Polisi Ruvuma atuhumiwa kujeruhi Raia kwa wivu wa kimapenzi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Jeshi la Polisi la mkoani Ruvuma linamshikilia askari wake aitwaye Pc Keneth Mkwela kwa kosa la kumjeruhi Andrew Milanzi mwenye umri wa miaka 33 kwa kutumia kitu chenye ncha kali kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, – Pili Mande amesema tukio limetokea katika Kijiji cha Magagula wilaya ya Songea kwenye nyumba ya wageni baada ya askari huyo kubaini Milanzi alikuwa akifanya mawasiliano na mwenza wake.

Amesema inadaiwa kuwa askari huyo alimchoma raia huyo na kitu chenye ncha kali katika eneo la chini ya ubavu wa kushoto na kumsababishia mjeruhiwa huyo maumivu makali ambayo yamesababisha kulazwa katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Polisi mkoani Ruvuma wanaendelea kumshilikilia askari huyo wakati akisubiri taratibu za kisheria pamoja na taratibu za kiaskari katika kipengele cha nidhamu ya askari.
 
wacha tumtie jela,ili awe na akili wakati mwingine.

askari wote wana demu zaidi ya mmoja,kenyewe kamekomaa na mmoja nayeye wanakapigia.
 
Baba mdogo kazingua ..apelekwe tu kunako jela maana amefanya Jambo la kipuuzi
 
Tena usikute huyo nwanamke wanae mgombania ni mwanachuo wa chuo cha maendeleo mlale,
Maan ma askari na wajeda ndo vichenchede vyao hivyo.
Ila huyu askari apelekwe jela, iwe fundisho kwa wengine.
 
Huyo askali angemuona LwandaMagere angemsaidia kumpa dawa ya shipa la kimkakati hakika huyo bint asingechepuka.
huyu jamaa sijui km atarudi mapema JF kujibu naona Telegram zile bukubuku zinamzingua maana lazima akuunge na Hadithi yake la sivyo watamdai waliolipa
Wangoni bwana ni kiboko kwa hapo chini, bora umpe pesa atafikisha lakini papuchi hafikishi
nini asili ya kupenda tunda hilo?
 
Back
Top Bottom