Polisi wa Tanzania wanasa Malawi wakifuatilia wahalifu

They are very lucky the Geneva convention accord and treaty came to their rescue otherwise they would have been lynched to death because by trespassing other sovereign state border is to breach international land border and that offense is attempted murder and if convicted straight away an execution sentence by firing squad.

They are lucky!
Aisee kumbe we Mkaldayo upo vizuri kwenye Mambo ya International Law. Big Up!
 
NIMEPITIA COMENTS ZOTE NAONA WENGI KAMA SIO WACHANGIAJI WOTE WANASEMA "WAPIGWE TU".

WENGI WANAONA HATA JANGA LILILOWAPATA NI DOGO WANGETAMANI WANGEPATA MADHARA MAKUBWA ZAIDI.

POLISI WAJITAFAKARI
NI KWANN RAIA WENGI HAWAWAPENDI?
Polisi wameambiwa wasimwamini raia yeyote na sisi hatumpendi Polisi yeyote - mmemwaga ugali tunamwaga mboga!
 
walienda kutafuta rushwa hao.
Ebu tuseme ukweli, kuna sura ya kutaka kukamata magendo hapa, au walichoona ni fursa tu ya hela ya mboga?

1631871770087.png
 
Sijasema lolote juu kujua au kutokujua Kiingereza.Nina Cho jua Polisi wa Tanzania ni zero kabisa Kwenye lugha tukiachana hayo waambie siku moja wavuke mpaka wa Sirari wafike Migori waone au wavuke mpaka wa Namanga waone.
Lugha zinapigana?
 
Nimesoma comments nyingi,naona
Ni namna gani Jeshi la polisi la Tanzania linavyochukiwa,

Bila shaka ni namna wananchi,yaani wenye nchi yao wanavyoonewa/nyanyaswa na Askari wetu.

Niseme tu jeshi letu lijitafakari,

Lakini pia,kwanini askari kabisa mwenye uelewa kichwani ukaingia kwenye nchi za watu bila kufuata sheria kweli?

Au ni wale waliowekwa na wajomba zao
Aibu kwa jeshi letu.
 
Hatari sana hii,inabidi polisi wepewe elimu kuhusu utaratibu wa kuingia mipakani
Sasa mfano hapo ungekuwa mpaka wa Somalia
Au wataliban si ndiyo hakuna kurudi tena

Ova
 
Siku zote tunasema IGP Sirro na genge lake lote wanaojiita Polisi uwezo wao wa kufanya kazi professionally na kwa kutumia akili ni mdogo sana, lakini watu wanabisha. Haya ndio matokeo. Hebu angalia maelezo ya hili tukio hapa chini, na ieleweke ni kina nani walifanya upumbavu wa namna hii. Angalia hata kuandika tu ni tatizo, hakuna hata vituo.

TAARIFA YA TUKIO LA ASKARI POLISI WETU 7 KUINGIA NCHINI MALAWI.

MNAMO TAREHE 15/09/2021 MAJIRA KATI YA SAA 16:30 - 17:30HRS HUKO MANEO YA KITONGOJI CHA MTIMA, KIJIJI CHA IKUMBILO, KATA YA CHITETE, TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA ILEJE NA MKOA WA SONGWE ASKARI G.3695 D/SGT RAMADHANI,H.694 PC EDWARD, H.8096 PC SAFARI, WP.12285 PC ANASTAZIA, H.9727 PC JOSEPH, H.9781 PC HUSSEIN NA H.8764 PC JUMANNE WAKIWA NA GARI PT.3676 TOYOTA L/CRUISER MALI YA JESHI LA POLISI TANZANIA WAKITOKEA VWAWA KUPELEKA WATUHUMIWA WA KESI YA MAUAJI PI.3/2020, WALIPOFIKA MAENEO YA MTIMA NA KUONA PIKIPIKI INAYOSADIKIWA KUWA IMEBEBA MAGENDO KUTOKA NCHI JIRANI YA MALAWI, WALIISIMAMISHA LAKINI PIKIPIKI HIYO ILIAMUA KUKIMBIA KUELEKEA NCHI JIRANI YA MALAWI, ASKARI. WALIAMUA KUIFUKUZIA NA KUVUKA MPAKA WA TANZANIA NA KUINGIA NCHINI MALAWI NA NDIPO WANANCHI WA MALAWI WALIIZINGIRA GARI HILO IKIWA NA ASKARI NCO G3695 DSGT RAMADHAN, H.8096 PC SAFARI, H9727 PC JOSEPH, H.694 D/C EDWARD, H.9781 PC HUSSEIN, WP.12285 PC ANASTAZIA NA H.8764 PC JUMANNE WAKIWA NA SILAHA MBILI AINA YA AK 47 NA KUANZA KUWASHAMBULIA.KWA.MAWE NA BAADAYE KUPATA MSAADA WA KUOKOLEWA NA ASKARI POLISI WA MALAWI(+) KATIKA VULUGU HIZO ASKARI MMOJA H8764 PC PC JUMANNE AMBAYE NI DEREVA ALIJERUHIWA KWA KUKATWA NA PANGA KICHWANI HALI YAKE SIO MBAYA ANAENDELEA VIZURI PIA GARI INASEMEKANA LIMEHARIBIWA KWA KUPIGWA KWA MAWE NA SILAHA AK 47 ZOTE MBILI ZIPO SALAMA NA ZIMEHIFADHIWA KITUO CHA POLISI CHITIPA MALAWI. ASKARI NO. G.3695 D/SGT RAMADHANI AMBAYE ALIKUWA KIONGOZI WAO, H.8096 PC SAFARI NA H.9727 PC JOSEPH WALIFANIKIWA KUTOROKA KATIKA VULUGU HIZO NA KURUDI KITUONI SALAMA NA WAPO MAHABUSU KWA HATUA ZA KINIDHAMU. MAWASILIANO KATI YA UONGOZI WA WILAYA NA MKOA TANZANIA NA MALAWI YANAENDELEA KWA AJILI YA KUWAREJESHA NCHI ASKARI HAO PAMOJA NA GARI NA SILAHA.
Huyu alieandika kiboko.Kwahiyo watuhumiwa wa mauaji wamekimbia.?
 
Yani police bongo ilitakiwa uzi kama hizi ipitie,ione jinsi gani raia hawawakubali kabisa.

Ili labda,yani labda tena labda waweze kujirekebisa.
 
Hahahaahhaa haaaahaahahaa
Hahahaahhaa haaaahaahahaa

Pole sana Policcm mlivamia bonde la wanywa gongo na wavuta sigara kali zilizochanganywa na bangi zenye pilipili na bahati yenu

Wamalawi wangewatindua Marinda

Shwain!
 
Sijasema lolote juu kujua au kutokujua Kiingereza.Nina Cho jua Polisi wa Tanzania ni zero kabisa Kwenye lugha tukiachana hayo waambie siku moja wavuke mpaka wa Sirari wafike Migori waone au wavuke mpaka wa Namanga waone.
Kiingereza cha Kenya,kenye lafidhi ya lugha za kienyeji
 
Yaani walihisi bodaboda una magendo wakaamua kuikimbiza? hawana tofauti na wale TRA waliofariki kwa ajali wakikimbiza gari "lililodhaniwa" limebeba magendo.

Hapo walikuwa wakikimbilia rushwa tu.
 
Sijasema lolote juu kujua au kutokujua Kiingereza.Nina Cho jua Polisi wa Tanzania ni zero kabisa Kwenye lugha tukiachana hayo waambie siku moja wavuke mpaka wa Sirari wafike Migori waone au wavuke mpaka wa Namanga waone.

Uko sahihi kabisa, hawa Police wetu ni zero brain
 
We nawe ni mpumbavu sana kuongea kiingereza mnaonaga kama ndio unafanana na malkia Elizabeth sio?
Polisi anahudumia watu wote, na wageni toka nje. Nimewahi shuhudia siku moja, (mji sitautaja) polisi wa kike alishindwa kumwelekeza njia ya kwenda hotel aliofikia binti mzungu mmoja. 'sorry madame, just follow the police, she will lead you to your hotel, it is not far from here', niliongea nae baada ya kuingilia nilipogundua lugha gongana. Mzungu wa watu alishukuru wakaondoka. Kilichoendelea njiani sijui. Polisi kujua lugha zaidi ya moja inasaidia.
 
Siku wakijaribu huku Kenya, tutawarudushia majeruhi.Polisi wa Tanzania hata Kiingereza tu hawajui
Siwapendi Police wa Tanzanian, but back to your concern kiingereza is just a language like Swahili,
 
Akili yao inakuwaga kwenye rushwa tu hadi wanajisahau kama wanaingia kwenye nchi isiyowahusu, ovyo kabisa.
 
Polisi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya wametandikwa na Raia wa Malawi baada ya kuingia nchi hiyo ya kigeni kwa lengo la kuwasaka wafanya magendo .

Bado Haijafahamika walikopata utaratibu huo wa kuingia nchi ya watu kutafuta wahalifu huku Nchi ya Malawi ikiwa na Polisi wake , hata hivyo tunaishukuru serikali ya Malawi kwa kuwanusuru na vifo baada ya kuingilia kati kuwaokoa.


====
Mnamo tarehe 15/09/2021 majira kati ya saa 16:30 - 17:30hrs huko maneo ya kitongoji cha Mtima, kijiji cha Ikumbilo, kata ya Chitete, tarafa ya Bulambya, wilaya ya Ileje na mkoa wa Songwe askari G.3695 d/sgt Ramadhani, H.694 pc Edward, h.8096 pc Safari, wp.12285 pc Anastazia, h.9727 pc Joseph, h.9781 pc Hussein na h.8764 pc Jumanne wakiwa na gari pt.3676 toyota l/cruiser mali ya jeshi la polisi Tanzania wakitokea Vwawa kupeleka watuhumiwa wa kesi ya mauaji pi.3/2020, walipofika maeneo ya Mtima na kuona pikipiki inayosadikiwa kuwa imebeba magendo kutoka nchi jirani ya Malawi, waliisimamisha lakini pikipiki hiyo iliamua kukimbia kuelekea nchi jirani ya Malawi, askari.

Waliamua kuifukuzia na kuvuka mpaka wa Tanzania na kuingia nchini Malawi na ndipo wananchi wa Malawi waliizingira gari hilo ikiwa na askari nco g3695 dsgt Ramadhan, h.8096 pc Safari, h9727 pc Joseph, h.694 d/c Edward, h.9781 pc Hussein, wp.12285 pc anastazia na h.8764 pc jumanne wakiwa na silaha mbili aina ya ak 47 na kuanza kuwashambulia kwa mawe na baadaye kupata msaada wa kuokolewa na askari polisi wa Malawi(+) katika vulugu hizo askari mmoja h8764 pc pc Jumanne ambaye ni dereva alijeruhiwa kwa kukatwa na panga kichwani hali yake sio mbaya anaendelea vizuri pia gari inasemekana limeharibiwa kwa kupigwa kwa mawe na silaha ak 47 zote mbili zipo salama na zimehifadhiwa kituo cha polisi Chitipa Malawi.

Askari no. G.3695 d/sgt Ramadhani ambaye alikuwa kiongozi wao, h.8096 pc Safari na h.9727 pc Joseph walifanikiwa kutoroka katika vulugu hizo na kurudi kituoni salama na wapo mahabusu kwa hatua za kinidhamu. Mawasiliano kati ya uongozi wa wilaya na mkoa Tanzania na Malawi yanaendelea kwa ajili ya kuwarejesha nchi askari hao pamoja na gari na silaha.
wao walivuka mipaka wanategemea nini? au ndo walikuwa wanaringishia na uniform zao, kwamba na wao wanaajira YEHODAYA.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom