Polisi Tabora waua majambazi watano


jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Messages
295
Likes
12
Points
0
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2010
295 12 0
Victor Kinambile, Tabora

POLISI mkoani Tabora, wamewaua watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kufanikiwa kukamata bunduki aina ya SMG, magazine tano, risasi 165 na bomu la kutupa kwa mkono.
Kwa mujibu wa Kamanda Polisi wa Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow, tukio hilo lilitokea juzi katika eneo la Kazima, umbali wa kilometa tano kutoka Tabora mjini, katika barabara kuu ya Tabora-Nzega.

Alisema kuuawa kwa watu hao, ni matunda ya ulinzi shirikishi unaofahamika kama Polisi Jamii.

Alisema watu hao walikuwa na mpango wa kuteka magari, lakini waligundua mpango huo na kutoa taarifa polisi.

Alisema polisi walizifanyia kazi taarifa hizo na kufanikiwa kuwakuta vijana hao, wakiwa wameweka mawe barabarani. wakisubiri malori yanayotoka mnadani kuelekea Tabora mjini.

Barlow alisema polisi walipofika katika eneo vijana waliaanza kuwarushia risasi, jambo lililowalazimisha askari, kujibu mapigo na kufanikiwa kuwaua watano ambao hata hivyo, hawajatambuliwa.

Alisema miili ya vijana hao, imehifadhiwa katika Hospitali ya mkoa wa Tabora, Kitete huku mamia ya wakazi wa mji wa Tabora, wakienda katika hospitali hiyo, kuwatambua watu hao.

Vijana waliouawa wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 20 hadi 25 na kwamba baadhi yao wanadhaniwa kuhusika katika matukio ya ujambazi, yaliyotokea katika Mkoa wa Tabora na mikoa ya jirani.

Kamanda alisema vijana watatu walipigwa risasi kifuani, mmoja kwenye tumbo na mwingine mgongoni.


Aliwashukuru wananchi kwa kushirikiana na polisi na kufanikiwa kuwadhibiti watu hao.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Gama

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
9,874
Likes
1,712
Points
280
Gama

Gama

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
9,874 1,712 280
Wana jf waliopo tbr tupeni ukweli maana saa nyingine unaweza kukuta habari hii inaukweli finyu.
 
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Messages
295
Likes
12
Points
0
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2010
295 12 0
Wana jf waliopo tbr tupeni ukweli maana saa nyingine unaweza kukuta habari hii inaukweli finyu.
Wewe GAma unataka Ukweli upi tena na ushahidi huo hapo Bonyeza hapo palipo andikwa Chanzo utapata Ukweli wa Mambo Acha uzito wa kusoma magazeti Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
mpenda pombe

mpenda pombe

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
1,255
Likes
441
Points
180
mpenda pombe

mpenda pombe

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
1,255 441 180
Ni habari ya kweli...
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,975
Likes
5,344
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,975 5,344 280
Ni habari ya kweli...
Mpaka imetoka katika Gazeti ni habari ya kweli unataka iwe habari ya uongo hao Polisi siku hiz kazi yao kuuwa Majambazi
 

Forum statistics

Threads 1,235,549
Members 474,641
Posts 29,226,540