Polisi ukweli wa kupotea dawa za kulevya Mbeya ni upi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi ukweli wa kupotea dawa za kulevya Mbeya ni upi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 16, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Janga la dawa za kulevya bado ni changamoto kubwa nchini hasa kutokana na kuwako kwa taarifa za kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha bidhaa hizo mara kwa mara ambazo ama zilikuwa zinaingizwa nchini kwa ajili ya matumizi, au kwa kupita njia kwenda nchi nyingine.

  Madhara ya dawa za kulevya ni makubwa sana kwa jamii, mbali ya kuleta tamaa potofu kwa wanaojishughulisha nayo kama njia ya kujipatia utajiri wa haraka haraka ambao hauongezi tija yoyote kwa taifa, zimeathiri kwa kiwango kikubwa nguvu kazi ya taifa hasa kundi la vijana.

  Vijana wengi wenye nguvu wakiwa na umri unaostahili kujituma kwa bidii katika kufanya kazi za kuwaletea maendeleo wao wenyewe na taifa kwa ujumla, wamejitumbukiza katika ubwiaji wa dawa hizo kiasi cha kuwapotezea kabisa mwelekeo wa maisha.

  Hawa wamekuwa kama walemavu, hawana nguvu yoyote, wamekuwa watumwa wa bidhaa hizo na mzigo kwa familia na taifa kwa sababu hawawezi kuzalisha si kwa ajili ya mahitaji yao tu, bali hata kwa wale waliotarajiwa wawe msaada kwao.

  Ukipita katika mitaa mingi ya miji yetu, hususan Dar es Saalaam maeneo kama ya Kariakoo, Kinondoni, Magomeni, Temeke, na kwenye mikusanyiko ya watu kama vituo vya mabasi, aghalab vijana walioathirika kwa kubwia dawa za kulevya wanajionyesha wazi. Wamedhoofika, wako hoi na hawana matarajio yoyote ya maisha. Ni watu wa kuhurumiwa sana.

  Pamoja na madhara haya kwa vijana, na kwa kweli jamii ikijua wazi kwamba dawa za kulevya ni hatari, bado waingizaji wakubwa wa bidhaa hizo nchini wamekuwa wakikwepa mkono wa dola mara nyingi, hivyo wanafanikiwa kumwaga janga hilo mitaani ambalo linatafuna nguvu kazi ya taifa hili.

  Ingawa habari za kukamatwa kwa dawa za kulevya kama ambavyo ilitokea Mbeya hivi karibuni, yaani tukio la Kasumulu katika mpaka wa Tanzania na Malawi wiki hii likihusisha kilo tatu za cocaine, na lile la Tunduma la mwaka

  juzi zikihusisha kiasi cha kilo 42 zinaweza kuwa ni za kutisha, pia ni habari njema kwamba walau vyombo vya usalama vina uwezo wa kutambua uingizaji wa shehena hizo nchini na kwa maana hiyo kuzikamata.

  Kwa maneno mengine, ukamataji wa dawa hizi unaelezwa kuwa ni mafanikio kwani kama zisingekamatwa kabisa basi zote zingemwagwa mitaani na madhara yake kwa jamii hasa kundi la vijana, yangekuwa ni mabaya zaidi kuliko inavyoonekana sasa katika mitaa mingi ya miji yetu nchini.

  Kwa hiyo, sisi tunachukua wasaa huu kuwapongeza polisi wote waliohusika na ukamataji wa bidhaa hizi hatari kwa ustawi wa taifa letu, tunawatia moyo waendelee na kazi hiyo ngumu, ya hatari na yenye vishawishi vikubwa.
  Si rahisi sana kwa mtu ambaye hana uhakika wa mlo wa siku kukamata mali ya hatari ya mabilioni ya fedha na

  kuifikisha kunakohusika kama kuna uwezekano wa kupewa kitu kidogo naye afumbe macho kana kwamba hajaona wala kusikia.

  Tunasisitiza kuwa tunawapongeza polisi wanaoshiriki katika operesheni hizi hatari. Ni kazi yenye majaribu makubwa na mazito hasa mtu anapotanguliza shida zake binafsi na kusahau kuwa kama akitimiza wajibu wake sawa sawa basi ataiponya nchi, lakini kama akiacha tu mambo yajiendee kiholela kwa kuwa yeye amenufaika kwa njia moja au

  nyingine, basi ameshiriki moja kwa moja katika kuchimba shimbo dhidi ya ustawi wa vijana na maendeleo ya taifa kwa ujumla wake.

  Hata hivyo, pamoja na pongezi hizi tuna angalizo kubwa hapa, katika matukio yote mawili ya Mbeya, yaani Kasumulu na Tunduma, kiasi cha dawa za kulevya kilichokamatwa kimekuwa na utata mkubwa; Tunduma ilielezwa kuwa kilo 42.3 zilikamatwa, lakini baadaye ikagundulika kuwa kiasi cha kilo nane hivi hakipo; vivyo hivyo Kasumulu kiasi

  kilichodiwa kukamatwa ni kilo tatu, lakini baadaye ikaelezwa kuwa ni kilo 1.8, yaani kilo 1.2 zimeyeyuka hivi hivi. Sisi hatujui nini hasa kimetokea.

  Mwaka juzi polisi walikwenda kuchunguza tukio la Tunduma, lakini hadi leo hakuna taarifa za kiasi kilichohakikiwa ni kipi hasa, na kama kuna waliocheza mchezo mchafu ni akina nani na wamefanywa nini.

  Tunafikiri, si vizuri sana polisi kujiweka katika mkao wa kutuhumiwa tena kwa vitu nyeti kama dawa za kulevya. Ni kwa jinsi hii tunafikiri uongozi wa juu wa polisi sasa unapaswa kuibuka na kueleza ukweli wa matukio haya mawili ya Mbeya.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...