Polisi Njombe, Iringa wadharau agizo la Waziri Lugola la 'kutokurusha jini'

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,496
41,004
Siku za karibuni Waziri Lugola aliliagiza jeshi la Polisi kuacha tabia yao ya kuyapiga picha magari halafu kuzirusha picha hizo mbele (kwa maneno yake alisema hao polisi wanaofanya hivyo wanaita "kurusha jini") ili waliopigwa picha hizo walipishwe adhabu kwa makosa ambayo pale wanapokamatwa hayawezi kuthibitika kwa vile picha hizo zimepigwa eneo ambalo hawalijui.

Waziri aliagiza picha za kuzidisha mwendo au makosa mengine, zipigwe eneo la tukio, na dereva aoneshwe picha yake kwenye speed camera, na siyo kwenye simu ya askari.

Mikoa karibu yote walitii agizo hilo na kulitekeleza isipokuwa mkoa wa Iringa na Njombe (labda ipo na mingine).

Wiki iliyopita nilithibitisha umuhimu wa agizo la waziri Lugola walilolikataa askari wa Njombe na Iringa. Nilifika eneo la karibu na Makambako nikitokea Njombe, na kusimamishwa kuwa nilikuwa nimezidisha speed eneo fulani ambalo sikulijua lakini nilikuwa na uhakika kuwa siyo kweli. Baada ya hapo vikaanza vitisho kwamba kama sikubali kosa, gari na mimi tupelekwe kituoni kwaajili ya kufungua charge ya kupelekwa mahakamani.

Nilipozidi kuichunguza ile picha, haikuwa ya gari yangu, na picha yenyewe ilikuwa haioneshi hata namba ya gari. Nikawakatalia kuwa ile gari siyo ya kwangu. Hapo walianza kofoka sana (mnawajua polisi wetu wengi wao walivyo). Kuondoka kwangu ilikuwa baada ya kupatikana mmojawapo mwenye busara, alichunguza, naye kukubaliana na mimi kuwa ile gari haikuwa gari yangu japo zote ni aina moja. Iliyopigwa haikuwa na carrier wakati ya kwangu ilikuwa na carrier. Ya kwangu haikuwa na maandishi ubavuni wakati iliyopigwa ilikuwa na maandishi.

Wakati yakiendelea ya kwangu, madereva wengine nao walikuwa wakipambana na yao, lakini yote ilikuwa ni uhakika wa hizo picha ambazo zilikiwa hazina hata namba za magari.

Kila aliyelalamika na kusema utaratibu huo umepigwa marufuku na Waziri Lugola, alijibiwa, "sisi hatufanyii kazi maneno ya majukwaani ya wanasiasa, tunafuata maelekeo ya Jeshi la Polisi". Kitu cha kujiuliza, kama maagizo ya waziri hayana maana kwa Jeshi la Polisi, Waziri yupo kwaajili ya nini?
 
"sisi hatufanyii kazi maneno ya majukwaani ya wanasiasa, tunafuata maelekeo ya Jeshi la Polisi". Kitu cha kujiuliza, kama maagizo ya waziri hayana maana kwa Jeshi la Polisi, Waziri yupo kwaajili ya nini?

Hapa umeandika swali zuri sana Mkuu. Kinachotakiwa Waziri Lugola ajitokeze na kutuambia kwanini anatumia kodi zetu kufanyia maigizo? IGP naye ajitokeze aseme yake.
 
thibitisha maneno yako..wataje hao askari unaosema walikunyanyasa na kukujibu hayo majibu unayoyasema?
 
Siku za karibuni Waziri Lugola aliliagiza jeshi la Polisi kuacha tabia yao ya kuyapiga picha magari halafu kuzirusha picha hizo mbele (kwa maneno yake alisema hao polisi wanaofanya hivyo wanaita "kurusha jini") ili waliopigwa picha hizo walipishwe adhabu kwa makosa ambayo pale wanapokamatwa hayawezi kuthibitika kwa vile picha hizo zimepigwa eneo ambalo hawalijui.

Waziri aliagiza picha za kuzidisha mwendo au makosa mengine, zipigwe eneo la tukio, na dereva aoneshwe picha yake kwenye speed camera, na siyo kwenye simu ya askari.

Mikoa karibu yote walitii agizo hilo na kulitekeleza isipokuwa mkoa wa Iringa na Njombe (labda ipo na mingine).

Wiki iliyopita nilithibitisha umuhimu wa agizo la waziri Lugola walilolikataa askari wa Njombe na Iringa. Nilifika eneo la karibu na Makambako nikitokea Njombe, na kusimamishwa kuwa nilikuwa nimezidisha speed eneo fulani ambalo sikulijua lakini nilikuwa na uhakika kuwa siyo kweli. Baada ya hapo vikaanza vitisho kwamba kama sikubali kosa, gari na mimi tupelekwe kituoni kwaajili ya kufungua charge ya kupelekwa mahakamani.

Nilipozidi kuichunguza ile picha, haikuwa ya gari yangu, na picha yenyewe ilikuwa haioneshi hata namba ya gari. Nikawakatalia kuwa ile gari siyo ya kwangu. Hapo walianza kofoka sana (mnawajua polisi wetu wengi wao walivyo). Kuondoka kwangu ilikuwa baada ya kupatikana mmojawapo mwenye busara, alichunguza, naye kukubaliana na mimi kuwa ile gari haikuwa gari yangu japo zote ni aina moja. Iliyopigwa haikuwa na carrier wakati ya kwangu ilikuwa na carrier. Ya kwangu haikuwa na maandishi ubavuni wakati iliyopigwa ilikuwa na maandishi.

Wakati yakiendelea ya kwangu, madereva wengine nao walikuwa wakipambana na yao, lakini yote ilikuwa ni uhakika wa hizo picha ambazo zilikiwa hazina hata namba za magari.

Kila aliyelalamika na kusema utaratibu huo umepigwa marufuku na Waziri Lugola, alijibiwa, "sisi hatufanyii kazi maneno ya majukwaani ya wanasiasa, tunafuata maelekeo ya Jeshi la Polisi". Kitu cha kujiuliza, kama maagizo ya waziri hayana maana kwa Jeshi la Polisi, Waziri yupo kwaajili ya nini?
Matamko siyo sheria, ukitaka yawe sheria yatungiwe kanuni au sheria mama ifanyiwe marekebisho mwafaka.
 
Back
Top Bottom