Polisi Tarime wasaidiwa simu 100 - HII IMEKAAJE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Tarime wasaidiwa simu 100 - HII IMEKAAJE?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mukuru, Jul 14, 2009.

 1. Mukuru

  Mukuru Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JESHI la Polisi limepokea msaada wa simu 100 kwa ajili ya kuwasaidia polisi waliopo wilaya za Tarime na Rorya, mkoani Mara kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika maeneo ya mapigano yanayotokea mkoani humo. Msaada huo wa simu ulitolewa jana na mfanyabiashara wa simu za mkononi, Zahoro Khamisi, maarufu kama Matelefone kama mchango wake kwa polisi jamii.

  Akikabidhiwa msaada huo katika makao makuu ya Polisi, Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kwa niaba ya jeshi hilo, alisema Matelefoni amekuwa mdau muhimu katika kulisaidia Jeshi la Polisi na matukio mbalimbali ya kijamii.

  Alisema mwaka huu katika kipindi cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), Matelefoni alitoa simu 350 kwa ajili ya mawasiliano kwa walemavu hao, ili kurahisisha kutoa taarifa pindi wanapomuona na kumjua mhalifu.

  "Kwa kuwa aliguswa na mauaji hayo na jana alitoa simu 100 zenye thamani ya sh milioni 4.5 kwa ajili ya kuwasaidia polisi waliopo Tarime na Rorya kutekeleza majukumu yao ipasavyo," alisema Kova.  ...................................................................................................  :confused:...Najua misaada ni mizuri ila nakuwa na wasi wasi vyombo vya serikali vinapopatiwa "misaada" na watu binafsi ikiwemo wafanya biashara. Ninadhani hii inaweza kuathiri utendaji wao kwa kuwafumbia macho hao 'watoa misaada'...ni mtazamo wangu. WanaJF, nyie mwaonaje?
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Unaweza ukawa msaada kweli ama ni malipo ya fadhila .Angalieni huko Bank nk cheque zinapitaje maana hawa jamaa bwana si mchezo
   
 3. M

  Mageta Opanga Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Kuna ukweli na mashaka kwenye mtizamo wako.
  Mie mimacho tu.

  Walakini,

  Inaeleweka kuwa eneo hili limekumbwa na matatizo makubwa na mawasiliano yamekuwa hafifu...au hakuna kabisa.

  Nafikiri apongezwe

  Huo msaada utasaidia kwa njia moja au nyingene
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mzalendo akitoa msaada anatiliwa shaka ,haya subirini wazungu wawape misaada na karatasi za mikataba ikifuatilia nyuma yake mtie saini.
  Kuna nchi moja huwa kila baada ya miaka fulani huwakusanya matajiri wake na kuwauliza wameifanyia nini nchi yao ,au wameisaidia kitu gani ? Kama ni kujenga barabara au zahanati ,sasa hapa jamaa ametoa imekuwa tena wananchi wahapa Jf wanaanza wasiwasi ,jamani kuna msemo kuwa sadaka huanzia nyumbani au akipeleka msaada huo nchi jirani mtasemaje ? Ila sheria itafuata mkondo wake kama akikamatwa.
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Typical init?

  mlitaka wapewe simu moja kisha wote washare


  halafu watu wakiposti habari ambazo hazina maana mnalalamika

  hivi kweli how can one have a serious debate na vichwa kama hivi?

  Kule watu wanapigana na kuumizana wewe polisi kupewa simu hupendi...angewapa Mbowe usingeona tatizo
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  GT,m
  You must have an obsession with Mbowe. Get a life!
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kantapeli unless amwambie Chale anilipe
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Then take it up with him privately. Tuendelee kujadilia ya maana hapa JF.
  Actually tatizo la Tarime needs more than just 100 cell phones. The government needs to involve itself more than it has done so far even if it means using a hammer. Ndugu zangu wa Tarime wanaelewa na kuheshimu the use of power. The police needs transportation and they need to be beefed up in the troubled areas. And the trouble makers need to be locked up.
   
 9. L

  Lemi New Member

  #9
  Jul 15, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Just a thought, pesa za vocha zitawagharimu kiasi gani kwa mwezi.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hii ni kampeni ya Sheikh Saidi Mwema ya "Polisi Shirikishi" na "Polisi Jamii", kusema kweli ni vizuri sana kwa Sheikh Saidi kuweza kushirikisha raia waisaidie Polisi kuwasaidia.

  Mtaani kwetu tumeanza mchango wa kapiki piki kakusaidia Patrol za usiku, na tunashukuru kuna watu wenye zao na watakao ulinzi, wame-pleji piki piki zaidi ya moja.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  bora misaada ya wafanyabiashara wa ndani, ya wazungu ndo inakuja na ndoana kubwa!

  GT umesema kweli, msaada ungetolewa na chadema hapa wala usingesikia watu kulalamika.

  waacheni raia watoe msaada kwa nguvu zao walizonazo..........
   
 12. D

  Damas Member

  #12
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  je akifanya makosa polisi hawatamwonea aibu?
   
 13. D

  Damas Member

  #13
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Polisi wanapokea misaada toka kwa wafanya biashara hii ni udhaifu fulani wakifanya makosa watafumbiwa macho
   
 14. D

  Domisianus Senior Member

  #14
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la Tarime ni tata na lina siri nzito sana zaidi ya ambavyo polisi wanafikiri, inabidi serikali ihakikishe kuwa inachukulia uzito wa aina yake na sityo vinginevyo na siasa isije ikaingizwa katika kushughulikia matatizo ya wana tarime, la sivyo tutakuwa hatujafanya lolote zaidi ya kupokea hizo simu na kuzitumia kwa matumizi binafsi, turudi nyuma tuangalie haya matatizo yameanza lini, je ni kweli kwamba miaka ya nyuma haya matatizo hayakuwepo , la hasha, matatizo ya huko ni sugu na ni ya muda mrefu.
  Moja ya mkakati mkubwa na ambao ungeweza kuliondoa hayo matatizo, ni kuwa na program maalum ya watoto weto kusoma mpaka form four ndo iwe darasa la saba,matatizo yataisha yenyewe na wala hata polisi hatakuwa na kazi tena huko, tatizo ni elimu na kutojua madhara ya migogoro ambayo haina maana yoyote.
   
Loading...