Polisi na dola wanatetemeka, kuna jambo wanalificha juu ya Abdul Nondo. Haya ndio niliyoyagundua juu yao...

Pia Tufikirie kwa umakini taarifa ya Polisi kuhusu Abdul Nondo.

Taarifa zinadai kuwa Abdul Nondo alijiteka na kwamba alifata mapenzi huko Iringa. Zaidi ya hapo, Polisi wamepanga kumfikisha Abdul Nondo mahakamani kwa kile kinachoitwa kudanganya umma na kuzua taharuki.

Ingawa taarifa hizo zinatolewa na chombo kilichopoteza imani kwa wananchi kutokana na vitendo vyake vinavyoashiria kutumika kama idara ya chama cha siasa, CCM, bado nitajitahidi kujadili suala hili bila kujali hayo ya kutumiwa na CCM.

Kwanza, Tukio la Abdul Nondo kupotea lilitaarifiwa na marafiki zake. Yeye hakuwahi kutoa taarifa hiyo na hadi kupatikana kwake hakupata nafasi ya kujieleza. Polisi wanasemaje alidanganya umma wakati hajawahi kuongea na chombo chochote cha habari?

Pili, Taarifa za kupatikana kwake zilitokea Mafinga. Huko inadaiwa kuwa 'aliokotwa' na wasamaria wema akiwa hajitambui, ambao walimpa nauli ya kwenda polisi. Taarifa hii ina mawaa, kwamba Msamaria mwema alimpa nauli 'mtu asiyejitambua' kwenda polisi. "Inakuaje mtu asiyejitambua anapewa nauli na kwenda polisi". Hapo ilibidi mtu aliyetoa taarifa hiyo na aliyemuokota na kumpa nauli naye ahojiwe.
Tatu, Hata hivyo taarifa za polisi zinadai kuwa Abdul Nondo alikuwa salama huko Mafinga na anaendelea na shughuli zake, swali! Kwanini Jeshi la Polisi lilimkamata mtu aliye salama akiendelea na shughuli zake na kumsafirisha hadi Dar es salaam. Ikumbukwe kuwa Abdul Nondo hakutoa taarifa za kutekwa, aliwaambia marafiki zake yupo kwenye risk (hatari) bila kueleza ni hatari gani.

Nne, Ikiwa tukio la kupotea kwa Abdul ni la Kihalifu, iwe alitekwa au alijiteka, basi moja ya maeneo ya uhalifu (crime scene) huo ni Mafinga alipo'okotwa' Je! Taarifa ya jeshi la police Mafinga inasemaje? Kuna uchunguzi wowote umefanyika kubaini namna alivyofika Mafinga? Alifikiaje? Kwa basi, kwa Noah, Land cruiser au kwa punda? Taarifa za namna alivyofika Mafinga, zingepatikana kwa ushahidi usio na shaka (physical evidence) zingetoa mwangaza kuelekea uchunguzi wa tukio hili. Ikiwa alisafiri kwa basi kama inavyodaiwa, je ni basi gani? Ratiba ya basi hilo inafanana na muda unaotajwa kutokea kwa tukio hilo la kutekwa/kujiteka?

Tano, Taarifa ya Kamanda Mambosasa inadai baada ya Abdul kupoteza mawasiliano na marafiki zake, bado aliendelea kuwasiliana na mpenzi wake akiwa njiani kuelekea Mafinga. Hapo maana yake ni kuwa Abdul Nondo alibadili laini ya simu lakini akiendelea kutumia simu ileile akiwasiliana na 'mpenzi wake'. Je! Kuna mahojiano yoyote baina ya polisi na huyo 'mpenzi' anayetajwa kama sehemu ya uchunguzi?

Mwisho.
Ni ukweli kwamba suala hili linapaswa kutolewa ufafanuzi na Polisi, sio mtu au chombo kingine. Kwa bahati mbaya, jeshi la polisi limepoteza na linaendelea kupoteza imani kwa wananchi. Hii ni kutokana na matendo ya kihuni yanayofanywa na jeshi hilo. Labda kwa sababu ya kukosa uwezo na umakini (incompetence) au kwa sababu ya kutojali (negligence). Tunasubiri bila matumaini taarifa za kupotea kwa Ben Saanane, kupigwa risasi Tundu Lissu na zingine. Bila matumaini.
Kuhusu suala la Abdul Nondo, Polisi inaacha maswali mengi. Taarifa hazijiungi. Ingependeza jeshi la polisi lieleze zaidi, litoe taarifa kamili.
Abdul alikuwa wapi usiku aliotekwa/aliojiteka? Maana muda huo hakuna usafiri wa umma, asafiri kwa usafiri gani? Na kama hakusafiri usiku huo alisafiri lini? Alifika saa ngapi? Taarifa hizo ni muhimu sana katika kuwasilisha ushahidi, ili kupunguza maswali mengi na isionekane ushahidi umetengenezwa.

Ni Vema Polisi ikafanya uchunguzi wa suala hili kama ina nia. Taarifa inayoitwa ya uchunguzi iliyotolewa na kamanda Mambosasa haina hadhi ya kuitwa Taarifa ya uchunguzi. It is far from being a forensic report. Labda ni "Preliminary report".
Kumpeleka mtu mahakamani na report hiyo ni kujitafutia fedheha mbele ya mawakili wasomi.
KUNA WATU MNAAKILI NYINGI SANA ....INAKERA LINAPOJITOKEZA JITU KUJA KUJIBU HOJA NZITO KAMA HII KWA VIHOJA VYEPESI ...WAKATI MTOA HOJA UMEUMIZA KICHWA NAKUTOA UCHAMBUZI MAKINI ....HONGERA SANA AISEEE """ NIOMBEE NA MIMI NIWE NA MAWAZO YAKUJENGA HOJA NZITO NZITO KAMA HAY .....IKIBIDI UNIPE NJIA ZITAKAZO NIWEZESHA KUFIKIA HIYO HATUA ...SAFI SANA
 
Mvivu wa kusoma,jipe mazoezi ya kusoma vitabu itakusaidia...,unaweza kuongeza IQ yako kwa kusoma vitabu au magazeti...don't give up, Bro,you got a lot of time to achieve that
MPE hiyo ...dawa imuingie ..ndio maana wanaufinyu wa maarifa kwaajili yakuendekeza uvivu wa kusoma
 
Me nikionaga police inatumia nguvu nyingi kukanusha najua hilo suala ni ukweli 95% sasa kama alikiteka mbona wanatumia Nguvu nyingi kukanusha wamwache dogo nae aongee naona wakina Mwigulu wanatumia Nguvu na Makonda kumshambulia dogo hivi hii Serikali haina kazi ya kufanya
serikali inaongozwa na watu wenye vyeti fake hzo kazi zakufnya watazitoa wapi ..wana subiri muda wa shilawadu ufike wakatizame kipindi
 
Na kwa ukumbusho tu, ukitaka kujua hatuna Jeshi la polisi bali genge tu linalolinda maovu ya watawala wetu chini ya CCM, hebu someni hii ripoti iliyowahi kutolewa na msemaji wa Polisi siku Mwandishi Daud Mwangosi alipouawa kijiji cha Mgololo mkoani Iringa mwaka 2012...


Baada ya hii ripoti ya polisi kutolewa tu, ikatolewa picha iliyowaumbua polisi kuhusika na kifo hicho. Naam, hao ndio polisi wetu Tanzania.
aiseeeeee kweli wana laaana
 
Wewe mbona unataka tu tuamini ya huyo mwanafunzi na tusiamini ya polisi?una uthibitisho gani na hayo unayoandika au ni ukasuku tu wa kuwa umesikia simuli za upande mmoja,huyo mwanafunzi ana nini zaidi cha kufanya hadi atekwe na sijui una uhakika gani hata kama alitekwa kuwa alitekwa na vyombo vya usalama,acheni kushabikia ujinga wa kuichafua serikali kwa tamaa zenu za kutaka uongozi,serikali ni zaidi ya huyu mwanafunzi aliyejiteka kumbe anakula uroda kwa kimada wake
AISEEEE KWELI UJINGA MZIGO ..HIVI UMEZIELEWA HOJA ZA MUANDISHI VYEMA ..HZO HOJA HATA BABA YAKO JPM HAWEZI KUZIJIBU ..SANA SANA ATAISHIA KUSEMA USINIJIBU HIVYO MIMI WWE .......muandishi anauliza kuna ambaye amewahi kum note NONDO akisema kuwa ametekwa ..kama hakuna so anashikiliwa kwa kosa lipi ...maana waliozusha huo uzushi wakutekwa ni rafiki zake NONDO nasio nondo mwenyewe "" ifahamike kuwa Nondo alituma text kwa marafiki zake ikisema kuwa yupo kwenye hatari na hakusema kuwa hatari hiyo ni ipi ?? yaweza kuwa alikuwa anakimbizwa na mbwa ..yaweza kuwa alikuwa anaendesha Gari likapinduka nakupata ajali " yaweza kuwa alikuwa ametumbukia ndani ya kisima etc ..sasa mnawezaje kusema kuwa Jamaa alijiteka wakati kinywa chake hakija sema kuwa alitekwa """" ?? hilo kosa mlilo mpachika mlipaswa kuwapachika walioitoa hiyo taarifa na wananchi walio saidia kuisambaza na sio kuipachika kwa Abdul nondo

MNAAKILI LAKINI MNATUMIA MAKALIO KUFIKIRI ..EMPTY SET WAHED
 
-
POLISI NA DOLA WANATETEMEKA, KUNA JAMBO WANALIFICHA JUU YA ABDUL NONDO.. HAYA NDIO NILIYOYAGUNDUA JUU YAO.

