Polisi na wabunge wa Upinzani vita inaendelea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi na wabunge wa Upinzani vita inaendelea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Najijua, May 31, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wadau maswali yanazidi kuniumiza kwanini polisi wana kasi kubwa sana za kukamata wabunge wa upinzani na kuwadhalilisha kana kwamba sio viongozi wa kitaifa?kwanini hawapewi heshima zao

  hebu angalau matukio ya mwaka 2001 ya CUF, Arusha, Nyamongo na Urambo hivi karibuni
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  umeona hilo kwa vile wa CUF amekamatwa? Ungeona hivyo kabla....
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Polisi wanafanya kazi zao kwa kusukumwa na nguvu ya chama cha magamba, na wanafanya hivyo kwa lengo moja tu la kuwadhalilisha.

  Mgombea ubunge wa magamba alimkata mitama ocd wa maswa mwaka jana lakini hakuna kilichofanyika, zaidi sana ni rpc kuongeza aibu kwenye tukio hilo kwa kusema hayo ni mambo binafsi kati ya mgombea na ocd.

  Wananchi kwa umoja wetu tunapaswa kusimama na kuwakemea polisi kwa tabia yao ya kuwadhalilisha viongozi pamoja wabunge wa vyama vya upinzani, ili kuhakikisha kwamba tabia hii inakomeshwa kabisa.
   
 4. H

  Haika JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  hivi umenikumbusha swali langu,
  je utaratibu wa kuvua magamba ukoje? ni nini kinajumuishwa katika 'kuvua magamba'?
  je ni kutolewa kamati kuu? - wangapi wametoka
  ni kuvuliwa uanachama wa ccm? wangapi tayari?
  ni kushitakiwa mahakamani? wangapi tayari?

  yani kwa kifupi, je tumeshaanza kuona huyo kiumbe mpya aliejivua magamba? au bado anatafuta mahali pa kujificha ndio avue?
   
 5. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Polisi wanapaswa kutambua vita ikigeuka ikaelekezwa kwao itakuwa ni balaa kuliko wanavyo fikiria. wasidhani wananchi wanatishwa na hayo magobore yao. Siku watakapo amua kujihami itakuwa ni balaa la ajabu. Naona dalili mbaya sana ya damu kuelea kila pande ya nchi huku mwenye kaya kakaa kimya. But why JK?? why is this happening & you remain silent JK, why? Inahuzunisha sana kuoina nchi yangu inaelekea kwenye dimbwi la damu.
   
 6. k

  kiloni JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yeah
  JK yuko kimya kwa sababu amewatuma.
  Lakini kinachoshangaza ni wananchi kupingana kisiasa hovyo! No hii si siasa tena ni vita kati wananchi wenye raslimali zao na mawakala wa wazungu wawekezaji yaani wakoloni weusi.
  Ni vita ya ukombozi ngumu kuliko ile ya Afrika kusini kwa sababu ni wenzetu tuliowapa ridhaa ya kutusimamia raslimali zetu wanaziiba na kuuza ovyo. Ni ngumu kwa sababu vyombo vya usalama vya umma vimegeuka kuwa vyombo vya kulinda mafisadi. Ni ngumu kwa sababu adui anatumia silaha zote zikiwemo ujinga wetu. Ni ngumu kwa sababu kuna wenzetu bado hawataki kuelewa kuwa tuko maskini kwa sababu tunaibiwa kila kukicha. Ni ngumu kwa sababu silaha za kutugawa zinatumika kama vile ukabila na UDINI.
  Ni hatari.
  Bahati nzuri ni kuwa polisi wamesahaulika katika mgao wa mafisadi hivyo ni "choka mbaya" kama sisi. Wanahitaji kueleweshwa na Tunisia itahamia bongo kabla ya 2015.
  Ee Mungu shuka utuhurumie na kutukomboa tunaangamia!!!!!!!
   
 7. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kwa mwenendo huu wa polisi na raia ni mbaya sana kwa serikali iliyopo madarakani. Polisi wakumbuke ya kuwa tanzania ni nchi ambayo ina wazawa na wazalendo wa taifa lao ambao wanapambana na mambo ambayo yamesababishwa na watu wachache. Badala ya polisi kulinda amani wao wamekuwa ndio wavurugaji na kuingilia mambo ambayo hayawahusu. Raia wanawasaidia sana polisi katika ulinzi lakini polisi imekuwa ikiwajeuka na kuwasaliti watanzania. Polisi inatakiwa iwaache raia na serikali wavimbishane ili kazi ifanyike kwa ufanisi zaidi sio kuuziana makesi kwenye magunia. Picha iliyopo Tz sasa hivi imekuwa kama hakuna serikali kuna raia na polisi ndio wanapambana. Kama kazi za serikali zinafanywa na polisi basi watuambie tujue hatuna serikali ili uitishwe uchaguzi raia wachague viongozi wanaowaamini kuliko polisi kundelea kupambana na raia wakati raia wanalilia, wanatafuta haki yao.

  Polisi itambue ikitoa ushirikiano mzuri kwa jamii watafanya kazi yao kwa ufanisi zaidi na wanaweza kusaidia kuelimisha umma kuliko kufanya kazi kwa visasi na kuwagandamiza wapinzani wakati wamekula kiapo cha kulinda raia wote. Wapinzani wa tanzania ni watu wazuri sana kwa sababu wanatii sheria za nchi na kwa bahati nzuri kabala ya kufanya kitu chochote wanapitia polisi kwanza kutoa taarifa hapo ndio polisi inatakiwa kutoa elimu yao sio kukataaa kama nchi ni yao . Hizo posho wanazotetea na mlungula wanaopewa na CCM au mafisadi kunasiku zitawatokea puani.
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwa kifupi polisi hawajaandaliwa kupokea mfumo wa vyama vingi. Kwa kweli ni mfumo mzima wa utawala nazile nguzo kuu tatu bado zinawaywaya. Hii ni hatari kwa usalama wa Taifa na hata CCM yenyewe ambayo inaondika madarakani 2015, hao hao polisi watawashughulikia. Kamuulizeni kaunda.:mod:
   
 9. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Jana nilisikitika polisi wanavyo wapiga watu!!! hii ikiendelea itakula kwa polisi. labda wahakikishe kwamba nimekufa. Lkn nikiugua nikapona vile walivyo fanya haki ya mungu nitalipiza. Polisi endeleeni kutudharirisha watanzania lakini mpira ukichenji, mtaula wa chuya.

  NAAPA POLISI WAKINIUMIZA, NITALIPIZA KISASI.MAKE INAVYO ELEKEA MAMBO KARIBU TUTAINGIA MITAANI KUPIGANA NA POLISI. MSIDHANI NCHI NI YENU PEKE YAKE. NYIE ENDELEA KUTUJAZA HASIRA. SIKU FILIMBI IKIPIGWA, TUTAONA MWENYE BAHATI NDIYE ATAPONA.
   
 10. p

  plawala JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo polisi hawasomi alama za nayakati,naamini hata kwenye mitandao kama JF hawamo,maana wangepata mrejesho ili wabadili mienendo yao,lkn destination ni kulipiza kisasi,ingawa hatuombei tufikie hatua hiyo,kwa sab yatakuwa mauaji ya halaiki kama ya rwanda,ee mungu ntuepushie mbali!
   
Loading...