Polisi Tanzania 1-1 Yanga SC | Sheikh Amri Abeid Stadium | VPL

Jane Lowassa

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,756
8,493
Yanga leo wanarusha karata yao nyingine baada ya kipigo cha mbwa koko pale Tanga.

Updates za mechi hiyo zipate hapa.

=======
VIWANJA VINGINE

FT: Mtibwa Sugar 0-2 Gwambina

FT' Coastal Union 0-0 KMC


=======

00' Mpira umeanza

17' Yondani anamuangusha Fiston nje kidogo ya box na kuwa mpira wa adhabu ndogo, mpira huo unashindwa kuzaa matunda kwa Yanga

19' Tuisila Kisinda anajaribu kulikaribia lango la Polisi lakini Yondani anakwamisha juhudi zake na kuzaa kona isiyo na faida kwa Yanga

25' Niyonzima almanusura aandike bao la kwanza kwa Yanga baada ya mabeki wa Polisi Tanzania kudhani Tuisila yuko 'offside'

29' Kassim anatandika shuti kali linaloguswa na golikipa wa Yanga na kugonga mwamba wa juu, Polisi Tanzania 0-0 Yanga

35' Ditram Nchimbi na mlinda mlango wa Polisi Tanzania wako chini baada ya kujaribu kuwania mpira wa juu

41' Fiston anaweka bao kwa kisigino baada ya pasi maridhawa kutoka kwa Haruna Niyonzima

45' Dakika mbili zimeongezwa

45+2' Mpira Mapumziko

61' Kaseke anaingia kuchukua nafasi ya Ditram

63' Polisi Tanzania wapata kona pacha lakini zote hazijatoa matokeo

64' Nassor Maulid anajaribu shuti la mbali lakini mprira unatoka nje kidogo ya lango la Yanga

68' Kelvin Yondani anapewa kadi ya njano kwa kumuangusha Abdulrazk

70' Kibwana Shomari anapewa kadi ya njano

71' Deusdedit anaingia upande wa Polisi Tanzania

78' Polisi Tanzania wanakoswa koswa baada ya Yanga kuwashambulia kwa nguvu

87' Kadi nyekundu kwa Kelvin Yondani baada ya kupewa kadi ya pili ya njano

89' Polisi Tanzania wanasawazisha kupitia kwa Pius Buswita, Polisi Tanzania 1-1 Yanga

90+2' Mpira umekwisha
 
Kwahiyo kwa sababu ulibahatisha matokeo ya mechi ya Alhamisi unasahau kuwa leo ni J'pili. Tunashinda Leo goli 2.
 
Game hii Yanga atashinda, kwa afya ya mchezo wa soccer Tanzania.

Itabidi namna ifanyike.
 
Yanga leo wanarusha karata yao nyingine baada ya kipigo cha mbwa koko pale Tanga.

Updates za mechi hiyo zipate hapa.

Utabiri wangu: Polisi Tanzania 1- 0 Yanga SC.

Mwenye macho na aone!
Nakuaminia sana dada yangu tatizo tu wewe ni CCM
 
Back
Top Bottom