Polisi na dola wanatetemeka, kuna jambo wanalificha juu ya Abdul Nondo. Haya ndio niliyoyagundua juu yao...

-
POLISI NA DOLA WANATETEMEKA, KUNA JAMBO WANALIFICHA JUU YA ABDUL NONDO.. HAYA NDIO NILIYOYAGUNDUA JUU YAO.

Na Josephat K. Nyambeya
nyambeya@yahoo.com

Kuna msemo wa lugha ya majahazi unasema "A sunk vessel (damaged) has no rudder. What is predestined is inevitable." Kwa maana ya kwamba chombo cha kuzama hakina rubani.

Mda mfupi uliopita nimetoka kumtizama SACP Lazaro Mambosasa akihutubia waandishi wa habari wengi waliokusanyika mbele yake juu ya tukio la kutekwa kwa Abdul Nondo mwanafunzi wa UDSM na Mwenyekiti wa TSNP. Nimeyafuatilia sana matamshi ya Kamanda ( sitamuita tena kamanda) SACP Lazaro Mambosasa moja baada ya jingine, alama za mdomo wake na jinsi alivyokuwa ananata na maneno nimegundua mambo yafuatayo.

1. SACP Lazaro Mambosasa (kwa wale wasiojua maana ya SACP hicho ni Cheo cha kipolisi cha Lazaro Mambosasa.. Lazaro Mambosasa ameshindwa kuonyesha uthibitisho wa kimantiki wa maneno aliyokuwa anataka kuwaaminisha Watanzania ya kwamba Abdul Nondo alizusha, Lazaro amejikita katika kumshambulia Abdul badala ya kuonyesha ukweli wa jambo alilokuwa anawaaminisha Watanzania mbele ya kamera za waandishi. Mathalani nimeweza kumsikia akisema ya kwamba Abdul alikwenda Iringa mwenyewe kumfuata mpenzi wake waliyekuwa wanawasiliana mda wote wa safari na kuanzia usiku wa tukio lile.

Alichojisahau Mambosasa katika taarifa yake hii ni kwamba hakuwaambia waandishi wa habari juu ya huyo mpenzi wake, Anaishi wapi? Anaitwa nani? Na amehojiwa lini na kuthibitisha lini kwamba Abdul alikuwa anamfuata yeye Iringa?

2. Katika kuendeleza taarifa yake Lazaro Mambosasa amesema ya kwamba Abdul alikamatwa na Polisi wilaya ya Mafinga na kwamba hakujipeleka mwenyewe polisi kuripoti tukio hilo. Huu ni uongo na uzushi wa maksudi kutoka kwa afisa mkubwa wa Polisi ndani ya nchi. Ni wachache sana wanafikia cheo cha Lazaro Mambosasa. Ni kwa nini nasema huu ni uzushi wa maksudi kutoka kwa jeshi la polisi?

A: Kwa mujibu wa Juma Dogan ambae ni mtu wa kwanza aliyetoa taarifa za kuonekana Abdul Nondo huko Mufindi mkoani Iringa alisema kupitia ujumbe ya kwamba yeye akiwa katika safari zake za kibiashara mkoani humo alimuokota Abdul Nondo akiwa hana kitu chochote na allipojaribu kumhoji alijibiwa ya kwamba yeye ni mwanafunzi wa UDSM, Juma Dogan ambae ni kada wa Chama cha Mapinduzi kutoka Bagamoyo alisema Nondo hakuwa na kitu chochote mkononi zaidi ya nguo alizokuwa amezivaa. Hivyo iliwabidi wamkodie taksi wakiambatana nae moja kwa moja kutoka Mufindi hadi Mafinga kuliko na kituo cha polisi ili akaripoti tukio hilo. Na walipofika hapo walimuacha. Kwa mujibu wa mtoa taarifa ambae ndie aliyemuokota Abdul hakuna sehemu yoyote aliyosema ya kwamba Polisi ndio waliyomkata Abdul Nondo kama ambavyo Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari.

B: Kwa mujibu wa ujumbe alioutuma Abdul kwa rafiki yake usiku ule wa tukio hakuonyesha kwamba ametekwa au kuzingirwa na watu waliokuwa na nia ya kumteka zaidi alisema "AM AT HIGH RISK" halafu akatoweka hewani. Kwa tafsiri rahisi ya Kiswahili Nondo alionyesha kuwa usiku ule alikuwa katika hatari aijuae yeye mwenyewe na ambayo ataisema endapo atapewa nafasi ya kusema baada ya kutoka kufungiwa ndani ya kuta za polisi.

Kwa hiyo ni jambo la ajabu sana Lazaro Mambosasa kusambaza taarifa za kwamba Abdul alisambaza ujumbe wa kutekwa ili kuzua mtafaruku ndani ya nchi. Nimwambie tu SACP Lazaro Mambosasa ya kwamba anaopaswa kuwalaumu kwa kusambaza taarifa za kutekwa Abdul siyo Abdul bali Watanzania walionyesha wasiwasi wa kupotea kijana huyo ikizingatiwa ya kwamba Nondo ni kiongozi wa TSNP na mwanaharakati wa haki za wanafunzi wa mda mrefu kwa sasa nchini. Kwa kuzingatia meseji aliyoituma Nondo kwa rafiki yake hakuna sehemu aliyosema katekwa zaidi alisema yupo kwenye hatari kubwa.

Anachopaswa kukipeleleza SACP Lazaro Mambosasa ni hatari gani aliyokuwa nayo usiku huo Abdul Nondo kama alivyosema kwenye meseji aiyomtumia rafiki yake? Je alikutana na chui? je alikuwa amezungukwa na mabomu? je alikuwa kakanyaga bomu la nyuklia ? Alikumbana na hatari gani usiku huo hadi kumtumia rafiki yake ujumbe huo?

Maswali mengine anayopaswa kujiuliza SACP Lazaro Mambosasa ni kwa nini Watanzania walipatwa na taharuki sana mara tu baada ya kusambaa kwa ujumbe wa kutoonekana kwa kijana huyu? Je hii ni kawaida kwa wanachi wetu kuonyesha taharuki kiasi hiki? Kama siyo kwa nini iwe hivyo kwa siku za karibuni.

3. Jambo lingine nililoligundua kutoka kwa maneno ya Lazaro Mambosasa ni kwamba ametoa taarifa yake kwa kufuata ujumbe uliosambazwa mitandaoni mchana wa siku iliyofuata baada ya Abdul Nondo kuokotwa. Kwa wale wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii watakubaliana na mimi ya kwamba kuna mtu alijitokeza kwa akaunti feki na kuanza kusambaza ujumbe akijiita JONATHANA PEMBE na kudai ya kwamba alisafiri na Abdul Nondo huku Nondo akiwa kashifunika shuka la kimasai mda wote wa safari bila kuongea na alikuwa akiwasiliana na mtu aliyeonekana kama mwanadada mda wote wa safari. JONATHANA PEMBE huyu alidai ya kwamba yeye alikuwa amekaa seat namba G4 na Nondo kakaa seat namba G3 na kwamba sura ya Abdul Nondo aliiona mara moja tu walipofika Morogoro mjini na hakuiona tena mda wote wa safari. Mtoa taarifa huyo alipomaliza kusambaza uzushi huo mitandaoni hakuonekana tena na hata rekodi zake hazipo tena kwenye mtandao wowote hadi sasa zaidi ya taarifa yake hiyo kutumiwa na vibaraka wa serikali kuisambaza mitandaoni kwa wingi.

Ni jambo la aibu sana ya kwamba Polisi na wao bila aibu wamelala kwenye taarifa hii, SACP Lazaro Mambosasa amelala humo humo Ni kwa nini Watanzania tusione ya kwamba Jeshi la Polisi na serikali ndio waliousambaza ujumbe huu ili kupooza hasira za wananchi?

4. Jambo lingine nililoligundua kutoka kwa SACP Lazaro Mambosasa ni kwamba Lazaro anayasema haya yote ili kuwaridhisha maboss wake wa kazi, ikumbukwe ya kwamba juzi akiwa mkoani Singida Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba (PhD) alimshambulia Abdul Nondo kwamba alijiteka mwenyewe na alikuwa akinukia pafyumu alipokwenda kuripoti kituo cha polisi. Mwigulu ambae ni boss wa moja ka moja wa jeshi la polisi alionyesha kabisa kutaka kumshugulikia Abdul bila ya madai yake kusikilizwa na mahakama ambao ndio wenye mamlaka ya kujua nani kakosea na nani kakosewa? Ni kwanini wanamhukumu Nondo kabla ya kusiiliza kilichomkuta?

Boss mwingine wa Lazaro Mambosasa ambae ni RC wa Dar es Salaam Paul Makonda alisikika akimshambulia Nondo kwamba anataka kuuchafua mkoa wake na hivyo watamshugulikia? Hawa watu ukiwasikiliza vizuri utaona jinsi walivyokuwa maskini wa utashi na fikra. How can you dare to attack a victim without applying natural justice theory? How can you come up with your answers while you haven't drafted a solution? Au ndio ile Waingereza wanasema a double jointed arm moves in one motion. (Like father like son).

5. Pamoja na mambo mengine ukosefu ukweli na uwazi ni jambo lingine nililoliona katika sakata hili. Abdul ana siku saba behind bars, hajafikishwa mahakamani. Hajasikilizwa akaeleza yaliyomkuta usiku ule. Ni kwa nini jeshi la polisi na serikali wanaoonekana wakiliongelea jambo lile peke yao? Wanataka kumfunika nani ? Au ndio wanaendana na ule msemo wa
kamanda Adolf Hitler usemao By the skillful and sustained use of propaganda, one can make a people see even heaven as hell or an extremely wretched life as paradise.

Ni vipi tunaweza waamini jeshi la polisi kwamba hawafanyi propaganda kwenye jambo hili ili kulinda maslahi ya wakubwa wao?

Na kama siyo propaganda kwa nini wamewakataza mawakili kumuona Nondo ? Kwa nini wamewakataza familia yake kumuona? Na kwa nini wamekaa nae siku 7 bila kumfikisha mahakamani kujibu hizo wanazoziita shutuma dhidi yake?

Nimalizie na ujumbe niliouandika mwanzo kabisa wa makala hii ya kwamba "A sunk vessel (damaged) has no rudder. What is predestined is inevitable." Kwa maana ya kwamba chombo cha kuzama hakina rubani.

SACP Lazaro Mambosasa asitake kujifanya kuwa rubani wa chombo kinachoelekea kuzama, hakizuiliki hiki lazima kizame. Anachopaswa kufanya ni kuwaokoa abiria waliomo kwenye chombo hiki na akiache kizame bila ya kuleta madhara yoyote kwa abiria. Amani ya nchi hii haitoletwa kwa vitisho wala uongo wa kundi fulani la watu, amani ni tunda la haki na usawa. Bila ya haki na usawa kutamalaki katka ardhi ya Tanganyika yataibuka mengi.

Jeshi la polisi ni kiungo kikubwa katika usimamiaji wa haki na usawa ninawaomba wasiwe bias kwenye utendaji wao wa kazi, wasiwe watu wanaoacha manung'uniko kwa kundi lingine la watu katika utendaji wao wa kazi.

Mwisho kabisa niseme . He who digs a well will also enter it himself.Mchimba kisima hungia mwenyewe.

Ni mimi Josephat K. Nyambeya
Mwananchi wa kawaida.
nyambeya@yahoo.com
kaka kunywa maji nitakulipia
 
Naiombea nchi yangu Tanzania. Waleee...kama tungekielewa vizuri maana hiki kiapo cha "Naahidi mbele za Mungu nitakulinda mpaka siku ya kufa" Leo hii hali ingekuwa tofauti kwa kila kinachoendelea nchini.
 
wasiojulikana wanajijua wenyeweee

kwaiyo huu mchezo hauhitaji hasira wala rafuuu
 
Polisi wameshamuhukumu bwana Nondo ilihali sio Kazi yao.
Hii inapelekea kuamini Kuwa kuna jambo nyuma ya pazia. Chombo pekee kinachoweza kutoa hukumu ni mahakama.

Lakin pia, kwanini uchunguzi wa bwana Nondo umechukua muda mfupi zaidi kuliko matukio mengine??

Anyway ni kamanda Mambosasa huyu huyu alietoa taarifa potofu (awali) kuhusu Dr shika. Mpaka Akasema Kuwa huenda shika alitumwa na Lugumi ili kukwamisha mnada. Alifanya hivyo bila facts mwisho wa siku ikafahamika Kuwa shika ni mtu mwingine kabisa.

Wakati wa tukio la kifo cha Akwila, kamanda Mambosasa alikiri polisi kutumia risasi za moto na kuua, ila baadae Akasema wao walipiga risasi juu.

Hivyo huyu bwana mkubwa Si wa kumsikiliza saaana
 
Wewe ndo uwe na mwisho mbaya kwa tamaa zenu za kutaka madaraka kwa nguvu.
Hamna maana tena na magwanda yenu ya mgambo.

Wewe ndo uwe na mwisho mbaya kwa tamaa zenu za kutaka madaraka kwa nguvu.
Hamna maana tena na magwanda yenu ya mgambo.
ahi Azory Gwanda ametokaQ ana maushahidi kibaoQ wahi Tundu lisu yuko njianiQ AIBU EHHHHHHHHHH hadi yule mwenye kidevu kirefu kimeshafika magotiniQ mashetani wakubwa nyie
 
Huyu mwandishi ameongea ukweli mtupu. Kama inawezekana, hii makala atumie Kamanda Lazaro Mambosasa
 
Luge aliwahi kusema-katika maisha ogopa Mungu na Teknolojia.
Cc Mambosasa
Check hii video hapa
 

Attachments

  • VID-20180314-WA0020.mp4
    2.6 MB · Views: 23
Hautoweza kuingia barabarani mkuu
kwanini...nitaingia barabarani hata nikiwa peke yangu,bora kufa kwa risasi za polisi wakati nagombani haki yangu na kizazi kijacho,kuliko kufa kitandani maiti yangu ikazikwa nikasahaulika,,
 
Back
Top Bottom