Polisi Tanzania walalamikia UDUNI wa makazi yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Tanzania walalamikia UDUNI wa makazi yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Jan 9, 2011.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Source:Gazeti la Habari leo(January 8,2011)

  ASKARI Polisi wameiomba Serikali kuangalia jinsi ya kuboresha nyumba wanazoishi walinzi hao wa Usalama wa raia kutokana na kile walichodai zimechakaa kupita kiasi na kwamba hali ya sasa haioneshi kuwa zinafaa kukaliwa na binadamu.

  Askari hao wanaoishi kambini walieleza kwamba nyumba hizo kwa sasa zilizo nyingi katika makazi yao kuta zake zimepasuka, vyoo vyake vimebomoka na hivyo kutishia usalama wa afya zao.

  Wakizungumza na gazeti hili , baadhi ya askari ambao hawakutaka kuandikwa majina yao walisema kwamba wameamua kuzungumzia hilo kutokana na hali halisi ya mazingira wanayoishi kambini humo, kitendo ambacho wamekielezea kuwa kinawakosesha raha.

  Walieleza kuwa, kutokana na uchakavu wa nyumba hizo zilizojengwa karibu miaka 80 iliyopita, enzi za ukoloni, kuna kila sababu ya kuzifanyia ukarabati mkubwa, au kuzibomoa na kujenga nyingine.

  “Kama ulivyoshuhudia tu mwenyewe mwandishi wa habari, sisi ndo tunaishi katika mazingira haya, inasikitisha sana,” alisema mmoja wa askari hao aliyeongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, baadhi ya askari wanalazimika kupanga uraiani ili kuepukana na adha ya mazingira ya sasa na pia udogo wa nyumba hizo.

  Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Barlow amekiri kuwepo kwa makazi duni kwa askari wake na kuielezea hali hiyo kuwa ni moja ya changamoto zinazolikabili Jeshi hilo muhimu kwa usalama wa raia na mali zao.
   
 2. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Wajinga hao ndio wanatumika kama kondom; wanalalamika nini sasa, wao ni mbwa wa ulinzi sio askali wa amani ndio maana wanapiga watu mabomu
   
 3. S

  Siao Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni wale polisi wa arusha ambao hawana tofauti yeyote na wanyama kwa kuumwa wenzao, wanapaswa waishi porini na wanyama wenza.

  Polisi wanajidhalilsiha wenyewe .. itachukua muda sana kuonyesha polisi ni mtu mwenye akili timamu. Yaani sasa inaonekana kama polisi ni mtu mendawazimu, maana ukiambiwa umuuwe mtu asiyekuwa hata na fimbo, na kweli ukamuua, wewe kweli ni kama papai kabisa.

  Ni aibu sana kwa polisi kuonekana kama watu ambao vichwani ni uji tu umejaa. Itawachukua polisi muda mrefu sana kuonyesha ni watu muhimu kwa jamii na kuwa wanastahili kutumia fedha za walipakodi kuboresha maisha yao.

  Sasa kama polisi hawafanyi chochote, ila kuuwa watu tena wasikuwa na hatia (maana sio walimwingza meya kazini kwanguvu) - sasa wapigwe na baridi kidogo watapa akili.

  neno polisi ni neno baya kwa sasa mpaka harufu chafu ipungue!
   
 4. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Waacheni wakae hukohuko mpaka akili zitakapo wakaa vizuri.
   
 5. R

  RMA JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli polisi wamebanana katika vijumba vibovu mithili ya panya katika shimo! Lakini cha ajabu wanawapiga mabomu hata watetezi wao! Kwa ufinyu wa mang'amuzi na elimu duni, hata hawana habari kwamba mapambano dhidi ya ufisadi ni kwa ajili ya maslahi yao pia. Waendelee tu kuishi huko hadi watakapopata akili!
   
 6. m

  mzalendo2 Senior Member

  #6
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  na bado, tukipata nafasi hata kukuueni tutafanya, wahuni nyie
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Umejitahidi kuchagua maneno ya kistaarabu kuchangia thread hii. Kuwalinganisha askari na condom kuna ukweli ndani yake.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Unajua mbwa tangu lini akalala ndani ya makazi? kulinda alinde nani sasa? (joke)
   
 9. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  full suti za mabati
   
 10. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hao polisi sidhani kama wanahitaji nyumba,watakuwa wanatania,toka lini mbwa anaishi ndani ya nyumba si inatakiwa akae bandani na wao si wanaishi mabandani sasa nini cha zaidi?POLISI wetu hawatofautiani na mbwa pia hata mbwa anaakili kwani akiambiwa kamata mtu huwa anaangalia hali ya hewa.Hawa ni hayawani.
   
 11. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  ndo maana ya asjari. waishi tu kama ilhvym. hatuna bajeti kwa sasa. kwany hawazlishi kama tra. kazi kupiga mabomu mabosi zao kwa maana ya wananchi. hatutaki kuwajengea makazi mapya tena aroo.
   
 12. Wameiba Kura

  Wameiba Kura JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani mlinzi analala, sasa kazi yake ni nini? wakae MACHO hadi wakome
   
 13. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatuna mapolisi tanzania,hao wanaolalamika ni wa nchi gani?
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  we hujui kuwa mbwa wanahesabika kuwa ni partya familia?nchi za mbele huko lakini
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  ya vasco da gama
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Miaka nenda miaka rudi tuliona hawa polisi wakiteseka kwa makazi duni, ni baada ya JMK kushika madaraka tumeona mishara yao ikipanda maradufu na majumba mapya ya kisasa ya polisi yakiendelea kujengwa kila siku. Jee, hamuyaoni? na yataendelea kujengwa mpaka ihakikishwe kuwa hakuna shida ya nyumba kwa walinda usalama wetu.
   
 17. W

  We can JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani POLISI wetu wamegawanyika makundi mawili au zaidi. Kuna walioupande wa wananchi wanyonge na kwamba dhamira zao zinawaambia kuwa kupiga mtu asiye na kosa ni kuandaa bomu ambalo litakulipukia wewe mwenyewe no later than soon. Utakuta mapolisi hawa hawapewi vyeo kwa muda mrefu hata kama wanastahili.

  Lipo kundi lingine la wale waliochukuliwa kwa undugu au waliokotwa mtaani (wakivuta bangi). Hawa hawajui kwamba hawajui. Kwa maneno mengine ni WAPUMBAVU. Hawa ndo wanaolidhalilisha Jeshi la polisi. Ni vihelehele, na hujipendekeza kwa lolote lile. Niaminivyo mimi hata JWTZ hali yaweza kuwa hivyohivyo.....
   
 18. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 271
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 45
  kaza buti JK mpaka wapewe mahema
   
 19. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Zombe;

  When was a last to time to go to see your Psychiatrist?
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  kwani wakifyatua risasi za moto na kuuwa raia huwa hawapandishwi vyeo?
   
Loading...