Polisi: Shahidi mkuu wa ajali mbili ni mharifu, alishawahi kukamatwa kwa kujifanya afisa wa jeshi la wanahewa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
55fc1fcadc4024c69de894c99ab9c4e7.jpg
Mwanamume aliyedai kuwa shahidi katika ajali mbili kwa kipindi kifupi ni mharifu ambaye amekuwa akisakwa na polisi.

Jamaa huyo akiwa amevaa miwani mieusi, aliyetambuliwa kama Denis Ngengi Muigai mara ya kwanza alionekana kwenye televisheni kuwa ni mmoja wa walioshuhudia mkasa wa ajali ya ndege aina ya helkopta ilioanguka katika ziwa Nakuru 21 Oktoba.

Aligonga vichwa vya habari kwa mara nyingine Novemba 6 alipodai kuwa mmoja wa watu wa kwanza walioshuhudia ajali ambapo Gavana wa Nyeri Wahome Gakuru alifariki.

Afisa mkuu wa upelelezi na jinai eneo la Msambweni, Kaunti ya Kwale aliomba makao makuu ya idara hiyo imwasilishe Muigai kwake ili ampeleke kortini kujibu mashtaka ya uharifu.

Mnamo Alhamisi Mkurugenzi wa idara hiyo (DCI) Ndegwa Muhoro alitangaza kukamatwa kwa Bw. Muigai eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu.

Kulingana na ripoti za polisi zilizoonwa na wanahabari, Muigai alishawahi kukamatwa mnamo 2014 katika eneo la Diani na kushtakiwa katika mahakama ya Kwale kwa kosa la kujifanya afisa wa Jeshi la Wanahewa.

DCIO wa Msambweni ameomba makao makuu ya DCI kumwasilisha Kwale ili ashtakiwe kwa kufeli kufika kortini baada ya kuachiliwa kwa dhamana, ambapo agizo la kumkamata lilitolewa na mahakama ya Kwale.

Kwenye mahojiano katika runinga ya NTV baada ya ajali ya ndege ya helkopta katika ziwa Nakuru, Bw. Muigai alidai kuwa yeye ni rubani wa serikali.

Kwenye mahojiano mengine na runinga ya Citizen, alisema kuwa alikuwa akifuata gari aina ya Mercedes Benz la marehemu Wahome Gakuru kabla ya kupata ajali.

======
Uchunguzi wa alama za vidole uliendeshwa na kitengo maalumu cha upelelezi na jinai umemuanika jamaa huyu kama mshukiwa sugu wa uharifu, jamaa aliyetokeza kama shahidi mwenye utu amegeuka mshukiwa uharifu kupitukia.

Kando na kusema uongo kuhusu kazi anayefanya, amebainika kutumia majini tofauti yapatayo 8 yamkini kuwapumbaza wakenya wasiomtambua.

Kulingana na taarifa iliyotumwa kwa mpelelezi mkuu Ndegwa Muhoro na shajili wa upelelezi maalumu, mshukiwa huyu ametumia majina hayo katika kesi tofauti maeneo kadhaa nchini Kenya.
 
Kuna waliosema kuwa Kenya napo kumbe polisi wana mambo ya ajabu kwa ajili ya kushikwa huyu jamaa.

Huyu ni hatari mno. Ajali mbili katika kipindi cha majuma mawili inawezekanaje kama si kiherehere
 
Sasa imebaki ni maamuzi ya busara kwenye hili jambo
Mkuu.. Huyu jamaa mengi yanazidi kuibuka kando kusema uongo kuhusu kazi anayefanya, imebainika kuwa ana kesi 8 za uharifu katika maeneo tofauti akitumia majina tofauti kupumbaza watu.
 
Atakuwa mjinga tu, angekuwa mharibu mbobezi asingekuwa mjinga kias cha kutaka atokee kwenye TV.
Angejua kuwa ni hatari kwake kukubari kuhojiwa tena kwa mbwembwe kwenye tv
 
Haiwezekani nyumba iwake moto mikocheni,mbweni,upanga kote wewe umekuwa shuhuda wa kwanza, lazima tukukamate tu!
Wale waliokuwa wakisema mbona kawaida wako wapi? Mtu anapumbaza watu kiasi hiki halafu anatetewa?
 
Wale waliokuwa wakisema mbona kawaida wako wapi? Mtu anapumbaza watu kiasi hiki halafu anatetewa?
Ajali za kutengenezwa huwa zinakuwa na watu kama hawa, utasikia mara dereva alionekana kama amelewa akaanza kuyumba na mwisho ajali ikatokea..

Au atasema dereva alikuwa katika mwendo mkali.. Hivi ni vitu vya kuangalia sana..

Hadi hapo hao wakenya wako vizuri!
 
kiherehere ya kipumbavu! akamatwe mkora huyo...haiwezekani kabisa mtu mmoja amekuwa witness kwa kesi mbili tofauti ndani ya mwezi moja...jamaa amekuwa akijiskuma kuhojiwa na wanahabari sijui anatafta umaarufu..
 
What a coincidence....2 fatal accidents same witness...Guy captured on camera...More than meets the eye...
 
duniani hamna jema. mtu wa watu kajitolea kutoa ushahidi bado manyanyaso yanazidi.
 
duniani hamna jema. mtu wa watu kajitolea kutoa ushahidi bado manyanyaso yanazidi.
Umeona eeh? Asante ya punda bana mtu anawasaidia maafisa wa polisi na ushuhuda wa bure katika ajali mbili tofauti afu wanampiga teke la uso. :D:D:D
 
Back
Top Bottom