Na Josephat K. Nyambeya
nyambeya@yahoo.com

Kuna msemo wa lugha ya majahazi unasema "A sunk vessel (damaged) has no rudder. What is predestined is inevitable." Kwa maana ya kwamba chombo cha kuzama hakina rubani.

Mda mfupi uliopita nimetoka kumtizama SACP Lazaro Mambosasa akihutubia waandishi wa habari wengi waliokusanyika mbele yake juu ya tukio la kutekwa kwa Abdul Nondo mwanafunzi wa UDSM na Mwenyekiti wa TSNP. Nimeyafuatilia sana matamshi ya Kamanda ( sitamuita tena kamanda) SACP Lazaro Mambosasa moja baada ya jingine, alama za mdomo wake na jinsi alivyokuwa ananata na maneno nimegundua mambo yafuatayo.

1. SACP Lazaro Mambosasa (kwa wale wasiojua maana ya SACP hicho ni Cheo cha kipolisi cha Lazaro Mambosasa.. Lazaro Mambosasa ameshindwa kuonyesha uthibitisho wa kimantiki wa maneno aliyokuwa anataka kuwaaminisha Watanzania ya kwamba Abdul Nondo alizusha, Lazaro amejikita katika kumshambulia Abdul badala ya kuonyesha ukweli wa jambo alilokuwa anawaaminisha Watanzania mbele ya kamera za waandishi. Mathalani nimeweza kumsikia akisema ya kwamba Abdul alikwenda Iringa mwenyewe kumfuata mpenzi wake waliyekuwa wanawasiliana mda wote wa safari na kuanzia usiku wa tukio lile.

Alichojisahau Mambosasa katika taarifa yake hii ni kwamba hakuwaambia waandishi wa habari juu ya huyo mpenzi wake, Anaishi wapi? Anaitwa nani? Na amehojiwa lini na kuthibitisha lini kwamba Abdul alikuwa anamfuata yeye Iringa?

2. Katika kuendeleza taarifa yake Lazaro Mambosasa amesema ya kwamba Abdul alikamatwa na Polisi wilaya ya Mafinga na kwamba hakujipeleka mwenyewe polisi kuripoti tukio hilo. Huu ni uongo na uzushi wa maksudi kutoka kwa afisa mkubwa wa Polisi ndani ya nchi. Ni wachache sana wanafikia cheo cha Lazaro Mambosasa. Ni kwa nini nasema huu ni uzushi wa maksudi kutoka kwa jeshi la polisi?

A: Kwa mujibu wa Juma Dogan ambae ni mtu wa kwanza aliyetoa taarifa za kuonekana Abdul Nondo huko Mufindi mkoani Iringa alisema kupitia ujumbe ya kwamba yeye akiwa katika safari zake za kibiashara mkoani humo alimuokota Abdul Nondo akiwa hana kitu chochote na allipojaribu kumhoji alijibiwa ya kwamba yeye ni mwanafunzi wa UDSM, Juma Dogan ambae ni kada wa Chama cha Mapinduzi kutoka Bagamoyo alisema Nondo hakuwa na kitu chochote mkononi zaidi ya nguo alizokuwa amezivaa. Hivyo iliwabidi wamkodie taksi wakiambatana nae moja kwa moja kutoka Mufindi hadi Mafinga kuliko na kituo cha polisi ili akaripoti tukio hilo. Na walipofika hapo walimuacha. Kwa mujibu wa mtoa taarifa ambae ndie aliyemuokota Abdul hakuna sehemu yoyote aliyosema ya kwamba Polisi ndio waliyomkata Abdul Nondo kama ambavyo Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari.

B: Kwa mujibu wa ujumbe alioutuma Abdul kwa rafiki yake usiku ule wa tukio hakuonyesha kwamba ametekwa au kuzingirwa na watu waliokuwa na nia ya kumteka zaidi alisema "AM AT HIGH RISK" halafu akatoweka hewani. Kwa tafsiri rahisi ya Kiswahili Nondo alionyesha kuwa usiku ule alikuwa katika hatari aijuae yeye mwenyewe na ambayo ataisema endapo atapewa nafasi ya kusema baada ya kutoka kufungiwa ndani ya kuta za polisi.

Kwa hiyo ni jambo la ajabu sana Lazaro Mambosasa kusambaza taarifa za kwamba Abdul alisambaza ujumbe wa kutekwa ili kuzua mtafaruku ndani ya nchi. Nimwambie tu SACP Lazaro Mambosasa ya kwamba anaopaswa kuwalaumu kwa kusambaza taarifa za kutekwa Abdul siyo Abdul bali Watanzania walionyesha wasiwasi wa kupotea kijana huyo ikizingatiwa ya kwamba Nondo ni kiongozi wa TSNP na mwanaharakati wa haki za wanafunzi wa mda mrefu kwa sasa nchini. Kwa kuzingatia meseji aliyoituma Nondo kwa rafiki yake hakuna sehemu aliyosema katekwa zaidi alisema yupo kwenye hatari kubwa.

Anachopaswa kukipeleleza SACP Lazaro Mambosasa ni hatari gani aliyokuwa nayo usiku huo Abdul Nondo kama alivyosema kwenye meseji aiyomtumia rafiki yake? Je alikutana na chui? je alikuwa amezungukwa na mabomu? je alikuwa kakanyaga bomu la nyuklia ? Alikumbana na hatari gani usiku huo hadi kumtumia rafiki yake ujumbe huo?

Maswali mengine anayopaswa kujiuliza SACP Lazaro Mambosasa ni kwa nini Watanzania walipatwa na taharuki sana mara tu baada ya kusambaa kwa ujumbe wa kutoonekana kwa kijana huyu? Je hii ni kawaida kwa wanachi wetu kuonyesha taharuki kiasi hiki? Kama siyo kwa nini iwe hivyo kwa siku za karibuni.

3. Jambo lingine nililoligundua kutoka kwa maneno ya Lazaro Mambosasa ni kwamba ametoa taarifa yake kwa kufuata ujumbe uliosambazwa mitandaoni mchana wa siku iliyofuata baada ya Abdul Nondo kuokotwa. Kwa wale wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii watakubaliana na mimi ya kwamba kuna mtu alijitokeza kwa akaunti feki na kuanza kusambaza ujumbe akijiita JONATHANA PEMBE na kudai ya kwamba alisafiri na Abdul Nondo huku Nondo akiwa kashifunika shuka la kimasai mda wote wa safari bila kuongea na alikuwa akiwasiliana na mtu aliyeonekana kama mwanadada mda wote wa safari. JONATHANA PEMBE huyu alidai ya kwamba yeye alikuwa amekaa seat namba G4 na Nondo kakaa seat namba G3 na kwamba sura ya Abdul Nondo aliiona mara moja tu walipofika Morogoro mjini na hakuiona tena mda wote wa safari. Mtoa taarifa huyo alipomaliza kusambaza uzushi huo mitandaoni hakuonekana tena na hata rekodi zake hazipo tena kwenye mtandao wowote hadi sasa zaidi ya taarifa yake hiyo kutumiwa na vibaraka wa serikali kuisambaza mitandaoni kwa wingi.

Ni jambo la aibu sana ya kwamba Polisi na wao bila aibu wamelala kwenye taarifa hii, SACP Lazaro Mambosasa amelala humo humo Ni kwa nini Watanzania tusione ya kwamba Jeshi la Polisi na serikali ndio waliousambaza ujumbe huu ili kupooza hasira za wananchi?

4. Jambo lingine nililoligundua kutoka kwa SACP Lazaro Mambosasa ni kwamba Lazaro anayasema haya yote ili kuwaridhisha maboss wake wa kazi, ikumbukwe ya kwamba juzi akiwa mkoani Singida Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba (PhD) alimshambulia Abdul Nondo kwamba alijiteka mwenyewe na alikuwa akinukia pafyumu alipokwenda kuripoti kituo cha polisi. Mwigulu ambae ni boss wa moja ka moja wa jeshi la polisi alionyesha kabisa kutaka kumshugulikia Abdul bila ya madai yake kusikilizwa na mahakama ambao ndio wenye mamlaka ya kujua nani kakosea na nani kakosewa? Ni kwanini wanamhukumu Nondo kabla ya kusiiliza kilichomkuta?

