Polisi wa Tanzania wanasa Malawi wakifuatilia wahalifu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,348
217,390
Polisi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya wametandikwa na Raia wa Malawi baada ya kuingia nchi hiyo ya kigeni kwa lengo la kuwasaka wafanya magendo .

Bado Haijafahamika walikopata utaratibu huo wa kuingia nchi ya watu kutafuta wahalifu huku Nchi ya Malawi ikiwa na Polisi wake , hata hivyo tunaishukuru serikali ya Malawi kwa kuwanusuru na vifo baada ya kuingilia kati kuwaokoa.

malawi N.JPG



====
Mnamo tarehe 15/09/2021 majira kati ya saa 16:30 - 17:30hrs huko maneo ya kitongoji cha Mtima, kijiji cha Ikumbilo, kata ya Chitete, tarafa ya Bulambya, wilaya ya Ileje na mkoa wa Songwe askari G.3695 d/sgt Ramadhani, H.694 pc Edward, h.8096 pc Safari, wp.12285 pc Anastazia, h.9727 pc Joseph, h.9781 pc Hussein na h.8764 pc Jumanne wakiwa na gari pt.3676 toyota l/cruiser mali ya jeshi la polisi Tanzania wakitokea Vwawa kupeleka watuhumiwa wa kesi ya mauaji pi.3/2020, walipofika maeneo ya Mtima na kuona pikipiki inayosadikiwa kuwa imebeba magendo kutoka nchi jirani ya Malawi, waliisimamisha lakini pikipiki hiyo iliamua kukimbia kuelekea nchi jirani ya Malawi, askari.

Waliamua kuifukuzia na kuvuka mpaka wa Tanzania na kuingia nchini Malawi na ndipo wananchi wa Malawi waliizingira gari hilo ikiwa na askari nco g3695 dsgt Ramadhan, h.8096 pc Safari, h9727 pc Joseph, h.694 d/c Edward, h.9781 pc Hussein, wp.12285 pc anastazia na h.8764 pc jumanne wakiwa na silaha mbili aina ya ak 47 na kuanza kuwashambulia kwa mawe na baadaye kupata msaada wa kuokolewa na askari polisi wa Malawi(+) katika vulugu hizo askari mmoja h8764 pc pc Jumanne ambaye ni dereva alijeruhiwa kwa kukatwa na panga kichwani hali yake sio mbaya anaendelea vizuri pia gari inasemekana limeharibiwa kwa kupigwa kwa mawe na silaha ak 47 zote mbili zipo salama na zimehifadhiwa kituo cha polisi Chitipa Malawi.

Askari no. G.3695 d/sgt Ramadhani ambaye alikuwa kiongozi wao, h.8096 pc Safari na h.9727 pc Joseph walifanikiwa kutoroka katika vulugu hizo na kurudi kituoni salama na wapo mahabusu kwa hatua za kinidhamu. Mawasiliano kati ya uongozi wa wilaya na mkoa Tanzania na Malawi yanaendelea kwa ajili ya kuwarejesha nchi askari hao pamoja na gari na silaha.

Pia soma: Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi
 
They are very lucky the Geneva convention accord and treaty came to their rescue otherwise they would have been lynched to death because by trespassing other sovereign state border is to breach international land border and that offense is attempted murder and if convicted straight away an execution sentence by firing squad.

They are lucky!
 
Hiyo ndio faida ya kuwa na polisi wenye div 4 na zero form 4,watazijulia wapi sheria...!
Ila elimu angalau ya diploma na degree ni muhimu sana kwa Polis wetu, ijapokuwa kuna ulakini katika elimu yetu ya juu!

Nilijaribu kufanya utafiti kidogo, na kubaini kuna utofauti mkubwa sana wa kimawazo kati ya Polisi au mwanajeshi mwenye bachelor degree na huyo form four failure!
 
Sikatai wao kukosa akili ya kufikiri ni wapi walikuwa wanaenda, lakini niwaulize hata macho ya kuona huu ni mpaka tunavuka walikosa? Japo pichani naona wana macho.
Au basi bora angekuwa 1 hapo sawa, sasa hicho kikosi chote wao hata kujadiliana tu kwa muda oya vp tuvuke au tusivuke?
Hili jeshi lijitafakari sana yaani unavuka boda hata raia mgeni huuliza sasa wao imekuweje?
Hiyo ndo inaonyesha hawana mahusiano mazuri na wenzao wa upande wa pili hata raia wa upande huo pengine wanafanyiwa vituko na hawa Askari wa Tz sio kawaida kabisa wapigwe hata kuguswa tu!
Yaani mi ndo naona aibu!
Hata kama mlifatilia mali zenu nendeni kihalali sio kibabe ona kilichowapata!
Simbachawene sijui hizi taarifa kazipokeaje au RPC na hata RCO.
 
Back
Top Bottom