Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Jamaa huyo akiwa amevaa miwani mieusi, aliyetambuliwa kama Denis Ngengi Muigai mara ya kwanza alionekana kwenye televisheni kuwa ni mmoja wa walioshuhudia mkasa wa ajali ya ndege aina ya helkopta ilioanguka katika ziwa Nakuru 21 Oktoba.
Aligonga vichwa vya habari kwa mara nyingine Novemba 6 alipodai kuwa mmoja wa watu wa kwanza walioshuhudia ajali ambapo Gavana wa Nyeri Wahome Gakuru alifariki.
Afisa mkuu wa upelelezi na jinai eneo la Msambweni, Kaunti ya Kwale aliomba makao makuu ya idara hiyo imwasilishe Muigai kwake ili ampeleke kortini kujibu mashtaka ya uharifu.
Mnamo Alhamisi Mkurugenzi wa idara hiyo (DCI) Ndegwa Muhoro alitangaza kukamatwa kwa Bw. Muigai eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu.
Kulingana na ripoti za polisi zilizoonwa na wanahabari, Muigai alishawahi kukamatwa mnamo 2014 katika eneo la Diani na kushtakiwa katika mahakama ya Kwale kwa kosa la kujifanya afisa wa Jeshi la Wanahewa.
DCIO wa Msambweni ameomba makao makuu ya DCI kumwasilisha Kwale ili ashtakiwe kwa kufeli kufika kortini baada ya kuachiliwa kwa dhamana, ambapo agizo la kumkamata lilitolewa na mahakama ya Kwale.
Kwenye mahojiano katika runinga ya NTV baada ya ajali ya ndege ya helkopta katika ziwa Nakuru, Bw. Muigai alidai kuwa yeye ni rubani wa serikali.
Kwenye mahojiano mengine na runinga ya Citizen, alisema kuwa alikuwa akifuata gari aina ya Mercedes Benz la marehemu Wahome Gakuru kabla ya kupata ajali.
======
Uchunguzi wa alama za vidole uliendeshwa na kitengo maalumu cha upelelezi na jinai umemuanika jamaa huyu kama mshukiwa sugu wa uharifu, jamaa aliyetokeza kama shahidi mwenye utu amegeuka mshukiwa uharifu kupitukia.
Kando na kusema uongo kuhusu kazi anayefanya, amebainika kutumia majini tofauti yapatayo 8 yamkini kuwapumbaza wakenya wasiomtambua.
Kulingana na taarifa iliyotumwa kwa mpelelezi mkuu Ndegwa Muhoro na shajili wa upelelezi maalumu, mshukiwa huyu ametumia majina hayo katika kesi tofauti maeneo kadhaa nchini Kenya.