Polisi Songea wazuia maandamano ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Songea wazuia maandamano ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 10, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Polisi Songea wazuia maandamano ya CHADEMA


  na Stephano Mango, Songea


  [​IMG] JESHI la Polisi wilayani hapa limezuia kufanyika kwa maandamano ya amani yaliyoitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yenye lengo la kupinga uamuzi wa mkuu wa wilaya hiyo, Thomas Oley Sabaya, wa kuwanyima vocha za pembejeo wakulima wa kata tisa, kati ya hizo tano zinaongozwa na chama hicho.
  Kata zilizonyimwa vocha ni kati ya 21 na sababu ya mkuu huyo wa wilaya kufikia uamuzi huo hazijajulikana.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za chama hicho zilizoko Mfaranyaki mjini hapa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime alisema kuwa CHADEMA wilaya ya Songea walipanga kufanya maandamano ambayo yalikuwa na madhumuni ya kupinga uchakachuaji wa vocha za pembejeo za wakulima uliofanywa na mkuu huyo wa wilaya.
  Fuime ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mjini kupitia CHADEMA alisema taarifa ya kufanya maandamano hayo ilitolewa tangu Januari 7 mwaka huu na mkuu wa polisi wa wilaya ya Songea.
  Lakini alishangazwa kuona mkuu huyo wa polisi akidai kuwa tatizo la wakulima kunyimwa vocha linashughulikiwa na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk. Christine Ishengoma
  Alisema pamoja na polisi kuzuia maandamano hayo kupitia barua yao iliyowafikia jana na kusainiwa na OCD Peter Kubezya yenye kumb,Na,SO/A.3/6/54 CHADEMA imeruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara ambao ulifanyika kwenye soko la samaki la zamani karibu na Shule ya Msingi Mfaranyaki
  Alieleza sababu zilizotolewa na OCD Peter Kubezya ni dhaifu na zilizozeeka na kwamba mkuu wa mkoa Dk. Ishengoma alipaswa kuchukua hatua za haraka kuwakomboa wakulima toka pale tatizo lilipojitokeza Desemba 15 mwaka jana.

  Alisema tukio hilo lililofanywa kwa makusudi na DC Sabaya ambapo maamuzi ya ajabu ya kukiukwa kikao cha wadau wa kilimo kilichofanyika Novemba 12 mwaka jana kiliazimia kuwa wakulima wa kata za Manispaa ya Songea wakachukulie vocha za mbolea ya ruzuku kwenye maeneo yao wanayoishi ambapo kuna kamati za pembejeo za kata ambazo zinawafahamu wakulima husika.
  Fuime alisema polisi wanapaswa kulinda raia na mali zao na kwamba hawapaswi kutumia uwepo wao kuwadhulumu wananchi haki zao ikiwemo ya kupewa mbolea katika kata zinazoongozwa na madiwani wa CHADEMA za Mjini, Lizaboni, Majengo, Bombambili na Misufini na kata nyingine nne za Matarawe, Mjimwema, Ruvuma na Seedfarm.
  Gazeti hili lilishuhudia askari wakiwa wamemwagwa kwenye eneo la mkutano na wengine wakiwa wanazunguka kwenye magari yao huku wakiwa na silaha mbalimbali.
  Askari hao walianza kuzunguka kuanzia saa tano asubuhi wakati mkutano wa CHADEMA ulikuwa umepangwa kuanza saa kumi alasili  [​IMG]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Hivi haki hizi za kimsingi ndani ya katiba hii yenye viraka 14 mbona polisi wanazichezea hivyo.............hili linanikumbusha wakati wa mkoloni ambaye ndiye aliyeanzisha vibali kutolewa na polisi na serikali hii bila ya kujua madhara yake imekuwa ikiiga mbinu za mkoloni za kukandamiza raia wasio na hatia...................
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Polisi ishawaambia wasiandamane, wakikaidi wakiandamana, wakazuiwa kwa nguvu na polisi, ni nani wa kumlaumu.

  Hilo la Mkuu wa wilaya lina njia zake za kutatuwa na maandamano sio mojawapo. Kuna sababu nyingi za kumfanya Mkuu wa Wilaya azuie hizo vocha.

  Chadema wangekwenda kuonana nae ofisini kwake awaeleze sababu zake. Nadhani hiyo ndio njia muafaka na rahisi lakini si maandamano.

  Au maandamano ni agenda ya siri ya chadema?
   
 4. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tayari wamesema sababu alizozitoa mkuu wa wilaya ni hafifu,na pia kata zilizokosa ni kule chadema ilikoshinda sasa hapo natumaini mtu mzima na akili zake ataelewa wazi ni uamuzi wa makusudi.Hizo propaganda mara mkuu wa mkoa atashughulikia ni ubabaishaji kwa nini DC asiwajibike kwa hilo.Haya ndi matatizo tunayopata kutoka kwa wakuu wa wilaya na mikoa wa CCM
   
Loading...