Polisi Mwanza waua jambazi mmoja, askari ajeruhiwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Mwanza. Polisi mkoani Mwanza wamemuua jambazi mmoja baada ya kujibizana kwa risasi muda huu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi ambaye yuko kwenye eneo la tukio, amesema katika tukio hilo, askari mmoja amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni na jambazi huyo aliyeuawa ambaye alikuwa na mwenzake anayedaiwa kukimbilia kwenye majabali ya mawe.

Amesema majibizano hayo yalianza saa 6.20 katika Mtaa wa Utemini, baada ya polisi waliokuwa doria kufuatilia nyendo za watu hao.

“Tulipokea taarifa kutoka kwa rai wema kuwa katika eneo hilo kuna watu wanaowatilia shaka, ndipo askari wakaamua kuwafuatilia.

Hata hivyo, amesema wamefanikiwa kukamata bastola moja iliyokuwa ikitumiwa na jambazi huyo.

“Unasikia milio hiyo ya risasi, askari wanaendelea kumsaka huyo mmoja aliyejificha kwenye mawe, naimani tutampata tu na hatuondoki hapa mpaka tumtie mikononi,” alisema Msangi na kuongeza:

“Hawa ni majambazi sugu ambao walikuwa wakituhumiwa kufanya matukio uporaji na mauaji jijini hapa, tulikuwa tukiwasaka kwa muda mrefu.”

Chanzo: Mwananchi
 
Wakimpata akiwa marehemu wananchi tutafurahi sana, tumechoka na hao watu samahani lakini
 
Alfajiri ya Leo nimesikia milipuko kama ya mabomu na baada ya kuuliza nimeambiwa tukio hilo limeanza jana SAA 3.30 usiku.
Watu hao wanasemekana wamejiicha kwenye mapango katika eneo hilo LA kata ya mkolani ambako hivi karibuni watu walichibjwa wakiwa msikiti.

Inadaiwa polisi waneomba msaada wa jeshi kukabiliana na watu hao ambao wamepambana kwa zaidi ya SAA nane.

Milipuko imesikika maeneo ya buhongwa, stendi ya nyegezi had nganza sekondari jirani na chuo kikuu cha saut.

Magari kadhaa yakiwa na askari polisi yalionekana jana yajipita maeneo ya nyegezi Kuelekea buhongwa ambapo taarifa za awali zilisema majambazi wamevamia eneo LA relini.
 
Leo nimeamini memba wengi wa jf Mwanza wanachofahamu ni kuripoti mikutano ya vyama tu basi! Hii habari ya majambazi wa Mwanza ilianza kusambaa hapa tangu jana saa tatu usiku, Leo asubuhi nilikuwa hapa mjini kati na watu wengi wakuwa wakiongea kuhusu milio ya risasi ambazo wanasema sio za kawaida wanadai ni kama makombora na pia wanadai polisi wamezidiwa maana hao majambazi sehemu walipo ni kwenye mapango na mapang yapo juu kwenye ki-mlima hivi kwahiyo polisi wapo chini hivyo maadui wanawaona polisi kirahisi.

Eneo lenyewe linaitwa Kanyelele, hadi mchana wa Leo nasikia bado "vita" inaendelea! Naelekea huko ntawapa update za kuhusu kinachoendelea!
 
Vipi kama wangemkamata akiwa hai ili wamuhoji ili kuweza kuwapata majambazi wengine.
 
Taarifa kamili bado tu
ujue tokea jana nipo hapa grocery nasubiria hiyo taarifa kamili
Leteni habari kamili
 
ITV imeriport walio kufa ni majambazi wa 3.
Kiukweli usiku zimelia sana maana binafsi sikulala nilikuwa naskilizia milio ya mashine tu mpaka kuna kucha.
 
Mza ooh Mza eeh.... Habari zinasema jambazi mwingine ameuawa Leo asubuhi eneo LA msumbiji jijini humo. Hiyo ndo Mza bujibuji wasemaje?
 
Connect dots
Mkolani ndiko walikouawa waumini msikitini
Wauaji wakidai kuwa kwa nini wanasali wakati wenzao wanashikiliwa na polisi
Na waliokuwa wanashikiliwa na polisi wanashikiliwa kwa tuhuma za kuvamia maduka ya M-PESA.

Mkolani ndiko limetokea tukio la leo na polisi wamepata info kutoka kwa jambazi/gaidi mmoja kati yao waliyemkamata juzi tarehe 4.06.2016 kwa tuhuma za kuvamia maduka ya M-PESA na baada ya kukili kosa alikubali kuwapeleka polisi walikojificha wenzake (kulingana na taarifa ya polisi kuhusu tukio la leo iliyochapishwa na mtandao wa Muungwana)

Sasa nawashangaa mnaopinga tukio hili kulihusianisha na ugaidi hivi hamuoni kuwa matukio haya yana uhusiano ulio dhahili kabisa.? Hivi kuchinja waumini msikitini sio ugaidi?
 
Haya majambazi yana udhi sana, yana nguvu lakini hayataki kufanya kazi halali, acha yauwawe kabisa, na yange kamatwa hai yachinjwe kam kuku.
 
Back
Top Bottom