Polisi Tabora iangaliwe

KIDUDU

JF-Expert Member
Sep 17, 2012
2,563
2,000
Wakuu salaaam.
Nimepita Tabora nikakaa kama wiki moja na nusu. Nimekuta changamoto kubwa ya Polisi wale wanaotembea na pikipiki maarufu kama tigo, wanakamata pikipiki kila sehemu hata kama imepaki, yaani wanatafuta makosa kama huna kabisa watakuuliza barakoa ipo wapi.

imekuwa ni kwero kubwa kabisa, kwa bahati mbaya hata faini hawaandiki ili ulipe iende serikalini, wanachukua elfu 10 nyingi za boda boda na wanaweka mfukoni, Ni wazi RPC anajua hili maana wanafanya kwa kujiamini kabisa, yaani wana usumbufu usio na kikomo, kwanza wanakuwa wamelewa yaani ni shida sana.

Naomba mamlaka husika waliangalie hili, kwa maana imezidisha uhasama kati ya polisi na raia pale mboka.

Mamlaka chukueni hatua, huu unyanyasaji umekithiri.

Wasalaam
KIDUDU
 

KIDUDU

JF-Expert Member
Sep 17, 2012
2,563
2,000
Acha majungu wewe mbuzi wa kafara. Kwa hiyo ilikuwa ukiwafuata kila sehemu walizopita!!
Yaani mpaka nimecheka, mimi ni mbuzi? JF yenyewe umejiunga 2017, leo unamuita binadamu mwenzio mbuzi? kwani ungeacha ku comment ungekufa?
Acha majungu wewe mbuzi wa kafara. Kwa hiyo ilikuwa ukiwafuata kila sehemu walizopita!!
 

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
15,325
2,000
Hizi TAKA-TAKA zisizo jielewa kwenye hili Taifa ndo zinatuchelewesha!,Mwenzio analeta hoja yenye maana kwa vijana wa Tabora kwa namnà wanavyosumbuliwa na kunyanyasika,wewe unaleta UWENDAWAZIMU WAKO!!,ZERO KABISA!!
Umeona eennhh???!!;
 

Hanitoni

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
1,153
2,000
Nikweli kabisa vijamaa vinakera Sana vinawapiga Sana hela bodaboda badae jioni vinaenda zero pub kutumbua uhalamia wao
 

agprogrammer

JF-Expert Member
Dec 7, 2015
467
500
Tunahitaji mabadiliko katika taasisi zetu watu wafanye kazi kama mikataba yao inavyowataka ndo tutaweza kusonga mbele. Muda ndo huu wakufanya mabadiliko.
 

Peter Mabala

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
1,071
2,000
Kuna eneo wanakaa na rungu wanasimamisha boda boda, ole wako usisimame

Ni kule kwenye nchi ya wagerasi.
 

Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
937
1,000
Askari wote wanaopewa Vyombo vya moto,Kama gari na pikipiki,Lazima wapeleke hesabu kwa mabosi wao,Kama ilivyo kwa Daladala drivers.Kwa maana hiyo Ma RPC, RTO pia Takukuru wanajua,.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom