Polisi Tabora waanza kuchunguza matukio ya watu kujinyonga

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Jeshi la Polisi Mkoani Tabora limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina wa ili kubaini chanzo cha matukio ya watu kujinyonga ambapo baadhi yao wengine wanakutwa na majeraha mbalimbali mwilini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Issa, amesema kuwa uchunguzi huo unafanyika baada ya kuwepo kwa dalili huenda watu hao wanauwa na kisha kuning’inizwa ili waonekane kama wamejinyonga.

Kamanda Issa ameyasema hayo akiwa katika eneo la Tukio la Mtaa wa Msikitini Kiloleni Mjini Tabora ambapo mkazi mmoja wa eneo hilo aliefahamika kwa jina moja la Musa amekutwa amejinyoga kwa kutumia kipande cha kitenge.

Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora amesema tukio hilo ni la tatu ndani ya wiki moja jambo ambalo limewashtua na kuamua kufanya uchunguzi ingawa hadi sasa amesema ni vigumu kusema moja kwa moja kuwa watu hao wameuawa.

Ameongeza kuwa katika tukio hilo mwili wa marehemu umekutwa na damu na michubuko chubuko hivyo polisi kwa kushirikiana na madaktari wanafanya uchunguzi ili kutoa ripoti kamali na kusema endapo ikibainika ameuawa basi wauaji watatafutwa na kuchukulia hatua kali.

Kamanda.jpg
 
Back
Top Bottom