tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,851
Zifuatazo ni double standards za Polisi Tanzania:-
1. Kutawanya Mikutano ya Vyama Vya Upinzani Vs Kulinda Mkutano wa CCM.
Hivi karibuni Jeshi la Polisi lilipiga marufuku Mikutano yote ya Vyama Vya Siasa, ikitumia nguvu kutawanya na kukamata viongozi na wafuasi wa vyama vya Upinzani, kwa kiisingzio cha figisu figisu za kintelijensia, eti zimegundua hili Mara lile. Ikiwemo mpaka kuzuia mahafali ya ndani ya Ukumbi ya Wanavyuo wa Vyama Vya Upinzani. Wakati huo huo Polisi nao nao wako Dodoma wakipiga gwaride kwa kodi za Watanzania, kulinda na kufanikisha Mkutano wa CCM! Tena wakiachia mahafali ya wanachuo wafuasi wa CCM. Huu ni Ukaburu.
2. Kauli ya Gwajima Vs Kauli ya Bulembo.
Gwajima alitoa kauli kwamba kuna watu wamejipanga kukwamisha JPM kuwa Mwenyekiti wa CCM, Polisi wakazingira nyumba yake na juzi juzi wamemkamata. Bulembo nae katoa kauli hiyo hiyo, kwamba kuna watu wanakwamisha JPM kuwa Mwenyekiti. Polisi mpo kimya na hamjazingira nyumba ya Bulembo. Na Bulembo yupo huru kitaa.
Double standards za namna hii zinalishushia Heshima Jeshi la Polisi.
Cc: JPM
IGP