Polisi Na Makahaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Na Makahaba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mfamaji, Jul 22, 2008.

 1. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Polisi Jijini wazidi kuwasomba makahaba

  2008-07-21 19:15:44
  Na Moshi Lusonzo, Polisi Kati


  Wanawake 21 na wanaume watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Ilala kwa tuhuma za kufumwa usiku wakidaiwa kufanya biashara ya ukahaba.

  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogire amesema wanawake hao na wanaume hao walikamatwa jana mishale ya saa 2:00 usiku katika baa za Kimboka, Asemwe na Sehewa silizopo Ilala.

  Akasema wanawake hao walikamatwa wakiwa katika maeneo hayo wakituhumiwa kufanya biashara ya uchangudoa wakati wanaume hao wanatuhumiwa kuwa wateja.

  Amesema watu hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

  Hivi hawa manjagu wa Kibongo wanaelewa kuwa ukahaba ni deal kwa wenzetu waliokwisha ona mbele? Wanalipa kodi na the game is authorised.
  Hapa bongo badala ya kuhangaika na ujambazi wanahangaika na kina dada poa. Wanatumia magari, pikipiki ,mishahara etc kupamabana na wanaouza na kununua ngono. Can,t they set priorities?
   
 2. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2008
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35


  Heshima mbele mkuu, nafikiri katika hili huwatendei haki askari kwani biashara hii ni haramu kwa nchi kama Tanzania na ni haramu katika maadili yetu ya kitanzania.Kodi ya uchangudoa si tu ni chafu mbele za mungu lakini pia ni chafu mbele ya mtu yoyote mwenye mapenzi mema. Hili si wazo jema unalokuja nalo na ninafikiri hatutakiwi tufike mahala ambapo biashara ya ukahaba itahalalishwa ni kama kupigia debe kuhalalishwa uuzaji wa gongo mkuu!
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Sawa mkuu. Sio lazima ihalalishwe. Lakini ni jambo linalotusumbua zaidi kuliko yote hadi wavalie njuga?. Tuna matatizo kibao zaidi ya uchangudoa.
   
Loading...