Polisi ni wa ajabu hadi wanasahau kutumia akili; unamkamata Mbowe kuwa anapanga kuua viongozi, halafu ndio unaenda nyumbani kwake kutafuta ushahidi?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Wazungu wana msemo kwamba "some people are so vain that they forget to be clever"

Ndivyo navyowaona Polisi wetu wa Tanzania. Yaani mtu mwenye tuhuma nzito za kutaka kuua viongozi, hadi unamkamata lazima uwe na ushahidi dhidi yake mzito. Sasa iweje unamkamata kwa tuhuma nzito kiasi hicho, halafu ndio unaenda nae nyumbani kwake kutafuta ushahidi na kuchukua tablets za watoto?

Halafu bila aibu unawatangazia watu kwamba Mbowe alijua karibu atakamatwa Dar kwa tuhuma za ugaidi kutaka kuua viongozi ndio maana akakimbilia Mwanza. Kwa hiyo, kwa akili ya Polisi, Mbowe amekimbilia Mwanza na kuacha ushahidi nyumbani unaoonyesha anakula njama za kuua viongozi! Mtu ambaye mnamfuatilia kwa makosa ya kutaka kuua viongozi mnampa nafasi hadi ya kusafiri Mwanza ina maana hamkuwa mnam-shadow 24hrs a day? Hadithi za kuuza kwa watu wenye akili hizo? Why are you insulting the intelligence of Tanzanians?

Hivi mtu anaepanga kuua viongozi anakuwa mjinga kiasi hicho cha kuacha ushahidi kwenye laptop nyumbani? Hapa kuna mawili, aidha Mbowe ni so vain, au Polisi ndio extremely vain.

Sasa kama Polisi mnataka kum-harass Mbowe, angalau tafuteni kitu chenye mshiko, sio uchwara kama huu wa kusema alitaka kuua viongozi ili tu mumtie ndani na kumnyima dhamanaa kwa lengo la kuua kampeni yake ya Katiba mpya. Mnakuwa so vain that you completely forget to be clever. Shame on you.
 
Nchi zetu bhana kila kukicha wanafikiri kuweka wapinzani ndani wakikaa huko peke yao utadhani lipo la maana wanajadili kumbe Mpesa ijenge bara bara mara property tax iwekwe kwenye Luku...hovyo kabisa..
Unajua kuna vitu hata kama haupo kwenye siasa vinafanya uwe kama mwanasiasa. Yaani inafikia hawa Polisi wanatia kichefuchefu hata kuwaona tu mtaani
 
Nadhani imefikia point viongozi wa Tanzania na Polisi wanatuona Watanzania ni wajinga, hatuna akili, tuko gullible, mazezeta, watu wa kuburuzwa, na hata wakitutia vidole sehemu yeyote ya mwili tuatabaki tunakenua macho tu kwa kuwaogopa.

Tutalipishwa kodi hatutafanya kitu, tutabanwa katika haki za binadamu hatutafanya kitu, kodi zetu zitaliwa hatutafanya kitu, viongozi watajineemesha na wao kutubambikia kodi wakati wao wanajilipa mamilioni hatutafanya kitu, tutadanganywa kama watoto wadogo hatutafanya kitu.

Hivi kweli Watanzania tuko hivyo?

Wale Watanzania Nyerere aliokuwa akisema ukiwasukuma sukuma kila siku kuna siku watainuka na kukuumiza , ndio sisi au ni Tanzania nyingine?
 
Nchi zetu bhana kila kukicha wanafikiri kuweka wapinzani ndani wakikaa huko peke yao utadhani lipo la maana wanajadili kumbe Mpesa ijenge bara bara mara property tax iwekwe kwenye Luku...hovyo kabisa..
Akili za watawala wa CCM ni kupambana na wapinzani basi
 
Nadhani imefikia point viongozi wa Tanzania na Polisi wanatuona Watanzania ni wajinga, hatuna akili, tuko gullible, mazezeta, watu wa kuburuzwa, na hata wakitutia vidole sehemu yeyote ya mwili tuatabaki tunakenua macho tu kwa kuwaogopa. Tutalipishwa kodi hatutafanya kitu, tutabanwa katika haki za binadamu hatutafanya kitu, kodi zetu zitaliwa hatutafanya kitu, viongozi watajineemesha na wao kutubambikia kodi wakati wao wanajilipa mamilioni hatutafanya kitu, tutadanganywa kama watoto wadogo hatutafanya kitu.

Hivi kweli Watanzania tuko hivyo?

Wale Watanzania Nyerere aliokuwa akisema ukiwasukuma sukuma kila siku kuna siku watainuka na kukuumiza , ndio sisi au ni Tanzania nyingine?
Jinsi tulivyoundwa from independence, Muungano hadi leo ndivyo tulivyo au unabisha?!
 
Nadhani imefikia point viongozi wa Tanzania na Polisi wanatuona Watanzania ni wajinga, hatuna akili, tuko gullible, mazezeta, watu wa kuburuzwa, na hata wakitutia vidole sehemu yeyote ya mwili tuatabaki tunakenua macho tu kwa kuwaogopa.

Tutalipishwa kodi hatutafanya kitu, tutabanwa katika haki za binadamu hatutafanya kitu, kodi zetu zitaliwa hatutafanya kitu, viongozi watajineemesha na wao kutubambikia kodi wakati wao wanajilipa mamilioni hatutafanya kitu, tutadanganywa kama watoto wadogo hatutafanya kitu.

Hivi kweli Watanzania tuko hivyo?

Wale Watanzania Nyerere aliokuwa akisema ukiwasukuma sukuma kila siku kuna siku watainuka na kukuumiza , ndio sisi au ni Tanzania nyingine?
Umeongea point kubwa mno
 
Umeongea point kubwa mno
Wanaudhi sana Mkuu.

Halafu wataumbuka tu. Kwa tuhuma kama hizi, itabidi wataje waliokuwa wamefanyiwa njama za kuuwawa ni kina nani. Huwezi kumtuhumu mtu kupanga njama za kuua bila kusema walitaka kumuua nani. Naweza nikasema kesho namuua Raisi, lakini ushindwe kunitia hatiani kwa sababu lazima unishitaki ukiwa na jina la mtu ninaepanga kumuua - victim ni nani.

Lakini nahisi hawa Polisi watasema walipanga kuua viongozi - Wenyeviti wa mitaa wa CCM sijui
 
Nchi zetu bhana kila kukicha wanafikiri kuweka wapinzani ndani wakikaa huko peke yao utadhani lipo la maana wanajadili kumbe Mpesa ijenge bara bara mara property tax iwekwe kwenye Luku...hovyo kabisa..
Nahisi Makonda amerudi kwenye kushika utamu, yaani hatamu
 
Fatma ngugambile I love yuuu!

1627026519444.png
 
Back
Top Bottom