za kusinyaa kwa uchumi

Kwanini polisi wasiwe wanaenda kwenye mitandao kuchukua taarifa za mawasiliano ya mtu wanaye mtuhumu badala ya kuchukua simu
 
Zitto Aachiwa, Polisi Wachukua Simu Yake, Ofisi za ACT Wazalendo Kupekuliwa Kutafuta Nyaraka za Kusinyaa kwa Uchumi



Leo Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto aliripoti Kituo cha Polisi Kamata jijini Dar es salaam kama alivyotakiwa awali na jeshi hilo. Jeshi la Polisi limechukua simu ya ndugu Zitto kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao, na wameahidi kuwa watairudisha kwake kesho jioni, na ametakiwa kurudi kituoni hapo Novemba 21, 2017.

Pia Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo, kwa Lengo la kufanya upekuzi wa Ofisi hizo wakitafuta nyaraka zilizotumika na Chama kufanya Uchambuzi wa Takwimu za Serikali ambao unaonyesha Uchumi wa Nchi yetu "UNASINYAA".

Ado Shaibu
Katibu - Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma
ACT Wazalendo
Novemba 7, 2017
Dar es salaam


HAHAHAHAHAH
Project ya Serikali hii na Chama cha zito
 
Ofisini na Nyumbani kwa hao viongozi wa ACT wangeenda kimya kimya, wasinge tangaza

Vitu kama Laptops, Tablets, Desktops na CPU zake, Flash disk, CD watavikosa

Watuhumiwa watavitoa na kuvificha kwingine

Vyombo vya usalama hapa wamekosea sana

Kiroho tunasema wamepigwa upofu! Na hii humtokea mtu anayefanya yasiyompendeza Mungu
 
Ila hali ya maisha imekuwa ngumu hasa kwa watumishi, serikali iongeze mishahara kwani itasaidia kuongeza mzunguko wa fedha kidogo na biashara kukua
 
Ofisini na Nyumbani kwa hao viongozi wa ACT wangeenda kimya kimya, wasinge tangaza

Vitu kama Laptops, Tablets, Desktops na CPU zake, Flash disk, CD watavikosa

Watuhumiwa watavitoa na kuvificha kwingine

Vyombo vya usalama hapa wamekosea sana

Sidhani kama polisiem wanajua tech ya dunia hii. Mimi naweza kuqa na laptop hapa lakini server ipo Poland. I access the sarver na kufanya yangu. Jkija kwenye laptop hukuti kitu...labda finger prints tu.
 
Ofisini na Nyumbani kwa hao viongozi wa ACT wangeenda kimya kimya, wasinge tangaza

Vitu kama Laptops, Tablets, Desktops na CPU zake, Flash disk, CD watavikosa

Watuhumiwa watavitoa na kuvificha kwingine

Vyombo vya usalama hapa wamekosea sana

Lini walipatia mkuu?? Walishindwa kumkill Lissu livu pale area D na livu bullets 38 kutumia bomba la SMG......gvt should invest in our national security.... kuna kazi zingine hawa form fours failures wanaweza kufanya...kama wasukuma mikokoteni,vijana wasungusungu vijijini n.k
 
Sema Zitto mwenyewe sio wakuonea huruma alitumika sana na JK .....muacha akione chamoto ...dhambi ya usaliti malipo ni hapahapa!acha wauwane tu.
 
Ni kinyume cha sheria kuchukua kitu cha mtu bila kutoka Kwa vyombo husika......hyo ni illegal obtain evidence
Ndomana serikali huwa wanashindwa sana kesi mahakamani

Ova
 
Back
Top Bottom