Polisi wa kikwete waua tena huko shinyanga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wa kikwete waua tena huko shinyanga!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkombemaro, Jan 8, 2011.

 1. nkombemaro

  nkombemaro Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WANANCHI wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamefanya maandamano hadi ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kulaani kitendo cha askari polisi kumuua raia mmoja kwa kukutumia risasi.
  Mbali na hilo wananchi hao pia waliandamana kupinga baadhi ya askari kuwabambikiza kesi wananchi.
  Tukio la kuuawa kwa raia huyo lilitokea wakati polisi walipowavamia baadhi ya vijana waliokuwa wakinywa pombe katika eneo la mnada wa Mhunze Desemba 16, mwaka jana.
  Wananchi hao waliandamana wakiwa wamebeba mabango yaliyotoa ujumbe kwa serikali, wakiitaka ichunguze tukio hilo kwa umakini na kusikiliza kilio cha wananchi hao na kudai kuwa wao hawana hatia.
  Kufuatia tuko hilo wananchi hao wameiomba serikali kuwachukulia hatua askari waliohusika na uonevu huo sanjari na kukomesha unyanyasaji kwa raia na kuongeza kuwa hali hiyo inawatisha wananchi kushirikiana na polisi katika kukabiliana na uhalifu.
  Akizungumzia hilo Diwani wa Kata ya Kishapu Daudi Matungwa alikiri kutokea kwa tukio hilo lililosababisha mmoja wa wananchi hao aliyejulikana kwa jina la Luhende kupoteza maisha baada kupigwa risasi na polisi siku chache zilizopita.
  Alisema kabla ya kifo chake, alipelekwa hospitali ya rufaa Bugando Mwanza na alifariki Desemba 19, mwaka jana.
  Kufuatia kifo cha raia huyo diwani huyo alisema wananchi wa kijiji hicho baada ya kupewa taarifa ya kifo cha mwananchi mwenzao waliamua kususia mazishi hadi pale ambapo serikali ingetoa muafaka wa tatizo hilo ambapo baadaye mwili huo ulizikwa.
  Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga, Hussein Kashindye, alipoulizwa alikiri kupokea taarifa hizo na kwamba ofisi yake inayafanyia kazi.
  Naye mkuu wa wilaya ya Kishapu Abudullah Lutavi alithibitisha kupokea maandamano ya wananchi na aliwaasa kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo. MY TAKE! INAMAANA HIZI RISASI ZA POLISI ZIMEKOSA KAZI? KWANINI KIKWETE ASIWAPELEKE POLISI WOTE WA TANZANIA HUKO AFGHANSTAN WAKAISADIE AMERIKA KUIMALISHA ULINZI?
   
 2. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hawa watu wamekua out of control.
   
 3. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtikila alisema mtu fulani ni gaidi kwa hiyo inawezekana polisi ni kikosi cha mtu huyo! Mimi simo
   
 4. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Idiot idiot idiot:A S-confused1:
   
 5. nkombemaro

  nkombemaro Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu tuondolee balaa hili! hivi ni tanzania tu au hata nchi nyingine ni hivo?
   
 6. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Wanakiuka haki za binadamu
   
 7. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Kuna risasi zinaitwa za plastick something like that kwa nini huwa ma police hawatumii hizo? Au hawana? Au ni makusudi yao la kufikisha ujumbe kwa kuua? Lakini enyi police kaeni mkijua damu ya mtu haimwagiki bure never
   
 8. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Kutokana na wingi wa risasi wanaamua kutumia ovyo ili zipungue kwenye maghala yao
   
 9. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hapa naona kama polisi wana rahana fulani inabidi waombewe kuondoa mikosi
   
 10. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  I think polisi wako frustrated na maisha, baya wanalolifanya nikutoa frustration zao kwa wrong people.
   
 11. T

  The Future. Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  that is too much, something to rescue these poor citizens.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hujaeleweka mkuu... idiot polisi, watu wa shinyanga, wewe, JF au sisi tunaosoma?
   
Loading...