Polisi: Sikukuu hii hatutapiga faini, tukikuamata ni ndani, watoa namba ya dharura

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,507
55,027
Heshima kwenu wakuu,

Jeshi la Polisi Kupitia kwa Lucas Mkondya, limeongea na wanahabari na kusema, Sasa hivi Trafiki wana vipimia kilevi. Tukikukamata umelewa barabarani tunakupeleka kituoni, sikukuu utailia ndani halafu hiyo faini unaenda kuilipa mahakamani jumatatu.

Kwanaza kasema tarehe 19 Polisi walikamata majambazi wawili wakiwa shotgun huko Kigogo Luhanga, Walikuwa kwenye Pikipiki mbili, waliwashambulia askari ili walizidiwa. Polisi walijeruhi wawili na wawili wakakimbia. Wakati tunawapeleka Hospital wakafariki. Tulikamata Postol pia maeneo ya mabibo .

Baada ya Mwezi mzima huu wa Mfungo wa Ramadhani tumejipanga. Nyumba zote za ibada kutakuwa na askari wa kawaida na askari kanzu na sehemu zote zenye mikusanyiko. Tutatumia vikosi vyetu vyote. FFU, helcopter, Farasi na Mbwa siku zote kuanzia idd mosi hadi Idd pili. Hivyo watu wakafanye Starehe zao bila hofu.

Tunawashauri walevi wasinywe kupita kiasi kwani inaweza ikakufanya usimuone hata mbaya wako, Wale wanaoshindwa kujizuia, watafute mtu wa kuambatana naye. Wale wa Kwenye fukwe wahakikishe hawaendi Kina kirefu.

Haturuhusu DISCO TOTO mwaka huu. Mmiliki Tukikuona unafanya disco toto tunakukamata. Kumbi za starehe zisijae sana, Kama ikitokea maafa ukumbuni utakutana na mkono wa Sheria.

Kwa Madereva ambao ni warevi Msinywe Pombe, ukinywa pombe nenda na dereva ambaye sio mlevi. Hii ni kwa usalama wako. Tukikukamata Umelewa tunakupeleka Lockup. Wengine unakuta na furaha kupita kiasi hadi wanavunja sheria, nawashauri Mpunguze mzuka sababu tukikukamata tunakuweka Lockup na sikukuu utaila ukiwa lockup kesho yake tunakupeleka kulipa faini mahakamani.

Nawaomba wananchi mtupe taarifa za watu wahalifu ili msherehekee sikukuu vizuri. Kama kuna mtu unamshitakia tuambie sisi.

Ukiona kuna mambo ambayo unaona yanaenda sivyo, tupigie simu.

Mwananchi tupe taarifa kupitia.

RPC Ilala:
0715009980
0754339558

Kamanda mkoa wa Temeke Grace Mloto
0715009979
0754397454/9

Kamanda wa Polisi Kinondoni Suzani Kaganda

0715009976
0684111111

Hizi namba zipo on Masaa yote 24/7

Tuna namba ya chumba cha Mawasiliano, ukiipiga tu hata haiiti(Ukipiga mara moja tu anapoke) inapokelewa hapo hapo. Hii namba ndo ya magari yetu ya doria. Ukipiga tu tunapokea hapo hapo.
0787668306.

Tunaomba tupeane taarifa kuweka Jiji letu salama.

---------

TAARIFA RASMI YA MSEMAJI WA JESHI LA POLISI

Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El Fitri, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao. Kipindi kama hiki cha sikukuu baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu na vitendo vingine ambavyo huhatarisha usalama wa watu na mali zao.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi nchini, limejipanga kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhakikisha kwamba wananchi wanasherehekea Sikukuu katika hali ya amani na utulivu.

Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.

Vilevile, Jeshi la Polisi linawatahadharisha watumiaji wa vyombo vya moto barabarani kuwa makini na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kwa wale wote watakaovunja sheria na kanuni za usalama barabarani kwa mabereva kutumia vilevi, bodaboda kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi pamoja na kupiga honi hovyo.

Pia, tunawataka wananchi wote kuwa wepesi katika kutoa taarifa kwa kupitia namba za simu za bure 111 au 112 pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara.

Tunawatakia watanzania wote Sikukuu njema ya Eid El Fitri.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba -ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
 
_20170623_134857.JPG

Ndugu zetu wa Mikoani mnaalikwa kufika Dar kula Eid ila upuuzi wenu uachieni KILUVYA,
Mkifanya ujinga hamtarudi MIKOANI,kama unatokea kusini mwa Tanzania ujinga malizia VIKINDU,kama unapitia njia ya Bagamoyo malizia MAPINGA,na kama unatokea Kisarawe basi ujinga malizia MSITU WA KAZIMZUMBWI.
 
Dar sio mji mzuri kupumzika, sioni kwanini mtu atoke maeneo mengine
eti akasherehekee Dar.
 
“Tuutatumia Vikosi vyetu vyote. Tutatumia Vikosi vya FFU, vitakuwepo mitaani kwa ajili ya kuimarisha doria. Tutatumia Helkopta, tutatumia Farasi, tutatumia Mbwa na Askari wengi sana watakuwepo. Kwa hiyo napenda kuwahakikishia Wananchi kwamba wasiwe na wasiwasi Jeshi lao la Polisi limejipanga katika kuwalinda na kuhakikisha kwamba Sikukuu Eid Mosi, Eid Pili zinapita salama bila kubughudhiwa.” – Lucas Mkondya, Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam
 
Wasije wakafanya na wananchi wakalipuliwa, maana hao wa Kibiti wana hasira na Polisi.
 
Back
Top Bottom