KIDUDU
JF-Expert Member
- Sep 17, 2012
- 2,554
- 1,920
Wakuu salaaam.
Nimepita Tabora nikakaa kama wiki moja na nusu. Nimekuta changamoto kubwa ya Polisi wale wanaotembea na pikipiki maarufu kama tigo, wanakamata pikipiki kila sehemu hata kama imepaki, yaani wanatafuta makosa kama huna kabisa watakuuliza barakoa ipo wapi.
imekuwa ni kwero kubwa kabisa, kwa bahati mbaya hata faini hawaandiki ili ulipe iende serikalini, wanachukua elfu 10 nyingi za boda boda na wanaweka mfukoni, Ni wazi RPC anajua hili maana wanafanya kwa kujiamini kabisa, yaani wana usumbufu usio na kikomo, kwanza wanakuwa wamelewa yaani ni shida sana.
Naomba mamlaka husika waliangalie hili, kwa maana imezidisha uhasama kati ya polisi na raia pale mboka.
Mamlaka chukueni hatua, huu unyanyasaji umekithiri.
Wasalaam