Boss mwingine wa Lazaro Mambosasa ambae ni RC wa Dar es Salaam Paul Makonda alisikika akimshambulia Nondo kwamba anataka kuuchafua mkoa wake na hivyo watamshugulikia? Hawa watu ukiwasikiliza vizuri utaona jinsi walivyokuwa maskini wa utashi na fikra. How can you dare to attack a victim without applying natural justice theory? How can you come up with your answers while you haven't drafted a solution? Au ndio ile Waingereza wanasema a double jointed arm moves in one motion. (Like father like son).

5. Pamoja na mambo mengine ukosefu ukweli na uwazi ni jambo lingine nililoliona katika sakata hili. Abdul ana siku saba behind bars, hajafikishwa mahakamani. Hajasikilizwa akaeleza yaliyomkuta usiku ule. Ni kwa nini jeshi la polisi na serikali wanaoonekana wakiliongelea jambo lile peke yao? Wanataka kumfunika nani ? Au ndio wanaendana na ule msemo wa
kamanda Adolf Hitler usemao By the skillful and sustained use of propaganda, one can make a people see even heaven as hell or an extremely wretched life as paradise.

Ni vipi tunaweza waamini jeshi la polisi kwamba hawafanyi propaganda kwenye jambo hili ili kulinda maslahi ya wakubwa wao?

Na kama siyo propaganda kwa nini wamewakataza mawakili kumuona Nondo ? Kwa nini wamewakataza familia yake kumuona? Na kwa nini wamekaa nae siku 7 bila kumfikisha mahakamani kujibu hizo wanazoziita shutuma dhidi yake?

Nimalizie na ujumbe niliouandika mwanzo kabisa wa makala hii ya kwamba "A sunk vessel (damaged) has no rudder. What is predestined is inevitable." Kwa maana ya kwamba chombo cha kuzama hakina rubani.

SACP Lazaro Mambosasa asitake kujifanya kuwa rubani wa chombo kinachoelekea kuzama, hakizuiliki hiki lazima kizame. Anachopaswa kufanya ni kuwaokoa abiria waliomo kwenye chombo hiki na akiache kizame bila ya kuleta madhara yoyote kwa abiria. Amani ya nchi hii haitoletwa kwa vitisho wala uongo wa kundi fulani la watu, amani ni tunda la haki na usawa. Bila ya haki na usawa kutamalaki katka ardhi ya Tanganyika yataibuka mengi.

Jeshi la polisi ni kiungo kikubwa katika usimamiaji wa haki na usawa ninawaomba wasiwe bias kwenye utendaji wao wa kazi, wasiwe watu wanaoacha manung'uniko kwa kundi lingine la watu katika utendaji wao wa kazi.

Mwisho kabisa niseme . He who digs a well will also enter it himself.Mchimba kisima hungia mwenyewe.

Ni mimi Josephat K. Nyambeya
Mwananchi wa kawaida.
nyambeya@yahoo.com
Mwananchi wa kawaida lakini si wa kawaida.
 
Screenshot_20180314-133449.png
 
Hivi watu hawaonagia aibu kudanganya!?
Unakubalije mtu akulishe maneno ya uongo na unajua kabisa kua ni uongo!??
Tena baba jitu zima lenye familia perhaps ad wajukuuuu
Shame on youu all kuanzia sizonje ad ao vbaraka wake
 
mapoint ulioyoongea hakuna police wa kuyajipu, polisi ya sasa ni jipu, wanampa full vitisho, watamfanya kama wema sasa hivi anakula na watesi wake.
 
Hivi katika hizo press waandishi wa habari hua hawaruhusiwi kuuliza maswali? Mfano Sawa bwana SACP tumekusikia upande wako tungependa kusikia na upande wa abdul nondo je lini mtamtoa ili tunsikilize upande wake pia?

Waandishi wa habari ni wachache sana ila kanjanjas ni wengi kama yule wa tbc alimuuliza mkuu unapenda nini baada ya kazi?
 
Nimekuelewa sana. najiuliza tu, Mbona wanamshambulia sana huyu kijana wa watu bila kutusikilizisha yeye anasema nini kuhusu hoja zao. wamebaki tu kumshikilia polisi. Apewe haki yake ya kusikilizwa na aje na yeye kwenye vyombo vya habari atolee ufafanuzi kipi kilimkuta na taarifa hizo za makamanda wa polisi ni za kweli. Kumnyima na kumshikiria huku viongozi wa serikali wakibwabwaja maneno jana kutwa nzima ni uonevu.
 
Mabosi wa mambosasa walishasema alijuteka,huo ndio uchunguzi was boss bashite,mambo hana uchunguzi tens.
 
Back
Top Bottom