commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,952
kutokana na Ripoti ya mwenyekiti wa kamati ya bunge ya miundombinu Mh Peter serukamba,bungeni sasa hivi.
Ni kwamba bandari ya Dar es salaam,imekumbwa na wimbi la kukimbiwa na wateja kwa wingi kutokana na sababu kadhaa.mojawapo ikiwa ni usumbufu wanaoupata wateja kwa kusimamishwa mara kwa mara barabarani na polisi wa Tanzania wanapokuwa safarini kusafirisha mizigo yao kutoka bandari ya Dar es salaam kuelekea katika nchi zao.
Ametoa mfano wa takwimu kwamba Lori moja likisafiri toka Dar es salaam hadi Rusumo mpakani mwa Rwanda,linasimamishwa na polisi njiani mara 45, na wakati huo huo akasema Lori linalosafirisha mzigo toka bandari ya Mombasa hadi Kigali kupitia Uganda linasimamishwa mara 5 tu.
My take: Namuomba IGP mwema atumie taarifa hii kufanya marekebisho makubwa katika jeshi lake ili kuokoa uchumi wa nchi yetu, ikiwa ni pamoja na kamata kamata ndani ya nchi yetu zisizozingatia haki ambazo zinasababisha nguvu kazi ya wananchi wengi kukaa mahabusu bila sababu za msingi na kuligharimu taifa chakula ulinzi na matibabu ikiwa ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi pamoja na kuwasababishia matatizo familia zao.ambazo mara zingine huwa ni wategemezi kwa ndugu hao.