Polisi na PF3, ni unyama au ushenzi - Mwema tusaidieni

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,060
22,755
Mtu anafikishwa hospitalini akiwa hoi bin taabani, eti matibabu hapati mpaka PF3 kutoka polisi. Nimetembea sehemu nyingi duniani na jukumu la kwanza la vituo vya afya ni kusave life.

Hapa kwetu TZ ni ama kwanza pesa au PF3 ndio maisha ya mgonjwa yaokolewe. Je, huu ni ujinga, unyama au ushenzi kwani jukumu la msingi la serikali yoyote ni kuokoa/kulinda maisha ya wananchi wake. Hebu shuhudieni hapa;
Wataka CCM iwabane polisi watoe PF3 - Mussa Juma, Hanang

VIONGOZI wa CCM katika Mkoa wa Manyara, wameshauriwa kuchukua hatua za makusudi, kuwashinikiza polisi wilayani Hanang, kutoa hati za PF3 kwa vijana walijeruhiwa na askari wa Kikosi cha Kuliza Ghasia (FFU) katika vurugu za kugombea ardhi zilizotokea hivi karibuni wilayani humo.

Ombi hilo lilitolewa juzi na wananchi wa Vijiji vya Mogitu,Ming'enyi na Gidagamownd, walipokuwa wakizungumza katika kikao cha kutafutia suluhu ya mgogoro huo,kilichokuwa kimeitishwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Manyara,Lucas Ole Mukusi.


Kikao hicho pia kilimshirikisha Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Hanang, Goma Gwaltu.

Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mogitu,Israel Dawi, alisema hali za vijana watano waliopigwa na kujeruhiwa wakati wa kuwafukuza wafugaji wanaopinga kuchukuliwa kwa eneo lao la malisho, si za kuridhisha.

Dawi alisema licha ya kupata dhamana, vijana hao bado hawajapata matibabu na kwamba hiyo inatokana na polisi kuwanyima fomu za PF3..

Aliwajata vijana hao kuwa ni, Charles Maushi (27) Daniel Petro (30), Israel Yohana (16),Reuben Anthon na Demaya Doha, anayesemekana kuwa ana matatizo ya akili.


Akizungumza mara baada ya kupokea maombi hayo , Ole Mukusi aliomba kupatiwa majina na majeruhi hao na alipopewa, aliahidi kufikisha suala hilo katika ngazi zinazohusika.

"Naomba mtupe majina ya hao vijana na sisi tutayachukuwa na kuyapeleka ngazi zinazohusika....tumekuja hapa kupata suluhu ya mgogoro wenu na hili halitatushinda,"alisema Ole Mukusi.

Mapema Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Goma Gwaltu, aliwataka wafugaji hao, kueleza malalamiko yao yote kwao ili waweze kujadiliana kwa pamoja ili kurejesha amani katika wilaya hiyo.

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa kumekuwepo mgogoro wa juu ya ugawaji wa mashamba yaliyokuwa ya Shirika la Taifa la Chakula(NAFCO) ambayo yamerejeshwa kwa wananchi tangu mwaka 2006.
Pamoja na yote sijui CCM wanaingiaje hapa, duh !
 
Back
Top Bottom