Polisi wa Arusha wampuuza Rais Samia, wakamata wateja baa na kuwapiga

Mragha

Member
Aug 12, 2021
9
6
Polisi wa Arusha jana Tarehe 14/12/2021 wamepita kwenye mabar na land cruiser nyeupe wanakamata wateja na wenye bar na kuwapiga na kuwadai sh 15,000 kwa kila mtu kwa madai wametumwa na wakubwa wao.

Kukamata watu waliopo kwenye mabar zaidi ya saa 5.

Kukamata sawa ila kupiga na kudai hela Mama Samia ameonya juzi akiwapa vyeo mabosi wao. Isitoshe kuna mamlaka inayohusika na wafanyabiashara wanao chelewa kufunga Afisa biashara kwanini wanapokamata wasiwapeleke huko wapingwe faini ambayo ni sh 50,000.
 
Majeshi kwenye nchi hii huwa yana kautawala kao ka ndani 🤣🤣..

Mwendazake baada ya kusalimu amri aliishia kusema kwamba waachwe kwa sababu eti ni vihera vidogo wanavypoata barabara.

Hapo ndio utajua unajua hujui.
 
Mama mwenyewe sio kwamba amewaonya,ni kwamba amewaomba kuacha rushwa.mtu ukiombwa jambo una uhuru wa kukubali hilo jambo au kukataa.kwa hiyo hao police wa arusha wameamua kukataa ombi la mama na hana cha kuwafanya I guess.
 
Polisi wa Arusha jana Tarehe 14/12/2021 wamepita kwenye mabar na land cruiser nyeupe wanakamata wateja na wenye bar na kuwapiga na kuwadai sh 15,000 kwa kila mtu kwa madai wametumwa na wakubwa wao.

Kukamata watu waliopo kwenye mabar zaidi ya saa 5.

Kukamata sawa ila kupiga na kudai hela Mama Samia ameonya juzi akiwapa vyeo mabosi wao. Isitoshe kuna mamlaka inayohusika na wafanyabiashara wanao chelewa kufunga Afisa biashara kwanini wanapokamata wasiwapeleke huko wapingwe faini ambayo ni sh 50,000.
Kazi iendeleeeee
 
Basi wataendelea kula rushwa. Watu wengine wanaweza kuvumilia ukata wa hela, ila siyo polisi.

Polisi hawawezi kuvumilia ukata, wakati wanamiliki nguvu na silaha za moto.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kwa mujibuwa maneno yako maaana yake hata hao wengine unaosema wanaweza kuvumilia ni kwamba sio kwamba wanaweza kuvumilia ila tu hawana nguvu,hawana silaha hivyo wanashindwa kula rushwa ila na wao wakipata hivyo vitu watafanya.
 
Wakiwa polisi ni lazima watakula rushwa tu.

Cha kufanya, maslahi ya polisi yaboreshwe, na pia waachane na division zero!

Back
Top Bottom