Polisi na fuvu la kichwa cha binandamu: Je, siyo fuvu hili hili lilitumika pia katika tukio la 2009

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
POLISI NA FUVU LA KICHWA CHA BINANDAMU: JE, SIYO FUVU HILI HILI LILITUMIKA PIA KATIKA TUKIO HILI LA 2009

Katikati ya wiki hii ambayo wizara la mambo ya ndani iliwakilisha bajeti yake na jeshi la polisi kujikuta katika lawama kubwa saana ya kubabikiza wananchi kesi, japo ndani ya bunge ilionekana kanakwamba iliwahusu saana wapinzani kwa maana ya CHADEMA. Lakini katikati ya wiki hii mambo yalijiziirisha wazi, pale polisi watatu na raia moja walipokamatwa na fuvu la kichwa cha binadamu, wakiwa wamekula njama ya kumbambikia raia kesi ya mauaji na baadaye kuomba rushwa.
Niliona habari hizi kupitia taarifa ya habari ya ITV na badaye kuzisoma katika vyanzo mbalimbali vya habari. Nilisikitishwa saana na kitendo hiki, ukizingatia kwamba, kesi ya mauaji haina dhamana na ni kesi zinazochukua muda mrefu saana katika nchi yetu. Kwa maana ya kwamba, ukibambikiwa kesi hii na ukashikiliwa na vyombo vya usalama pasipo ushahidi kwa muda mrefu, mipango mingi na pamoja na familia ya mtuhumiwa wanapoteza malengo yao yote katika maisha. Polisi kama hawa, siyo wa kuwavumulia hata kidogo, sijui kwanini wananchi waliruhusu watu kama hawa kuendelea kuishi na mppaka kuwafikisha kituo cha polisi, anyway, pengine Mungu alitaka haya yadhihirike miongoni mwa watanzania na hasa kwa waziri anayeshughulikia mambo haya.

Nimejaribu kuvuta kumbukumbuku zangu, kuhusu tukio kama hili, liliwahi kutokea huko kibaha. Masikini, sielewi hii kesi ilishaje au bado ipo na watuhumiwa bado wako ndani kwa kesi ya mauaji. Habari hii iliandikwa katika gazeti la TANZANIA DAIMA (Waliokamatwa na fuvu la kichwa washtakiwa kwa mauaji) mwaka 2009. Kwa mazingira ya upekuzi wa kesi hii na taarifa za mjumbe wa nyumba kumi, majirani an ndugu wa watuhumiwa walioshiriki kwenye upekuzi wa kesi hii tajwa, napata wasi wasi, kwamba hili FUVU LA KICHWA CHA BINADAMU huenda ndilo limekuwa likitumika kubabikiza wananchi kuhusika na kesi za mauaji. Je, ni wananchi wangapi wamekutana na fuvu hili na kulizwa pesa zao? Ni wangapi wamewekwa rumande kutokana na fuvu hili.
Hebu soma habari hizi mbili na unganisha dots uone kwanini nakuwa na wasiwasi na hili fuvu na polisi wetu.

Waliokamatwa na fuvu la kichwa washtakiwa kwa mauaji
TANZANIA DAIMA 2009
na Julieth Mkireri, Kibaha

C:\DOCUME~1\ADMINI~1\LOCALS~1\Temp\msohtml1\01\clip_image001.gif

WANANDOA, Ally Ramadhani (36) maarufu kama Puku na Mwanaidi Ramadhani (34), wakazi wa Maili moja, Wilaya ya Kibaha, ambao walikutwa na fuvu la kichwa cha binadamu nyumbani kwao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha kujibu shtaka la mauaji.
Wanandoa hao walifikishwa jana mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Sekela Mwaiseje, wakikabiliwa na kesi ya mauaji yaliyofanyika tarehe isiyojulikana.
Washtakiwa hao walidaiwa kuwa siku isiyofahamika, walimuua mtu asiyefahamika na kubaki na fuvu la kichwa chake ambalo lilikutwa nyumbani kwao Desemba 30 mwaka jana.
Baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa kesi za mauaji husikilizwa Mahakama Kuu. Kesi itatajwa Januari 21 mwaka huu na watuhumiwa wamepelekwa rumande.
Habari zilizopatikana nje ya mahakama, zimeonyesha utata umegubika upatikanaji wa fuvu hilo kutokana na ndugu wa mshtakiwa Ramadhani kudai fuvu hilo lilipatikana mlangoni mwa geti la kuingilia katika nyumba hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, balozi wa nyumba kumi katika Mtaa wa Central, Maili Moja, Damiani Mbalamula, alidai polisi alioongozana nao katika upekuzi kwenye nyumba ya mfanyabiashara huyo hakupata kitu ndani ya nyumba na badala yake fuvu hilo lilipatikana pembeni mwa geti la nje ya nyumba hiyo.
Mbalamula alidai taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani humo hazikuwa sahihi ambazo zilidai kuwa fuvu hilo lilipatikana ndani ya nyumba na uvunguni mwa kitanda anacholala mfanyabiashara huyo.
“Mimi kama balozi nilishirikishwa kwenye upekuzi huo na nilishuhudia sadolini yenye fuvu ikiwa kwenye geti la kuingilia ndani ya nyumba hiyo na si chumbani kama taarifa ya polisi ilivyodai,” alidai balozi huyo.
Kwa upande wake, ndugu wa mfanyabiashara huyo, Ridhiwan Ramadhani, alidai polisi wamepotosha taarifa, kwani hawakuweka wazi kile walichoshuhudia.
Ridhwan, alisema wakati polisi wanataka kufanya upekuzi katika nyumba hiyo aliwashauri awepo na balozi kama shahidi na kwamba kwa mujibu wa maelezo waliyopewa na mtoa taarifa fuvu hilo lilikuwa ndani getini na ndipo walipolikuta.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, hakupatikana kuzungumzia madai hao yalitolewa na balozi na ndugu wa mshtakiwa huyo.



[h=2]Polisi wakamatwa na fuvu la binadamu[/h]
MTANZANIA: IJUMAA, MEI 10, 2013 04:42 NA MERINA ROBERT, KILOSA
*Wadaiwa kulitumia kuomba rushwa kwa mfanyabiashara
*Washikiliwa kituo cha polisi kwa mahojiano
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limeingia kwenye kashfa nzito baada ya askari wake watatu na raia wanne kukamatwa wakiwa na kichwa cha binadamu. Tukio hilo lilitokea Mei 7 mwaka huu katika eneo la Mgudeni- Dumila wilayani Kilosa.
Inaelezwa kuwa polisi hao kwa kushirikiana na raia hao walikwenda nyumbani kwa mfanyabiashara Samson Mura na kutaka kumbambikizia kesi ya mauaji.

Mbali ya kubambikizia kesi hiyo, polisi hao wanadaiwa kuomba wapewe Sh milioni 25 na mfanyabiashara huyo ili wasimpeleke kituoni.

Wakizungumza na MTANZANIA jana, baadhi ya wananchi walisema wameshangazwa na askari hao ambao wawili ni wa Kituo cha Polisi Dumila na mmoja wa Kituo cha Polisi Mvomero.

Walisema siku ya tukio, polisi hao walifuatana na raia mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya masuala ya usalama.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgudeni,Zaituni Kifutu alisema walishangazwa na tukio hilo.

“Tumeshangazwa mno na askari hawa… sijui walichukulia wapi mafunzo yao? Kama walibaini kuwapo tukio hili kwa nini hawakutaka kulifikisha kituoni?

“Inasikitisha mno, eti wao kwa kushirikiana na mfanyabiashara wanakwenda kudai kwa mwanakijiji mwenzetu wapewe Sh milioni 25… haiingi akilini hata kidogo wakamate mhalifu halafu washirikiane kwenda kuomba fedha.

“Tunaona na mazingira ambayo askari na raia huyo ambao walifika kwenye nyumba ya mfanyabiashara huyo, Samson Mura na kumtuhumu kukutwa na kichwa hicho si mazuri ni ya kutaka kumbambikizia kesi tu. Yaani inasikitisha jeshi kujaa uozo kiasi hiki,”alisema Kifutu.

Naye Musa Magisu alisema polisi hao walifika kwenye nyumba ya Mura na kufanya upekuzi ambao hata hivyo hawakuambulia kitu.

“Pamoja na kupekua kwa nguvu kubwa, hawakukuta kitu. Sisi tunamfahamu Mura ana silaha yake ambayo anamiliki kisheria,”alisema.

Alisema baada ya polisi hao kutoka nje ya nyumba walikwenda moja kwa moja kwenye gari lililokuwa limeegeshwa nje ya nyumba.

“Baada ya kufika kwenye gari, yule raia na wale polisi waliona kuna mfuko wa rambo chini na ghafla wakaanza kuuliza eti mfuko huu una nini na walipofungua wakakuta kuna kichwa cha binadamu.

“Yaani baada ya kukuta kichwa kile, walimuamuru mfanyabiashara yule atoe Sh milioni 25 lakini alikataa katakata akidai hajawahi kufanya tukio la aina hiyo,”alisema.

Alisema mpaka sasa hawajui kwa nini polisi ambao ni walinzi wa raia na mali zao, wamegeuka watu wa kumbambikizia kesi wananchi wasio na hatia.

Ofisa Upelelezi Msaidizi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro, Asifiwe Ulime alikiri kutokea tukio hilo na kusema mpaka sasa polisi hao wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Alisema hata yeye mwenyewe, alifika eneo la tukio na kushuhudia fuvu.

“Tunawashikilia polisi watatu na mwananchi mmoja kwa mahojiano ili watoe maelelezo ya kina juu ya tukio hili,”alisema.

Kutokana na hali hiyo, Ulime amewaomba wananchi wa Dumila kuwa watulivu wakati uchunguzi unaendelea.
 
kubambikiwa watu kesi hapa tanzania ni jambo linaloanzia ccm na polisi.utakumbuka polisi wa airport walikuwa makibambikia watu madawa ya kulevya,huko moro fuvu na hata ya kibaha naamini ni ubambikaje tu. MWIGULU LAMECK NCHEMA NAE NI BINGWA WA KUBAMBIKA KESI.
 
Njaa zitawaua na kuwahukumu hao jamaa. Leo nimeona gari 1 la polisi hapa tabora linafanya kazi za mabasi ya kubeba abiria. Lilikuwa linaenda katavi likapita stendi ya tabora na kusanya watu mpaka katavi eti wanakula vichwa! Je wakipata ajali huko safarini, abiria wanahaki ya kutibiwa na jeshi la polisi? Bro njaa mbaya sana.
 
Back
Top Bottom