Polisi Tarime na Rorya yagundua ekari 20 za mashamba ya bangi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya imegundua Ekari 20 za mashamba ya bangi, yakiwemo magunia 40 ya bangi kavu katika oparesheni kali ya kupambana na kilimo na biashara ya dawa za kulevya inayoendelea Wilayani Tarime Mkoani Mara.

Chanzo: Radio one

bangi.jpg
 
Marekani na nchi zinginezo za Ulaya bangi ni zao linalolipa sana na limehalalishwa. Ukubwa wa mashamba tunayoshuhudia hapa ni wazi hata hapa huenda linalinda uchumi wa watu wengi sema hawana TIN za biashara hiyo.

Badala ya kuhangaika hivi ni bora tungetafakari kwa umakini wazo la Mheshimiwa Mbunge, tena badala ya kuwatafutia zao mbadala tuangalie jinsi ya kuhalalisha hili hili na kudhibiti matumizi yake badala ya kuchoma moto.
 
Mkuu unatulisha matango pori, Ulsya hawajaruhusu kulima bangi ila ukikamatwa nayo kidogo unaweza kuwaambia polisi ni kwa matumizi yako binafsinavwakakuacha. Kwa wagonjwa wanaotumia kupunguza maumixu wanna kibali cha dr
 
Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya imegundua Ekari 20 za mashamba ya bangi, yakiwemo magunia 40 ya bangi kavu katika oparesheni kali ya kupambana na kilimo na biashara ya dawa za kulevya inayoendelea Wilayani Tarime Mkoani Mara.

Chanzo: Radio one

Waache upumbavu!Unagundua kitu ambacho kipo na ulitegemea kukiona?Waseme wameona.Shitholes.Something big has gone!
 
Kule kunahitaji doria ya helcopter, na uteketezaji wake watafute mashine ya kuvunia (harvester) imbayo inakuwa imetegenezewa kifaa cha kuchoma mpaka majivu (incinerator) tofuti hao wana usalama wanaoteketeza hawataweza kufikia maeneo yote na huo moshi wanaochoma kienyeji utawaathiri
 
Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya imegundua Ekari 20 za mashamba ya bangi, yakiwemo magunia 40 ya bangi kavu katika oparesheni kali ya kupambana na kilimo na biashara ya dawa za kulevya inayoendelea Wilayani Tarime Mkoani Mara.

Chanzo: Radio one

Hili litakuwa shamba la yule mbunge wa zamani wa CCM ambaye alikuwa anasifikana kuvuta bangi kabla ya kuingia bungeni kulala.
 
Mkuu unatulisha matango pori, Ulsya hawajaruhusu kulima bangi ila ukikamatwa nayo kidogo unaweza kuwaambia polisi ni kwa matumizi yako binafsinavwakakuacha. Kwa wagonjwa wanaotumia kupunguza maumixu wanna kibali cha dr
Hapo kwenye underline/bold ndio maana ya nikasema tufikirie upya na mradi Mh. Mbunge keshaomba lijadiliwe ni bora wanaweza kufikia mwafaka. Hiyo ni pamoja na kusema labda mkulima lazima awe na kibali kutoka mamlaka husika, mtumiaji ajulikane anatumia kwa malengo gani kama ilivyo kwa vileo haviruhusiwi kwa chini ya miaka 18 hata kama una pesa ya kununua.

Unafikiri hizo stress na magonjwa yanayopelekea wazungu waruhusiwe na madaktari sisi huku hayapo!? Au hayo 'matumizi binafsi' hapa Tanzania au Africa hatuna!

Siku nyingine tukumbuke tu kuwa mkulima wa kijijini anayevuta bangi kwa sababu zake binafsi na kiongozi wa umma anayesababishia nchi hasara ya trillion mbili ni nani mbaya zaidi kwa maendeleo ya nchi.
 
Namchukia George Marato. Mara chache anaweza kuripoti tukio la wananchi kukosa haki ila mara nyingi hua anaripoti negative side ya wana tarime. (Sio kwamba nafurahia maovu)
 
Tunaoumia ni sisi walaji.sasa unapoteketeza shamba la ekari ishirini unasababisha deficit sokoni.wanashindwa kupambana na bandari bubu (ziko zaidi ya 60 )zinazoingiza tani kibao kila wiki za heroine na cocaine kutoka udosini na umangani wanashadadia zao la biashara la wanyonge.shenzi kabisa
 
Back
Top Bottom