Polisi 'vinara' wa daladala mbovu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi 'vinara' wa daladala mbovu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Mar 24, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,337
  Likes Received: 19,507
  Trophy Points: 280
  Polisi 'vinara' wa daladala mbovu Send to a friend Wednesday, 23 March 2011 21:28 0diggsdigg

  Geofrey Nyang'oro
  MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imewashtaki askari wa Jeshi la Polisi kwa Rais Jakaya Kikwete ikidai kuwa ndiyo chanzo cha uvunjaji wa kanuni, sheria na taratibu za usafiri barabarani kutokana na baadhi yao kumiliki magari ya usafiri yakiwemo mabasi ya kusafirisha abiria ya daladala, mengi yakiwa ni mabovu.Mashtaka hayo ya Sumatra dhidi ya polisi yalitolewa jana na Mkurugenzi wake Mkuu, Israel Sekirasa wakati Rais Kikwete alipofanya ziara katika Wizara ya Uchukuzi.

  Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo, Sekisara alisema Polisi ndiyo wasimamizi wa Sheria na kanuni za usalama barabarani, lakini akasema licha ya kubeba jukumu hilo, wanamiliki magari ya usafirishaji, hivyo jukumu hilo la kuzisimamia kuwawia vigumu.Katika taarifa yake, Sekirasa alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili Sumatra, kubwa ikiwa ni wasimamizi wa sheria kuwa na ubinafsi katika utendaji wao wa kazi (conflict Interest).

  Kauli hiyo ilimshtua Rais Kikwete ambaye alionyesha hali ya mshangao na kukatisha maelezo ya Sekirasa na kuuliza: "Unasema watu wana ubinafisi kivipi, ni kina nani hao?." Sekirasa akajibu: "Polisi." Jibu hilo lilimshangaza zaidi Rais Kikwete ambaye aliuliza tena, “Polisi!?” Sekarasa akamjibu: "Baadhi ya maofisa wa polisi."

  Majibu hayo ya Mkurugenzi wa Sumatra yalimfanya Rais kuangua kicheko na kisha akasema: "Hii ya leo ni kali," na kuwataka Sumatra kufanya kazi bila woga na kuahidi kuisaidia mamlaka hiyo.Mkurugenzi huyo wa Sumatra alisema baadhi ya maofisa ambao wameingiza magari yao kwenye mzunguko wanapopewa kazi ya kusimamia sheria na kanuni za usalama barabarani, huwa ngumu kwao na hivyo kushiriki kuzivunja.

  Alisema hali hiyo ndiyo iliyosababisha Sumatra kuchukua hatua ya kuingia mkataba na kampuni binafsi kusimamia utekelezaji wa sheria na kanuni za usafirishaji barabarani ingawa kampuni hiyo ilikuwa na tatizo lake binafsi.
  Rais Kikwete aliitaka Sumatra kuendelea kutimiza majukumu yake kwa kuwa sekta hiyo ni muhimu kwa uchumi wa taifa.

  Awali, Rais Kikwete alihoji sababu za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kufanya kazi kwa kusuasua... “Alipokuja Bush Rais Mstaafu wa Marekani), hapa tuliambiwa fanyeni mkutano wenu kabla ya saa tano kwani muda huo kutakuwa na mvua na kweli ikanyesha, sasa tatizo nini. Kwa nini wataalamu wetu hamfanyi hivyo?”

  Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Agnes Kijazi alimweleza Rais kuwa mamlaka hiyo inafanya kazi chini ya kiwango kwa kuwa haina vifaa vya kutosha... “Tuna upungufu mkubwa wa vifaa vya kufanyia kazi na vinapatikana kwa gharama kubwa.”
  Kauli hiyo ilimfanya Rais Kikwete kutaka kujua gharama ya vifaa hivyo huku akihoji inashindwaje kuvipata?

  Aliitaka imshirikishe katika jukumu hilo na kusema yupo tayari kufanya kazi pamoja... “Hivyo vifaa kiasi gani?" Aliuliza Rais na kusisitiza kuwa hakuna ulazima wa kusubiri mtu wa nje kuja kusaidia. Dk Kijazi alijibu kuwa vinauzwa kati ya Sh100 milioni hadi Sh300 milioni ndipo Rais alipoomba ashirikishwe katika kila hatua.

  Katika ziara hiyo, pia Rais Kikwete alitaka ujenzi wa reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma na kuunganisha nchi jirani za Rwanda na Burundi kuanza ndani ya kipindi cha miaka mitano.Alisema ujenzi wa reli hiyo ambao unatarajiwa kugharimu dola za Marekani 5.1bilioni hadi kukamilika, utasaidia kuboresha usafiri na kupunguza uharibifu wa barabara, akisema kitendo cha mizigo mingi na mizito kusafirishwa kwa malori ndiyo sababu ya kuharibika kwa barabara hapa nchini.

  Rais Kikwete aliiagiza Wizara ya Uchukuzi kufufua na kuimarisha Reli ya Tanga hadi Musoma na Kigoma ili kupunguza adha ya usafirishaji mizigo nchini.Pia aliitaka wizara hiyo kuhakikisha kuwa inaimarisha usafiri wa anga kwa kuboresha viwanja vya ndege na kujenga vingine, akitolea mfano wa Mji wa Singida ili kuimarisha sekta hiyo.

  Awali, Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu alisema sekta hiyo ya reli inakabiliwa na matatizo makuu matatu, uchakavu wa Reli ya Kati katika maeneo mbalimbali, uchakavu wa mabehewa na kushuka kwa morali ya wafanyakazi wa shirika hilo.
   
 2. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hapo kuhusu daladala na hata tax mbovu amenena mkuu,wala hajakosea kabisa.
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  katika hilo ni sahihi.....biashara ya daladala bila wao hujaifanya, ujiunge nao au uwahonge....vinginevyo ukiingia ukakuta unawaongezea gari katika njia utaishia kukamatwa wewe kila mara pasipo tija hali magari mabovu yanaendelea na kazi ....utalipishwa faini mpaka ukae chonjo...!
  KWELI ...WAPIGANAPO FAHALI WAWILI ZIUMIAZO NI NYASI....baaada ya sumatra kugundua hili na kuwaingiza majembe ndo kabsaaa.....TRAFIKI NA MAJEMBE WAKAANZA KUSHIRIKIANA KUTOZA FAINI ZA AJABU PASIPO NA KOSA
  TUSEMAPO SERIKALI INAWAJALI WAWEKEZAJI WA NJE NA KUWAPUUZA WA NDANI NI KATIKA SEHEMU KAMA HIZI.....NAOMBA WABADILIKE
   
Loading...