Polisi tafuteni pa kujificha au kujifichia

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,930
3,803
Tunaelewa mnamuogopa muajiri wenu aliepo ingawa sheria haziwafungi mpaka mnavuka mipaka ya kazi zenu badala ya kuilinda serikali mnakilinda chama cha CCM. Tunajua kura ni siri.

Sawa kuweni huko japo kura ni siri ,mbali ya kufanya yote hayo jificheni katika mambo ya aibu wanayoyafanya CCM,mfano yule mtu mzima aliemtukana Maalim Seif matusi ambayo nina hakika Mgombea Uraisi wa CCM kwa upande wa Zanzibar hakuyafurahia na inasemwa kuna mambo mengi hayafurahii,lakini waliomzunguuka hana nguvu nao kwa sasa,inakuwa anafuata mkumbo tu. Yule mzee mungelimkamata kwa kutumia lugha chafu sana mbele ya jamii ,mngekuwa mmejificha japo kidoogo.

Kubandua bendera na picha za vyama na wagombea wengine ,wafuatilieni mumkamate japo mmoja,wanaorushia mawe wapinzani wanapopita na wagombea wa CCM watieni mkiki mkiki ndio kujificha kwenyewe huko.

Isiwe mnawakandia walioupinzani kwa sasa,jificheni kwenye vitendo viovu vilivyo dhahiri vinavyofanywa na CCM,angalau mjisitiri maana kubwa lijalo mtakuwa na pa kujifichia.
 
Back
Top Bottom