Polisi wacharuka Dar es Salaam

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,070
253
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu 47 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi sugu waliokamatwa baada ya msako mkali uliofanikisha kukamatwa kwa magari 12 ya wizi, pikipiki tatu, silaha za moto, lita 200 za gongo na puri 500 za bangi.

Hayo yameelezwa na jana jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova aliyesema kwamba, jeshi lake limejipanga kukabiliana na aina zote za uhalifu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka.

Alisema, matunda ya kazi ya jeshi hilo yamepatikana kutokana na msako wa nyumba hadi nyumba uliofanywa Oktoba 29 mwaka huu katika eneo la Kawe, Mbezi Beach, Goba, Salasala, Mbezi Juu na baadhi ya maeneo ya Kimara, waliwakamata watu 17 huku wakiwa na silaha wakijiandaa kufanya uvamizi.

Aliwataja watu hao kuwa ni pamoja na David Dunia (23), Sued Tamba (22), Nassa Ndiaje (21) wote wakazi wa Kawe, Joseph Marwa (38) mkazi wa Mbezi Juu, Idd Mbaruku (32) mkazi wa Mwenge, Kelvin Luambano (27) mkazi wa Mbagala Kipati na Matola Rashid (26) mkazi wa Ubungo msewe.

Aliwataja wengine kuwa ni pamoja na Hiari Juma (39) mkazi wa Ilala Mchikichini, Hija Kibendo (40) mkazi wa Mbagala Kongowe, Obeti Mwakasanga (34) mkazi wa Yombo, Haji Jafari (26) ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma na mkazi wa Kijitonyama sambamba na Richard Shirima (36) mkazi wa Tanki bovu pamoja na wenzao watano.

Kwa mujibu wa Kova, Shirima ni mtuhumiwa hatari ambaye alikamatwa na polisi akiwa na bastola mbili aina ya Browing No. 061522 ikiwa na risasi sita na nyingine No. 540979 akiwa ametoka kufanya tukio la ujambazi.

Mbali na tukio hilo inadaiwa kuwa Aprili Mwaka huu, Shirima alitoroka katika gereza la Segerea na pia kwa sasa ni mfungwa wa miaka 30 kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha, sambamba na silaha hiyo mtuhumiwa huyo na wenzake walikamatwa wakiwa na vitu mbalimbali kama vile televisheni, Kamera, kompyuta ndogo, simu za mkononi, deki, pasi za umeme pamoja na mashine moja ya kusafishia zulia.

Kova alisema watuhumiwa hao pamoja na wenzao 30 pamoja na vibaka 12 waliokamatwa katika vitu mbalimbali vya daladala pia wamemkamata mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu wa magari aitwaye Harod Kanza (37) akiwa na magari manne aliyokuwa ameyaficha katika maeneo tofauti.

Aliyataja magari waliyokamatwa nayo kuwa ni Toyota Corolla T 923 BCH rangi ya fedha, Toyota Spacio T 352 BHH, Toyota Chaser T 923 BCY, Nissan HardBody lenye namba za usajili T 684 ADH pamoja na Pikipiki moja No. T 191 BBC aina ya HAONJIN.

Kova alisema, mshitakiwa baada ya kuhojiwa alishindwa kutoa maelezo ya uhalali wake, huku akimtaja mshiriki wake katika shughuli hiyo ya wizi kuwa ni Didas Matemu (32) mkazi wa Boko, aidha alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika. Magari mengine yalikamatwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom