Polisi wa Magufuli nimempiga bonge la chenga.

deluxelub

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
250
250
Salam zenu,
Ilikuwa siku Jumamosi kama saa 10:00 asubuhi hivi. Kwa kawaida kazini kwetu huwa siku za weekend tunafanya kazi asubuh hadi mchana tu.

Mkuu wangu wa kazi alikuja nilipo na kunipa maagizo niende na gari kumchukuwa mgeni wa ofisini katika Airport flani hivi hapa hapa tz. Namie nikafanya hivyo baada ya kuchukuwa taarifa za mgeni pale mapokezi na kuanza safari.

Nilipofika pale Airport kama 9:45 asubuhi nikaweka gari kwenye maegesho na kusubiria tarifa za ndege ambayo yumo mgeni wangu, mara naskia mlio wa simu yangu ndogo kanokia cha tochi pwerrr pwetrrr pwerrrr na kamtetemeko chake zzzzzzzzzz.

Nikapokea simu kwa sauti ya kawaida tu mana ilikua nambari ngeni sana. Nikaskia mtu akizungumza kwa lugha ya kigeni huku akijielezea kuwa yeye ndio mgeni ambae nimepangiwa nikamchukuwe pale Airport na mie sikuzembea nikamwambia nipo ndani ya Airport Compound. Akashkuru pale na kuniambia yuko kwenye sehemu ya arrivals tayari.

Basi nikajisogeza mdogo mdogo pale na kasimu changu mwenyewe mara kaniona akaniita kwa jina langu tukasalimiana vizuri tu afu nikachukuwa mabegi yake nakuingiza kwenye gari ya ofisini.

Nikawasha engine na kutembea mdogo mdogo kuelekea geti la kutokea njee, mara namuona askari polisi kanisimamisha na kunitaka niteremshe kiyoo cha gari na kuanza kunihoji kuwa yule niliempakia amekuja kwa kutumia Visa ya kuwa mtalii au vp. Sikusita nikamwambia muulize mwenyewe. Mgeni akatowa passport yake na kumuonyesha yule polisi.

Apo sasa ndio noma. Polisi akaniambia gari niliyoenda nayo hairuhusiki kwa kuchukulia wageni na kuwatembeza. Akimaanisha gari husika huwa ni private hire. Mie najua hili jambo lkn sikutegemea kama pale yule polisi atakuja na swaga hizi. Basi tukazinguana pale weeee mpaka kaanza kuhamaki na kuniamuru niondoshe gari pale.

Ahh mjini shule bwana nikamwambia yule mgeni aende kukaa kwenye sehemu ya kupata vinywaji pale akae kidogo ili mie nitowe gari njee afu yeye anifuate njee kwa mlango wa kutokea resta. Yule polisi nikamwambia naenda kuchukuwa gari nyengine ambayo itafaa kwa kupakia wageni. Namie nilijiongeza kidogo pale nikatowa simu yangu kubwa sasa nikawa na gusa nambari kwenye kiyoo sasa huku nazugisha kupiga simu naulizia ofisini kuna dereva yoyote pale aje na gari ya private hire mana kuna polisi kanizuiya kuchukuwa mgeni. Nikaambiwa gari zipo ila dereva ndio hapana. Basi polisi akaniruhusu nikafuate gari nyengine.
 

deluxelub

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
250
250
Afu siunajuwa hawa jamaa wanakuaga na njaa sana. Wao wako kwenye rushwa tuuu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom