Polisi Mwanamke Mwenye Pepo la Ngono Asimamishwa Kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Mwanamke Mwenye Pepo la Ngono Asimamishwa Kazi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Mar 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,913
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Jessica Parfrey Sunday, March 07, 2010 4:00 AM
  Afisa mmoja wa polisi mwanamke wa nchini Australia amesimamishwa kazi kutokana na usumbufu anaowapa maafisa wa polisi wa kiume kwa kuwabembeleza afanye nao mapenzi. Afisa wa polisi Jessica Parfrey mwenye umri wa miaka 19, amesimamishwa kazi kutokana na usumbufu anaowapa maafisa wenzake wa kiume kwa kuwataka afanye nao mapenzi.

  Ndani ya siku chache za kuanza kazi kama afisa wa polisi wa mjini Sydney nchini Australia, Jessica alimtongoza bosi wake akimwambia kuwa "Kila mtu anajua kuwa unatakiwa uwe na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi mwenzako".

  Mwezi mmoja baada ya kuona bosi wake hana dalili zozote za kukubali, Jessica alimfuata na kumwambia "Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 19, unaonaje tukifanya mapenzi tu, hivi wewe una matatizo gani?"

  Mahakama ya mambo ya kazi iliambiwa pia kuwa Jessica alifanya mapenzi na afisa mwingine wa polisi kwenye choo cha baa.

  Jessica hakuishia hapo, alimsumbua afisa mwingine mwanaume wa polisi kwa kumpigia simu mara 12 na kumtumia meseji sita kabla ya kumuahidi kumsaidia afisa huyo kwenye mtihani wake wa mambo ya polisi. Jessica alimwambia afisa huyo kuwa kwa kila swali moja atakalopata basi yeye atasaula nguo yake moja. Afisa huyo alikataa dili hilo.

  Awali Jessica alisimamishwa kazi mwishoni mwa mwaka 2007 lakini alikata rufaa akisema kuwa matukio ya yeye kuwataka maafisa wenzake yalitokea wakati wakiwa baa nje ya muda wa kazi.

  Mahakama ya kazi ya mjini Sydney ilitoa uamuzi wake juzi na kuitupilia mbali rufaa ya Jessica.

  Mahakama hiyo iliunga mkono hukumu iliyotolewa awali ya kumfukuza kazi Jessica kwa kukiuka maadili ya kazi na kuwasumbua maafisa wenzake.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Duh, kaazi kwelikweli. Wampeleke kwa pastor Hummer akaombewe.
   
 3. Sydney

  Sydney Senior Member

  #3
  Mar 8, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo dada ni hatari, maana katika dunia ya leo hata kama sayansi na teknolojia imebadilisha mambo mengi lakini Jessica amepitiliza sasa jamani Du, hadi nahisi aibu!
   
 4. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Angekuwa bongo huyo sidhani kama angefukuzwa kazi, ungeshangaa kukuta anakaribia kuwa IGP.
   
 5. T

  Tall JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Unatakiwa
   
 6. T

  Tall JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Unatakiwa uwe na tabia njema hata nje ya kazi zako,kwa namna fulani huko nje unamwakilisha mwajiri/ofisi/kampuni
   
 7. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,468
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Wamelete Bongo huyo muone kazi yake, huchelewi kusikia amekuwa mbunge wa kuteuliwa!
   
 8. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #8
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,405
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]

  Jessica Parfrey outside court.


  Mrembo kama huyu angekuwa hapa Bongo mbona maafisa wetu wenge mfaidi sana na punde tu engepadishwa daraja.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,935
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  DAH Nadhani angekuwa Bongo ofisi yeyote ile angekuwa deputy director/manager/msemaji wa Kampuni na safari kila siku za nje, wabongo wamemeza mkia wa fisi maji.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  natamani angekuwepo kituo kidogo cha polisi pale kwa ali maua njia ya kwenda home kwangu..daaaaah ningemdandia mimi huyu
   
 11. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,033
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Aletwe kwa majaribio.
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  mbona afisa mwenyewe mdogo mambo mazito dah!
   
 13. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,667
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Demu mwenyewe bomba hivyo, anayejua email yake anipe nimuunganishe na mwanaume mwenye pepo kama yeye.
   
 14. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ameonewa sana, kwani maandiko yanasemaje? mmepewa bure nanyi toeni bure, kosa lake nini?
   
 15. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,440
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Afisa huyu aletwe kwa kina Mwema na Kova mwenyewe atakiona cha moto! Nyama ya Afande..
   
 16. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Mi natamani ningekuwa ri afande pande zile!!
   
 17. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ama kweli penye miti hapana wajenzi!
   
 18. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  anayehitaji contacts zake, nitumie PM haraka... :) vigezo na masharti kuzingatiwa
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Kaitaba si kiivyo ...
   
 20. y

  yegomwamba Member

  #20
  Mar 8, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Huyo demu ana pepo la ngono anafaa kupepewa.Laiti angekuwa hapa bongo,angeteuliwa kushika wadhifa wa kamanda Kova.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...