Polisi na udhanifu wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi na udhanifu wao

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngambo Ngali, Oct 27, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Ni Polisi, Mgambo, JKT, Magereza
  [​IMG] Tossi asema Polisi peke yao hawatoshi
  [​IMG] Mwema ataka matokeo yaheshimiwe  [​IMG]
  Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema


  p { margin-bottom: 0.08in; }
  Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa litashirikiana na askari Mgambo, Magereza na wale wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), katika kulinda vituo vya kupigia kura siku ya Uchaguzi Mkuu.
  Vile vile, Jeshi hilo limewataka wananchi kuheshimu matokeo yatakayotangazwa na kuachana na hisia kuwa yamechakachuliwa hali inayoweza kusababisha vurugu.
  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Venance Tossi, alisema vituo vya kupigia kura viko zaidi ya 51,000 hivyo polisi pekee hawawezi kumudu kuvisimamia.
  Katika mkutano huo pia alikuwepo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mohamed Abdulwakil na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Peter Kivuyo.
  Tossi alisema ndiyo sababu hata baadhi ya sehemu zilizokuwa zikilindwa na askari polisi Zanzibar, sasa zinalindwa na askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), kwa kuwa askari wamepangiwa kazi zingine.
  Alisema ingawa Zanzibar askari wa JWTZ watakuwepo katika baadhi ya maeneo lakini shughuli nzima ya ulinzi itafanywa na askari wa Jeshi la Polisi. Alisema Jeshi hilo lina ushirikiano mzuri sana na lile la JWTZ hivyo wamejipanga kwa pamoja katika suala la ulinzi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.
  Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, alisema siku ya uchaguzi suala muhimu kwa wananchi ni kupiga kura tu na si vinginevyo.
  Alisema wananchi wanapaswa kuheshimu matokeo yatakayotangazwa na waachane na uvumi, maneno ya uongo, hisia au visingizio vyenye lengo la kuwazuia wengine kwenda kupiga kura au kuvuruga zoezi la uchaguzi.
  Alisema vitendo vyovyote vya uvunjwaji wa Sheria kabla na baada ya uchaguzi ni uhalifu na kwamba Sheria haina udhuru kwani itachukua mkondo wake pindi ukiukwaji utakapofanyika.
  "Matokeo yanapotangazwa ni muhimu kutambua kuwa aliyeshinda ndiye aliyepigiwa kura nyingi pia ni vyema kutambua kwamba hayo ndiyo matokeo ya maamuzi ya walio wengi ambayo tunawajibika kuyaheshimu na kuyakubali," alisema.
  Mwema alisema kutii sheria na taratibu uchaguzi ni wajibu wa kila mpiga kura na kila mwananchi.
  "Nawaomba wananchi ushirikiano katika kukataa kushawishiwa ama kuhusishwa katika uvumi, fujo au vurugu zozote zinazoweza kuiingiza nchi katika machafuko yasiyo na maana yoyote na nawahakikishia kuwa amani na utulivu vitadumishwa wakati wote kabla na baada ya uchaguzi," alisema Mwema.
  Mwema aliongeza kuwa kura ni siri ya mpiga kura na hakuna mtu mwenye uwezo wa kutambua ni mgombea gani aliyempigia kura.
  Alisema kila mwananchi anapaswa kuondoka eneo la kituo cha kupiga kura baada ya kupiga kura ili kuepuka uwezekano wa kusababisha mikusanyiko inayoweza kutafsiriwa kwamba ni haramu.

  MAONI YANGU


  Polisi acheni hizo, mbona mnakuwa aprehensive sana, inaelekea mnajua kitu gani kinataka kufanyika. Hii press conference tell us a lot of things nashangaa kwa nini waandishi hawakuwauliza maswali baada ya hii press conference. Anyway najua Mwema unasoma hebu jibu haya maswali machache:

  1. Mgambo ni mtoto wa dhana ya CCM ya ulinzi, mpaka sasa mgambo wanatokana na CCM je kulifanyika vetting ya migambo wataokuwa deployed kwenye vituo kuondoa dhana kuwa wengi wa waliosimamia ulinzi ni CCM.

  2. JKT, kuna vijana wapya walioingia JKT je hao ni sehemu ya wasimamizi wa vituo vya kura? Kigezo kipi kilitumika kuwachukua vijana hao kuingia JKT?????

  3. Kwa nini polisi mnakimbilia kusema matokeo yaheshimiwe, ni nani, lini na wapi alisema hataheshimu matokeo, shimbo kasema wewe unarudia kuna nini hapa au mabosi wako wanataka kuiba kura?

  4. Suala la muhimu sio kupiga kura tuu, mimi naona suala la muhimu ni kupiga na kuilinda kura yangu niliyowaachia Mgambo wa CCM na Vijana wa JKT ambao sijui walikotoka.

  5. Kama jeshi la polisi litachukua mkondo wa sheria endapo kuna uvunjifu kabla na baada ya uchaguzi, mbona mgombea wa CCM aliyempiga OCD hajafikishwa mahakamani au lile sio kosa la jina???

  6. Kama mwanasheria nadhani unajua fika kuwa sio lazima kila anayeshinda uchaguzi ndiye aliyepigiwa kura nyingi. Kuna chaguzi nyingi tu zimebatitlishwa kwa sababu ya aliyetangazwa kutokuwa na kura nyingi kama unavyosema.

  7. Kwa jinsi press statement ilivyokaa ungemaliza na ushauri wa bure kuwa chama tawala na serikali yake kikubali matokeo ya uchaguzi na nyinyi polisi, magereza, JKT mgambo etc hamtambeba mgombea yoyote na wala hamtapokea na kutekeleza amri yoyote itakayokuwa kinyume cha katiba na sheria.
   
 2. K

  KIURE Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa wanajua kinachoendelea na kitakachofanyika siku (au usiku) hiyo/huo. Sheria inaruhusu watu wakae mita 100 toka kituo cha kura yeye anasema waende nyumbani! Watu wasikubali, wafuate sheria inavyosema. La sivyo maandamano nchi zima kupinga matokeo feki. Hawa wanataka watu waaundejeshi la kujikomboa toka kwa mafisadi wanaoongozwa na CCM. Ni raihisi tu, kikundi kidogo cha wapambanaji wanaanza kuwashughulikia vinara mmoja baada ya mwingine kwa kuanzia Kikwete, Lowassa, Rostam, Makamba, Ridhiwani, Salma, viongozi wa makampuni yaliyofadhili CCM, viongozi wa majeshi waliojitokeza hadharani kutisha raia, January, Salva, Jaji Makame, Kiravu, Majaji waliokataa hoja ya mgombea binafsi, wezi wa BOT/Kagoda/Meremeta, wawekezaji wanaonyanyanyasa raia, n.k. Hawa wakishughulikiwa wenzao watatia akili na nchi itarudi katika mstari. Tume huru ya uchaguzi itaundwa, Katiba mpya itatungwa, mahakama huru zitaanzishwa, n.k. Bila kuwashughulikia hawa watatawala milele kwa kuwa Mahakama, Majeshi, Bunge, Tume za uchaguzi, na sheria zinawapendelea.
   
 3. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sasa kama mshakata tamaa,, si mseme tu!
  mlipongia mlidhani mchezo wa kitoto?
   
Loading...