Polisi na wengine: Huu si Wakati wa Kuibeba CCM!

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,611
1,250
Kwa vyombo vyote vya polisi inaonekana kuna baadhi ya wakuu wa polisi wanaelewa kazi yao na hawapo tayari kuhusishwa kazi yao na masuala ya kisiasa kwa maana ingine wanafanya wajibu wao bila ya kujali huyu anatoka chama gani ,wao wanafuata taratibu za kazi zao.

Na kuna polisi wengine wao hawajui kuwa CCM ni Chama Cha Siasa kama ilivyo vyama vingine ,na polisi hawa ni wakubwa kwa wadogo hawajui kabisa kama ipo siku CCM inaweza kupoteza madaraka ,polisi hawa ni sawa na wale wananchi ambao hawajui kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikwisha kufa kitambo ,wao wanajua bado Mwalimu yupo hai ,hivi ndivyo walivyo baadhi ya polisi wetu ,wao wanaona bado tupo katika mfumo wa Chama kimoja ,angalia mambo ya mikutano ni rahisi sna kuona utashi wa polisi kupendelea au tuseme kuwaogopa CCM ,yanapokuja kuja mambo ya maandamano ,polisi wanazuia ya vyama vingine na kuyaruhusu ya CCM.

Polisi wasipoangalia watakuja kutoswa na hapo ndipo CCM watakapowaruka ,hawatawaona wale waliokuwa wakiwapa maelekezo ,maelekezo kutoka ndani ya Chama Cha CCM ,yaani polisi anaelekezwa na balozi au mwenyekiti wa mtaa kuwadhibiti watu wa upande mwengine.

Polisi wanawaogopa CCM na wamekuwa wakiendeshwa kwata na kupewa maelezo kuyatekeleza kinyume na kazi yao ,polisi wanashindwa kusoma yanayowakuta wengine ambao walikuwa ni viongozi ama wa polisi au jeshi ,baada ya utawala kupita yanawakuta mashtaka ,mashtaka ambayo hayana tofauti na amri wanazozitekeleza polisi amri zitolewazo kwa maelekezo ya CCM ,dalili zote zinaonyesha kuwa CCM inaporomoka ni suala la muda tu ,polisi mkiendelea kuwakumbatia CCM basi uchafu waliokuwa nao utawakumba na kuwatapakaa na nyinyi ,CCM ni wa kuepukwa.
 

Haji Salum

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
1,022
0
Magamba yanastahili adhabu hii!

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom