Polisi na NEC waanza kuhofia barua za Amsterdam & Partners LLP?

Ni jambo jema pia kama NEC na Jeshi la Polisi likaweka adhabu kali kwa yeyote atakaye chana kipeperushi cha mgombea awe wa udiwani, ubunge au Uraisi. Pia bendera za vyama vyote ziheshimiwe si kwenye mikutano au ofisi na barabarani.
Ni wakati wa uchaguzi haki sawa.
Nawasilisha.
 
Kuwa nchi huru hakukupi haki ya kuwafanyia vurugu wengine, huu ni utetezi wa kishamba.

Jamaa hajui kuwa hakuna uhuru katika maswala yanayohusu haki za binadamu. Hajui kwani Tanzania ni mwanachama wa UN au African Union au EAC. Hajui vyombo hivyo vinaratibu mambo gani. Anadhani uhuru ni wa kufanya jambo lolote na mtu asiwajibishwe!! Dunia hiyo ilikuwepo zamani sana!! Nchi zote zina wajibu wa kuimarisha uwepo wa binadamu na maendeleo yake bila mipaka!!
 
Nakumbuka uhuru Kenyatta alikuwa anaikabidhi ikuru kwa makamo wake kisha yeye anakwenda kusimama kizimbani hukouko kwa mabeberu
 
Haina effect yoyote; na mbaya zaidi inaweza kuwa inamharibia sana Lissu kisiasa.

Nchi hii imeshakuwa na tabia ya kutokutaka kuingiliwa na watu wa nje katika mambo yao ya ndani kwa muda mrefu sana; yaani tangu tulipoanza siasa za kujitegemea- tuliwahi kufunga ubalozi wa Ujerumani na wa marekani kwa sababu za kutaka kuingilia mambo yetu ya ndani. Ingawa wakati wa Kikwete nchi hiyo iliyumba kidogo, hadi tukasimamisha ujenzi wa barabara ya Arusha-Musoma kwa kusikiliza kelele za nje, wakati huu uyumbaji huo umeondoka tenad ndiyo maana bwawa la Nyerere lilijengwa pamoja na kelele zote zilizotaka nje.

Kwa hiyo huyo Amsterdam anamdhuru Lissu kisiasa tu; barua yenyewe ni "open letter" kwenye mtandao, siyo official letter! Open letters huwa ni za kiuoga za kutaka kuepelea ujumbe bila kuwa kuwa na haja ya kuusimamia ujumbe huo
 
Polisi wakiongozwa na IGP na NEC wafanye kazi zao kwa usawa na haki vinginevyo wakifanya kazi ili wamfurahishe mtu mmoja nawaambia lolote baya litakalo tokea mwaka huu wao ndio watajibu na sio huyo mtu mmoja wanae taka kumfurahisha. Wanasemaga akili za kuambiwa... Kazi kwenu
huyo mtu mmoja sio mkubwa kuliko nchi na si lazima awe raisi ii aishi afanye hata kazi zingine lakini amani yetu na nchi yetu i muhimu zaidi,uraisi sio cheo cha kudumu
 
Mnachekesha, sisi ni nchi huru, tunajiamlia mambo yetu. Wazungu wajanja hapo hiyo gharama imeahidiwa kulipwa kwa mikataba minono ya upendeleo atakayo itoa lisu pindi akiwa rais (kitu ambacho hawezi kuwa rais maana watamuua akishindwa urais).
Kumbe mmepanga kumuua mkifanikiwa kumpoka urais.
 
Polisi na tume kama wangeamua kutenda HAKI na kuheshimu maamuzi ya Watanzania kila kona Nchini kuhusu nani anayestahili kuwa Mbunge wa Jimbo na nani anastahili kuwa Rais wa Nchi hii barua kutoka Amsterdam Partners & LLP isingekuwa tishio kwao, lakini kwa kuwa wanajua dhambi zao tangu 1995 sasa wanaweweseka.
Hakika mkuu..

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Je, hizi zinaweza kuwa dalili kwa jeshi la polisi kuanza kubadilika au ni kwa sababu ya vitisho vya barua za Robert Amsterdam?
Polisi wakifanya kazi mnasema wameogopa barua
Polisi wamewaachia mumpokee lissu mkajiuliza kulikoni
Serikali ipo kimya mkajiuliza mbona kimya kingi?
Mlishazoea vurugu na maandamano ili kuhalalisha kushindwa kwenu
Mwaka huu mnapigwa kweupeee na hamtapata nafasi ya kufanya vurugu
 
The police force in Tanzania have a reputation for being very unprofessional in the way they perform their duties.

Needless to say the police are being used by the ruling party as the militant wing for the party to harass, torment and intimidate the government critics both real and perceived. That's what is known of the discredited Tanzania police force.
 
Polisi wakifanya kazi mnasema wameogopa barua
Polisi wamewaachia mumpokee lissu mkajiuliza kulikoni
Serikali ipo kimya mkajiuliza mbona kimya kingi?
Mlishazoea vurugu na maandamano ili kuhalalisha kushindwa kwenu
Mwaka huu mnapigwa kweupeee na hamtapata nafasi ya kufanya vurugu
Watu lazima washangae mambo yanatokea kinyume na ilivyozoeleka kwani wamezoea kuona ubabe mwingi na ukiukwaji wa sheria toka kwa hawa polisi.
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom