Polisi msilete ubaguzi na uchonganishi, "Gaidi mfia dini" ndio nani?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
309
1,000
Nimesoma maelezo ya DCI kwenye taarifa iliyoandikwa kwenye ukurasa wa Mwananchi news kua Marehemu Hamza alikua "Gaidi mfia dini" , hivi ni kweli kabisa ofisi ya DCI imeshindwa kupima kabisa uzito wa kauli hii? Kwa maana hiyo wafia dini wote ni magaidi?

Hamza alikua muumini wa dini ya kiislam kwa taarifa za majirani na familia yake, DCI awaambie umma wa waislam "Gaidi mfia dini" ni nani? Awaeleze watanzania ni dini gani inayotuma watu kua magaidi? Ugaidi wa Hamza wameuhusisha vipi na dini yake?

Hii chuki ambayo mnataka kuiingiza kwenye imani za watu ni uchokozi mtu na siyo sawa.Mnapaswa kuwaomba radhi waumini wa dini ya kiislam ambao kimsingi siyo wao waliomtuma Hamza kufanya aliyoyafanya.
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,924
2,000
Yote ni njia ya kujisafisha dhidi ya tetesi kuwa walikamata madini yake.

Walianza kwa kuwalaumu wazazi wake, sasa wamehamia kwenye dini yake. Yote ni kutaka watu waamini kwamba Hamza alikuwa gaidi ili waweze kufuta Tuhuma dhidi yao za kupora madini yake.
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,481
2,000
Hili jambo linahitaji Tume huru kuujua ukweli

Hata Wale Jamaa wa Madini wa Morogoro 2006 waliporwa madini wakanyukwa Risasi wakabatizwa Majambazi

Tume huru ikagundua walidhulumiwa Madini baadae wakadhulumiwa Uhai

Hata kwa Hamza ikiundwa Tume huru tunaweza kuuujua Ukweli kwa sababu sasa hivi Polisi wanaongea peke yao

Juzi Familia iliambiwa isipochukua mwili utazikwa na Jiji ikiaminishwa wameususa wakati Wanajua kabisa Familia hiyo ipo Mahabusu wakati huo

Tume ikithibitisha kuwa ni Gaidi sote itatubidi tushirikiane kumlaani na kulaani matukio yale kwa kuwa ni kinyume na maadili ya Nchi yetu na dini yetu
 

wakaliwetu

JF-Expert Member
Jul 16, 2020
656
1,000
Jamani viongozi wetu wote mpaka mjumbe wa Nyumba kumi wote ni walevi wamadaraka hata uwaambie nini hawatakuelewa wala hawata kusiki wanajijali wao na kufikiria hizo nafasi walizonazo tu.

Maandiko matakatifu yalishasema tutaumba dhambi kwa ndimi zetu, hawachuji kauli yakuitoa mbele ya jamii wala hawatafakari itapokelewaje ktk jamii. Mungu atunusuru na hawa watawala.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
6,522
2,000
Kawaida yao hao

Hata Wale Jamaa wa Madini wa Morogoro 2006 waliporwa madini wakanyukwa Risasi wakabatizwa Majambazi

Tume huru ikagundua walidhulumiwa Madini baadae wakadhulumiwa Uhai

Hata kwa Hamza ikiundwa Tume huru tunaweza kuuujua Ukweli kwa sababu sasa hivi Polisi wanaongea peke yao

Juzi Familia iliambiwa isipochukua mwili utazikwa na Jiji ikiaminishwa wameususa wakati Wanajua kabisa Familia hiyo ipo Mahabusu wakati huo
Ndugu zao waliachiwa na walishauzika na wakaomba msamaha kwa watanzania

USSR
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
6,162
2,000
Terrorism; the unlawful use of violence and intimidation, especially against civilians, in the pursuit of political aims.

Matumizi ya Ubavu mara nyingi kwa raia ili kufanikisha matakwa ya mtu (matakwa hayo yanaweza yakawa ya Kisiasa, Ki-imani hata mapambano dhidi ya wanyonyaji)

Hata Mandela to kwa macho ya wengine alikuwa ni Gaidi..., (intimidation and violence) ni Key world..., na Motive ndio inapelekea tumuite Gaidi wa aina gani
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,866
2,000
Kila wakati mtu au kiongozi anapofungua kinywa chake siku hizi ni uozo tu

Halafu wanakuja baadae kuomba radhi

Kila anaeamini Mungu atafia kwa anachokiamini

Yaani Mfia dini imekuwa kosa la jinai?

Yeye atafia kwa dini gani ya police labda
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom