Polisi wa Tanzania wanasa Malawi wakifuatilia wahalifu

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
12,303
2,000
Watu wengi wanatype kuuliza 'Hawakuuona mpaka?' wakidhani ni kama kwenye muvi kwamba mpaka utakua na watu wa custom, askari wengine, maafisa uhamiaji n.k.

Yes, sehemu ambayo mtu anataka kupita kihalali itakua hivyo.

Lakini hawa walikua wanafuatilia magendo unadhani wangepitia hapo? Logically it means walipita njia za panya na njia hizo zilivyo kujua kwamba upo sehemu nyingine ni kazi ya ziada. Kwani mnavyosikia kuna waTz wananunua sukari Malawi unafikiri wanapita wapi? Kwenye hilo eneo la ukaguzi?

Na kuna swala jingine hapa. Hii ishu haitakua treated kama askari wameingia Malawi bali itakua ni waTz wameingia Malawi. Na haitasemwa wananchi wa Ipenza wamerushia mawe gari la askari wa Tz no itakua ni waMalawi wamewashambulia waTz.

Kwahiyo mtu yuko bize kusema hao askari ni divisheni zero but actually hata yeye hana tofauti na hao askari na inamaanisha tu hata kiingereza hajui. WaTz tubadilike tusiione habari na kuipokea kwa kuangalia inafeed vipi ego zetu badala yake tuielewe habari na tusisome ili tujibu, tusome kuelewa.

Kama unashangaa hao askari kuingia Malawi huku hawana hata ramani nikikuambia kuna jenerali wa jeshi aliingia nchi nyingine, akiwa na ramani na akasimika bendera ya nchi yake eneo jingine huku akiwa na kikosi bila kujua kama yupo nchi nyingine utasemaje?
Usiwatetee polisi wamefanya uzembe, kwenye gari umebeba watuhumiwa wa mauaji unaenda kuhangaika na pikipiki ili iweje? Yote hiyo ni kutaka rushwa tu, sasa unajua hao watuhumiwa wa mauaji walipo? Je kama wametoroka kutokana na hilo sekeseke
 

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,852
2,000
wao walivuka mipaka wanategemea nini? au ndo walikuwa wanaringishia na uniform zao, kwamba na wao wanaajira YEHODAYA.
Hongera sana polisi wetu kutuwakilisha vizuri kwa kuipeleka Tanzania kimataifa, kuwathibitishia kuwa utendaji wenu unaovuka mipaka kufikiri kiweredi na kulalamikiwa na watanzania ni wa kweli.
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
12,303
2,000
Polisi anahudumia watu wote, na wageni toka nje. Nimewahi shuhudia siku moja, (mji sitautaja) polisi wa kike alishindwa kumwelekeza njia ya kwenda hotel aliofikia binti mzungu mmoja. 'sorry madame, just follow the police, she will lead you to your hotel, it is not far from here', niliongea nae baada ya kuingilia nilipogundua lugha gongana. Mzungu wa watu alishukuru wakaondoka. Kilichoendelea njiani sijui. Polisi kujua lugha zaidi ya moja inasaidia.
Kwahiyo kila mzungu anajua kingereza? Pumbavu wewe
 

Ntozi

Member
Feb 1, 2021
50
125
Sikatai wao kukosa akili ya kufikiri ni wapi walikuwa wanaenda, lakini niwaulize hata macho ya kuona huu ni mpaka tunavuka walikosa? Japo pichani naona wana macho.
Au basi bora angekuwa 1 hapo sawa, sasa hicho kikosi chote wao hata kujadiliana tu kwa muda oya vp tuvuke au tusivuke?
Hili jeshi lijitafakari sana yaani unavuka boda hata raia mgeni huuliza sasa wao imekuweje?
Hiyo ndo inaonyesha hawana mahusiano mazuri na wenzao wa upande wa pili hata raia wa upande huo pengine wanafanyiwa vituko na hawa Askari wa Tz sio kawaida kabisa wapigwe hata kuguswa tu!
Yaani mi ndo naona aibu!
Hata kama mlifatilia mali zenu nendeni kihalali sio kibabe ona kilichowapata!
Simbachawene sijui hizi taarifa kazipokeaje au RPC na hata RCO.
Wale mahabusu waliokuwa wanapelekwa Ileje ilikuweje?Au nao walitokomea
 

VYEMELO

Senior Member
Jul 21, 2020
109
250
Polisi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya wametandikwa na Raia wa Malawi baada ya kuingia nchi hiyo ya kigeni kwa lengo la kuwasaka wafanya magendo .

Bado Haijafahamika walikopata utaratibu huo wa kuingia nchi ya watu kutafuta wahalifu huku Nchi ya Malawi ikiwa na Polisi wake , hata hivyo tunaishukuru serikali ya Malawi kwa kuwanusuru na vifo baada ya kuingilia kati kuwaokoa.


====
Mnamo tarehe 15/09/2021 majira kati ya saa 16:30 - 17:30hrs huko maneo ya kitongoji cha Mtima, kijiji cha Ikumbilo, kata ya Chitete, tarafa ya Bulambya, wilaya ya Ileje na mkoa wa Songwe askari G.3695 d/sgt Ramadhani, H.694 pc Edward, h.8096 pc Safari, wp.12285 pc Anastazia, h.9727 pc Joseph, h.9781 pc Hussein na h.8764 pc Jumanne wakiwa na gari pt.3676 toyota l/cruiser mali ya jeshi la polisi Tanzania wakitokea Vwawa kupeleka watuhumiwa wa kesi ya mauaji pi.3/2020, walipofika maeneo ya Mtima na kuona pikipiki inayosadikiwa kuwa imebeba magendo kutoka nchi jirani ya Malawi, waliisimamisha lakini pikipiki hiyo iliamua kukimbia kuelekea nchi jirani ya Malawi, askari.

Waliamua kuifukuzia na kuvuka mpaka wa Tanzania na kuingia nchini Malawi na ndipo wananchi wa Malawi waliizingira gari hilo ikiwa na askari nco g3695 dsgt Ramadhan, h.8096 pc Safari, h9727 pc Joseph, h.694 d/c Edward, h.9781 pc Hussein, wp.12285 pc anastazia na h.8764 pc jumanne wakiwa na silaha mbili aina ya ak 47 na kuanza kuwashambulia kwa mawe na baadaye kupata msaada wa kuokolewa na askari polisi wa Malawi(+) katika vulugu hizo askari mmoja h8764 pc pc Jumanne ambaye ni dereva alijeruhiwa kwa kukatwa na panga kichwani hali yake sio mbaya anaendelea vizuri pia gari inasemekana limeharibiwa kwa kupigwa kwa mawe na silaha ak 47 zote mbili zipo salama na zimehifadhiwa kituo cha polisi Chitipa Malawi.

Askari no. G.3695 d/sgt Ramadhani ambaye alikuwa kiongozi wao, h.8096 pc Safari na h.9727 pc Joseph walifanikiwa kutoroka katika vulugu hizo na kurudi kituoni salama na wapo mahabusu kwa hatua za kinidhamu. Mawasiliano kati ya uongozi wa wilaya na mkoa Tanzania na Malawi yanaendelea kwa ajili ya kuwarejesha nchi askari hao pamoja na gari na silaha.

Pia soma: Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi
Askari polisi wa Tanzania hawana weledi wa kutosha. Kozi yao ni fupi mno. They are not professional.
 

VYEMELO

Senior Member
Jul 21, 2020
109
250
Ila elimu angalau ya diploma na degree ni muhimu sana kwa Polis wetu, ijapokuwa kuna ulakini katika elimu yetu ya juu!

Nilijaribu kufanya utafiti kidogo, na kubaini kuna utofauti mkubwa sana wa kimawazo kati ya Polisi au mwanajeshi mwenye bachelor degree na huyo form four failure!
Ukikuta askari polisi mstaarabu anafuata na kuzingatia ethics za jeshi la polisi, ukifuatilia utakuta ni mwenye diploma, adv. Diploma, au degree.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom