Polisi waagizwa kuwakamata wanaofunga ving’ora na vimulimuli kwenye magari

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Jeshi la Polisi Tanzania limewaagiza makamanda wa polisi wa mikoa na wakuu wa usalama barabarani kuendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaokiuka sheria ya matumizi ya ving’ora.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ameagiza kuchukuliwa kwa hatua za kisheria kwa wanaofunga ving’ora, vimulimuli, taa zenye mwanga mkali na taa zenye kuwakawaka kwa kubadilisha rangi ambao sheria haijawapa kibali cha kufanya hivyo na hawana vibali kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

Jeshi hilo limeeleza kuwa kwa mujibu wa sheria wanaoruhusiwa kufunga ving’ora na vimulimuli ni magari ya dharura ambayo ni ya polisi, majeshi, magari ya kubeba wagonjwa au magari mengine na matela ambayo yamepata kibali kutoka wizara yenye dhamana.

Magari mengine ni yale yanayotumiwa na viongozi wakuu wa kitaifa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo kwa yeyote ambaye hayupo kwenye makundi hayo anakiuka sheria akiweka chochote kati ya vilivyoelezwa.

Chanzo: TBC
 
Itakuwa poa sana kama suala hili litachukuliwa Kwa uzito Kwa Sisi tunaoendesha Magari hapa dar watakubaliana na Mimi juu ya usumbufu tunaoupata nyakati za usiku.

Ila shida ni pale hivi vimulimuli huwa vinatembea usik ambapo traffic wanakuwa hawapo barabarani.
 
Bora ukiwa dar, balaa ni unapokuwa kwenye safari ndefu usiku, yaani imekuwa kero!! Hasa kwenye mafuso, na maroli, ni vimulimuli tu!!
 
Wakuu wa wilaya wengi wamefunga vimulimuli
Pia Kuna tabia ya kubandika namba bandia,hasa zile za Singapore.. hii tabia wanayo polisi ,ika siku hizi ata Tra, uhamiaji,manispaa,pccb wanabandika TU manamba ya ajabu
Kisheria magari ya serikali yenye namba za kiraia Lazima wapate Kibali Cha katibu mkuu kiongozi iliwaweke namba za kiraia
 
Nice move but a bit too late.. Pole kwa wale wafanyabiashra waliokwisha agiza huu mzigo
Unaagizaje vitu usivyoruhusiwa? Kuna kipindi nilikuwa nchi zilizoendelea, kaka yangu mmoja akaniagiza nimnunulie hizo taa za ving'ora akasisitiza red and blue. Nikatafuta wauzaji wa hivyo vitu, wakaniambia red and blue ni emergency vehicles tu ambulance,police na fire brigade. Kama nataka hizo wakaniambia niwaoneshe vibali/barua kutoka mamlaka za Tz kuruhusu niuziwe hivyo ving'ora. Nikawaambia ni kwa ajili ya kampuni ya ulinzi wakasema kampuni ya ulinzi taa zao ni orange tutakuuzia hata container zima. Kaka anasisitiza anataka blue and red basi tenda nikaikosa,nafikiri alinunua huko China.
 
Wakuu wa wilaya wengi wamefunga vimulimuli
Pia Kuna tabia ya kubandika namba bandia,hasa zile za Singapore.. hii tabia wanayo polisi ,ika siku hizi ata Tra, uhamiaji,manispaa,pccb wanabandika TU manamba ya ajabu
Kisheria magari ya serikali yenye namba za kiraia Lazima wapate Kibali Cha katibu mkuu kiongozi iliwaweke namba za kiraia
Hawa jamaa wanahisi sheria za nchi haziwahusu.
 
Most likely ni China ndio maana hata boda boda wanauwezo wa kufunga na kusumbua mitaani... China yeye anatafuta pesa haachi senti yako
 
Yeah China unapata chochote, hela yako tu. Lengo la kutofautisha hizi taa ni kuwa ukiona tu blue and red unapisha kwasababu unajua ni magari ya dharula. Lakini sasa imekuwa kero usiku unaona vimulimuli ukipisha bajaj!
 
Unaagizaje vitu usivyoruhusiwa? Kuna kipindi nilikuwa nchi zilizoendelea, kaka yangu mmoja akaniagiza nimnunulie hizo taa za ving'ora akasisitiza red and blue. Nikatafuta wauzaji wa hivyo vitu, wakaniambia red and blue ni emergency vehicles tu ambulance,police na fire brigade. Kama nataka hizo wakaniambia niwaoneshe vibali/barua kutoka mamlaka za Tz kuruhusu niuziwe hivyo ving'ora. Nikawaambia ni kwa ajili ya kampuni ya ulinzi wakasema kampuni ya ulinzi taa zao ni orange tutakuuzia hata container zima. Kaka anasisitiza anataka blue and red basi tenda nikaikosa,nafikiri alinunua huko China.
mchina hawazi anachoangalia ni pesa yako tu.
 
Kwahiyo na wliofunga Taa za booster itakuwa vipi au wao hili haliwagusi...?
 
Wakuu wa wilaya wengi wamefunga vimulimuli
Pia Kuna tabia ya kubandika namba bandia,hasa zile za Singapore.. hii tabia wanayo polisi ,ika siku hizi ata Tra, uhamiaji,manispaa,pccb wanabandika TU manamba ya ajabu
Kisheria magari ya serikali yenye namba za kiraia Lazima wapate Kibali Cha katibu mkuu kiongozi iliwaweke namba za kiraia
I think hapo kwenye kubandika namba za bandia wanafanya hivyo kwenye kufuatilia mishe za upelelezi maana wakitumia namba zao halisi ni rahisi watu kuwatambua mapema na kuharibu upelelezi. (inategemea na mission yenyewe).
 
Back
Top Bottom