Polisi wachukua simu ya Zitto, ofisi za ACT Wazalendo kupekuliwa kutafuta nyaraka za kusinyaa kwa uchumi

Kwanini wapambane na Zitto badala ya kupambana na uchumi wenyewe uliosinyaa..???

I thought we could embrace his confidence to go to public na kusema kweli kuhusu uchumi wetu kwamba umesinyaa, kuliko mwingine ambaye angeamua kukaa kimya..!!!

Kwanini serikali inapenda kusikia kile tu ambacho inatamani kukisikia..???

Nonsense...!!!
 
Lakini polisi wetu wako makinii sana kupambanua mambo uchumi wa tz pia heheheh

Ova
 
dawa ni iphone tu na unaweka kidole wasichofikiria ili wasiweze kukusumbua
 
Give them inch will take a yard give them a yard will take a mile.

Tatizo ni kwamba jeshi la polisi linaendeshwa kwa mifumo na wawazo ya kikoloni.

Tumepiga hatua ndogo tu kutoka wenye mentality ya kikoloni.

Bado safari ndefu.

Lakini namna hii yakufikiri/kutenda ya vyombo vya dola inadumaza sana wananchi.
 
Hawa polisi . Watakwenda kufanya upekuzi. Sasa hata kama ni mimi si nitaficha hizo documents. watakuja kesho kufanya upekuz!!!!!
 
Zitto Aachiwa, Polisi Wachukua Simu Yake, Ofisi za ACT Wazalendo Kupekuliwa Kutafuta Nyaraka za Kusinyaa kwa Uchumi



Leo Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto aliripoti Kituo cha Polisi Kamata jijini Dar es salaam kama alivyotakiwa awali na jeshi hilo. Jeshi la Polisi limechukua simu ya ndugu Zitto kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao, na wameahidi kuwa watairudisha kwake kesho jioni, na ametakiwa kurudi kituoni hapo Novemba 21, 2017.

Pia Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo, kwa Lengo la kufanya upekuzi wa Ofisi hizo wakitafuta nyaraka zilizotumika na Chama kufanya Uchambuzi wa Takwimu za Serikali ambao unaonyesha Uchumi wa Nchi yetu "UNASINYAA".

Ado Shaibu
Katibu - Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma
ACT Wazalendo
Novemba 7, 2017
Dar es salaam




Hongereni jeshi la policcm kwa kuishikilia simu ya Mh.Zitto,ipekueni taratibu na hasa kwenye phone book maana yawezekana humo kwenye phone book kukawa kumefichwa viwanda zaidi ya 250,hakikisheni simu hiyo inapimwa mkojo na baada ya hapo ikabidhie kwa kikosi cha watu wasiojulikana ili waiteke au waipige risasi ili viwanda vyote vilivyofichwa humo vitoke.

Haiwezekani nchi iyumbe kiuchumi kwa sababu ya kasimu ka tochi ka Mh.Zitto,vunja mara moja,anafikiri uchumi unajengwa kwa kubadilishana na migebuka?
 
Mboba wanasumbuka hivyo...! Mambo mengine inatubidi tucheke tuuh..
 
Back
Top Bottom