POLISI Mwanza Wapiga STOP Mkutano wa Hadhara wa CHAGULANI: Hofu ya makundi yatanda CDM

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
POLISI Mwanza Wapiga STOP Mkutano wa Hadhara wa CHAGULANI:
  • Hofu ya makundi yatanda CDM
  • Kambi za wanasiasa wenye uchu na mapandikizi Kukitafuna Chama

Kuna kila dalili za wazi kuwa zile kambi mbili ambazo zimekuwa zikitajwa kuitafuna CDM katika Mkoa wa Mwanza zinaendelea kuimarika hasa baada ya maamuzi ya kuondosha mapandikizi kulikofanywa na kamti kuu.

GR anaendelea kusaka kiini cha kambi hizi na athari zake katika majaaliw ya CDM mwanza (tutakutana katika thread nyingine juu ya hili)

Hadhari kubwa na mashaka yanaelekezwa kwa Viongozi wa CDM ambao mara kadhaa wameshutumiwa hapa jamvini kwa kuendekeza makundi na kuonyesha dhahiri ulafi wa madaraka ambao umeendelea kuwa kansa inayoutafuna umahiri na kasi ya CDM katika baadhi ya maeneo Nchini ambayo mtandao wao unaonekana kushamiri huku Mwanza ikiwa moja ya vitovu vya uasi huu.

Mdi haya ambayo yamekiwa yakipuuzwa au hata kupewa majibu mepesi wakti mwingine sasa ni wazi kuwa hatua za madhubuti zinahitajika kama ninavyojidhihiri kwenye my take hapo chini.

Hapa tunaguswa na uamuzi huu wa siku chache Baada ya kuenguliwa uanachama wa CDM kwa madai ya kukiuka kanuni na miongozo ya Chama, Chagulani Ibrahim Adam pamoja na Henry Matata walipanga kufanya mkutano wa hadhara jijini Mwanza kuelezea mustakbal wao baada ya uamuzi wa kamati kuu ya CDM.

Chanzo cha GR kutoka Jeshi la Polisi Mwanza(Jina linahifadhiwa) kililazimika kusitisha mkutano huo kutokana na kuwepo na tetesi za kugawanyika kwa makundi ya wafuasi wa CDM huku kundi jingine linalomuunga mkono Mmoja wa Viongozi wa Chama hicho (jina linahifadhiwa hadi kukamilika kwa uchunguzi wa madai haya) anayedaiwa kuwa na bifu la muda mrefu na kambi inayomuunga mkono Chagulani.

Katika hatua nyingine inasemekana kuwa wanasiasa hao waliopokwa uanachama watakutana leo na mwanasheria wao kujipanga kufungua madai ambayo GR na wanyetishaje wake huko mza hawajayabaini ila harakati zikifanikiwa tutakutana nayo hapa jamvini.

My Take

  1. CDM msiridhike na maamuzi ya kamati kuu fuatilieni matokeo baada ya maamuzi haya kuepusha dalili za makundi katika chama kama ambayo yanawatafuna nyinyiemi kwa sasa.
  2. Chagulani sijui kama uamuzi huu ulikuwa wa busara kwa sasa?

<font size="3">

ADIOS
 
Last edited by a moderator:
Tatizo chama kizmezidi sana kuwachekea sana mapandikizi yakiongozwa na Zitto, pia hawa madogo wote wanapata kiburi kutoka kwa Zitto.... Na kama chama kitawachekea na kuondoa vidagaa vidogo vidogo( chagulani na henry) pia na kuwaacha mapapa kama( Zitto) basi mwisho wa siku chama kitaisoma namba tu.....................

Pia chama kiwafatilie zaidi na kuwaondoa mara moja vijana njaa ndani ya CDM.

Period...
 
Nachelea kutaja majina kwa kuwa sijapata maandishi yanayothibitisha kuwepo na mtandao huu pandikizi. Najiuliza intelijensia ya chama ipo kweli?????
 
Ndio ukomavu wa kisiasa huu mtu akienda kinyume kinachotakiwa ni kufanya maamuzi magumu japokuwa yanakitia doa chama lakini mwisho wa siku nidhamu inakuwepo na sio wanakaa na kuanza kumwona mwenzao hivyo wanazungumza tu matatizo yao ndani ya chama
 
wataishia kuomba msamaha kama wale madiwani wa arusha...kwenye msafara wa mamba na kenge wamo,wengine wanavumiliwa wengine wanatoswa,..hapo ndo wasiwasi wangu.,naona kuna double standard fulani sababu mtu kama shibuda alitakiwa awe analima pamba shambani kwake by now.
 
wakati mwingine tuwe watu wakutafakari sio maamuzi ya cc yanafaa sioni sababu ya kufukuzwa uwanachama mtu anapokosea. Hii ni sababu ya vyeo vya juu kugombaniwa, maslahi ya mtu binafsi Hapo mbele sana kuliko taifa ubabe nao uwahadaa walio cc, wanatoa maamuzi ya ubabe sababu ya nafasi walizopo, kama kweli mnatimua vijipandikizi vya ccm anza na shibuda mbowe, yeye amewapinga hadharani tena maamuzi ya chama mf bungeni Hapo ndo ntaamini hamna uchu wa madaraka ila mnajenga nchi, binafsi ni follower wa highness na wenje na nipo ilemela ila haya maamuzi sijaridhika nayo. tafakarini
 
Kumbe Highness nae ana jeshi jingine? Lakini nionavyo na kama ulivyo ulingo wa siasa si vibaya kuwa na kambi ila muhimu ni mgongano wenu wa kimasilahi una athari na manufaa kw kiasi gani katika Chama.

Sijui mnalitazamaje hili suala la matabaka kwa majaaliwa ya umoja wa CDM mza?
 
Nashangazwa na jambo moja! Kwanini CDM wanashindwa kuvunja migawanyiko kama hii mapema? Tunadhani 2015 ni mbali? Viongozi wanaposhindwa kuchukua hatua mapema kwa wanachama wasio waaminifu watafanya nini tukiwapa serikali? Huu mwendo huu mbona unataka kufanana na CCM iliyolea madogo kwa muda mrefu sasa yameisambaratisha.

Kwanza maamuzi ya kamati kuu yamechukua muda mno kwa mambo yaliyo wazi kikanuni! Si ndio haya haya ya tume za CCM tunazopigia kelele?

Kufukuza wanachama haitoshi,lazima ufanyike usafi kweli kweli kuelekea 2015 otherwise tutawakatisha tamaa wananchi!
 
Ni kweli jana mkutano ungefanyika kungechafuka mwanza.Zitto alikimbia kamati kuuu hakuwepo kwa nini?
 
Ccm igeni cdm.waloshindikana fukuza.chagulani ana uroho wa madaraka.amia kwa nape
 
Wapiga kura wa Igoma wana maoni gani kuhusu jambo ili.

Nahisi MwanaBodi Swali lingependeza kama lingesomeka hivi: Sample ya Igoma kwenye population ya CDM inaakisi chimbuko la kansa ipi ndani ya chama ambayo bila shaka mjadala huu unaweza kuwa muendelezo wa kusaka mwarobaini wake.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom