Polisi mkoani Simiyu inamshikila mtu 1 baada ya kukamatwa na bunduki na meno ya Tembo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mtu mmoja kwa mkazi wa kijiji cha Mwabagimu wilayani Meatu baada ya kukutwa na bunduki moja aina ya Rifle 375 yenye namba B7054 ikiwa na risasi 15 na meno mawili ya Tembo yenye uzito wa kilo 8 ambayo thamani yake ni shilingi milion 8 na laki 8 pamoja na ngozi moja ya mnyama aina ya Nyegere yenye thamani ya shilingi laki 6.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Onsemo Lyanga amesema pamoja na vitu hivyo pia walifanikiwa kukamata podo mbili zenye jumla ya mishale 10 ambapo kati ya hiyo mishale sita inadhaniwa kuwa na sumu.

Kamanda Lyanga amesema mtuhumiwa huyo anatarajia kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamalika ambapo pia amewaonya wale wote wanaojishughulisha na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Serengeti na mapori ya akiba kuacha mara moja kwani jeshi hilo kwa kushirikiana na askari wa idara ya wanyama pori haliwafumbia machowale wote wanaohusika na vitendo hivyo.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom