Polisi Tanzania: Hatutegemei kuona sherehe za Pasaka wakati Nchi bado ipo kwenye maombolezo

Jeshi la polisi nchini limewataka waumini wa dini ya Kikristo na Watanzania wote kusherehekea sikukuu ya Pasaka huku wakikumbuka bado Taifa liko katika siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime amesema, Jeshi hilo halitarajii kuona sherehe na shamrashamra kama ilivyozoeleka kila inapofika sikukuu hiyo, lengo likiwa ni kuendelea kuomboleza kifo cha kiongozi huyo.

Amesema Jeshi la Polisi nchini limejipanga vizuri kuhakikisha Waumini wa dini ya Kikristo wanashiriki ibada ya Ijumaa Kuu, ibada ya mkesha wa Pasaka siku ya Jumamosi na Ibada ya Pasaka siku ya Jumapili katika mazingira ya amani, utulivu na usalama na Wananchi wengine wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Ameziomba kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada na sehemu zingine kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini katika suala zima la kudumisha amani, ulinzi na usalama.

Msemaji huyo wa Jeshi la Polisi Nchini David Misime, pia amewahakikishia Watanzania wote kuwa hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari, ingawa kuna matukio machache ya kiuhalifu wa kijinai na ajali za barabarani, mambo yanayoendelea kushughulikiwa.

Polisi wetu hawana Mungu.Mungu wao amekufa!
Wanatuonea wivu tukishangilia ushindi was Kristo kushinda mauti
 
Ilikuwa ni huzuni kuliko huzuni zote Yesu mwokozi alipokufa.

Sasa ni furaha zaidi ya furaha zote masihi Yesu anapofufuka.

Tuachane na wanaopambania vitu vya duniani(Jeshi la Polisi),hawajui walitendalo.

Hiyo siku tufurahie zaidi ya furaha zote,maana Yesu yu hai.

Natoa onyo kwa hao jeshi la polisi na wengineo,
Wasijitafutie laana ya bila sababu.

Na iwe hivyo.
 
Wewe unaohimiza watu na wale wanaokataza watu wote ni wale wale tu.....

Kupangiana maisha ni Udikteta kila mtu afanye anachopenda ilimradi asivunje sheria...., Na kama kuna Sheria ipo inayomkataza mtu kufanya kile anachopenda iwapo anachopenda sio bughuza kwa wengine (anti social behaviour) basi sheria hii haifai...

Kwa hili Jeshi limekosa Busara na Hekima..., na kwa wale watakao politicise ukosaji huu wa Busara watakosa Hekima
 
Jeshi la polisi nchini limewataka waumini wa dini ya Kikristo na Watanzania wote kusherehekea sikukuu ya Pasaka huku wakikumbuka bado Taifa liko katika siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime amesema, Jeshi hilo halitarajii kuona sherehe na shamrashamra kama ilivyozoeleka kila inapofika sikukuu hiyo, lengo likiwa ni kuendelea kuomboleza kifo cha kiongozi huyo.

Amesema Jeshi la Polisi nchini limejipanga vizuri kuhakikisha Waumini wa dini ya Kikristo wanashiriki ibada ya Ijumaa Kuu, ibada ya mkesha wa Pasaka siku ya Jumamosi na Ibada ya Pasaka siku ya Jumapili katika mazingira ya amani, utulivu na usalama na Wananchi wengine wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Ameziomba kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada na sehemu zingine kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini katika suala zima la kudumisha amani, ulinzi na usalama.

Msemaji huyo wa Jeshi la Polisi Nchini David Misime, pia amewahakikishia Watanzania wote kuwa hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari, ingawa kuna matukio machache ya kiuhalifu wa kijinai na ajali za barabarani, mambo yanayoendelea kushughulikiwa.

Hapa ni tofauti za mtazamo, serikali haina dini hivyo Pasaka haimo kwenye katiba, wananchi wana dini hivyo kila mtu atulie kivyakevyake.
 
Hapa ndio uwa naona jeshi la polisi wamejaa waseng.e umo, unawezaje kutamka kauli kama izi kwa taifa kama hili ambalo tumeishi bila udini kwa kiasi kikubwa? Aisee uyu mtu avuliwe madaraka yake yote hawa ndio chanzo cha udini.
 
Tatizo lingine kubwa la polisi letu ni

ELIMU ELIMU ELIMU.

Form 4 + miezi 6 ya Depo+viseminasemina(short courses)

Haitoshi mno kwa kazi kubwa hii ya kulinda raia na mali zao.
 
Hao ni wale wanataka matendo ya jiwe yaendelee kuishi.
Hawashtuki kuwa kuna teuzi na tengua teuzi zinaendelea.
 
Back
Top Bottom