Polisi wa doria za Pikipiki wamejisahau

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
image061.jpg
Tangu nimerejea Tanzania miezi 7 iliyopita nimekuwa nashangazwa sana na ongezeko la Polisi wenye pikipiki maarufu kama TIGO wanaofanya kazi ya kukagua stickers za Bima, kukagua kama umelipia Kodi ya mwaka ya umiliki wa gari, wanakagua malori ya mkaa , pia wako busy kukagua bodaboda na kusimamisha pickups ili kujua kama mzigo uliobeba umekatiwa receipts.
nilipodadisi nikaambiwa kumbe walipewa pikipiki zile si kwaajili ya kuwasaidia Trafic na maofisa wa TRA KAZI ZAO BALI ni kwaajili ya kukabiliana na uhalifu kwa maana ya Ujambazi na kuwa katika hali ya tahadhali kwa matukio makubwa.

Wanapaswa kufanya Doria za mtaa kwa mtaa, kukabiliana na wahalifu wa silaha na sio kukabiliana na waendesha bodaboda na malori ya mkaa
 
Hizo pikipiki wamepewa ni za kutafutia hela kupitia rushwa ya kulazimisha, kutisha raia ili wapewe hela, kufanya ujambazi kwa kutumia silaha zao.
Hawana faida yoyote zaidi ya hasara
 
Kwa taarifa yako hizo pikipiki wamekabidhiwa lakini mafuta hayatolewi na serekali ikiharibika ni juu ya askari kuitengeneza.Je kama ni wewe ungefanyeje ili mafuta yawezekupatikana sambamba na matengenezo yake?.
 
Acha ujinga mafuta na matengenezo pamoja na mishahara ya askari hawa vyote vinalipwa na walipa kodi wa Tanzania. kilichopo hapa ni kwamba ule ni mradi wa wakubwa wa polisi na kama askari akiaminika na wakubwa na kupewa piki piki maana yake ni kwamba aweke mafuta, afanyie ukarabati na bado mwisho wa siku apelike hesabu ya makusanyo kwa mkubwa wake. usicheze na polisi wa tanzania bana wote ni wezi kama serikali na chama chao CCM.
 
hayo ni makubwa , kuumbe ! unajua kuna mambo mengi hatuyajui juu ya utendaji kazi, maana kuutwa wako pembezoni mwa barabara wanasaka wauza mkaa, kukagua sticker ya TRA na Ile ya Bima
 
Wapo busy kukamata waendesha boda boda wanakusanya buku 2 2 na kama umenunua khanga au kitu chochote ukasahau kuomba receipt usiombe ukutane na hawa jamaa tiGo
 
Inaelekea Saidi Mwema ameshindwa kuwadhibiti askari hawa. Wanachofanya sasa ni kuwatisha raia kwa bunduki ili watoe rushwa. Tanzania ni nchi pekee duniani ambapo askari wenye silaha wanakagua leseni za magari.
 
yaani wamepewa vitendea kazi wao wanavitumia kutafutia fedha haramu
 
Wana JF,nina mashaka na uzalendo wenu,thread hii ni ya maana sana kwa jamii kutokana na dhuluma kubwa inayofanywa na hawa askari wa piki piki na waathirika wakubwa ni wananchi wa kawaida,wana muliwa vilivyo kwa hicho kidogo wanacho kihangaikia jijini.Wachangiaji hapa kiduchu,lakini ingekuwa ni thread ya CDM VS CCM watu kibao wangerushiana maneno ya Kila aina humu.Uzalendo Kama moja wapo ya tunu za Taifa,ndugu zanguni hamna.
 
Back
Top Bottom