Polisi mkoa wa Kilimanjaro wadaiwa Sh1 bilioni na TANESCO

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,495
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kilimanjaro, Mahawa Mkaka amesema wanadai zaidi ya Sh1 bilioni polisi mkoani hapa kutokana na malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.

Akizungumza ofisini kwake leo, Mkaka alisema madeni hayo yanatokana na malimbukizo ya zaidi ya miaka mitatu.

Mkaka alisema kutokana na deni hilo kuwa kubwa, polisi wanaweza kuingia mkataba na TANESCO ili kuona namna ya kulilipa badala ya kusubiri kukatiwa huduma.

Alisema zipo taasisi za Serikali na binafsi zenye malimbikizo ya madeni ya muda mrefu. Alizitaja kuwa ni idara za maji, Magereza na Shule ya Polisi Moshi (TPS).

Kuhusu magereza, Mkaka alisema wanadaiwa zaidi ya Sh500 milioni huku idara za maji wilaya za Same na Mwanga, zinazodaiwa Sh400 milioni kwa pamoja na TPS inadaiwa zaidi ya Sh250 milioni.

“Tunasisitiza watu waje ofisini tukubaliane namna ya kuliopa, ili tuingie mkataba, wapo baadhi ya wateja wameanza kupunguza madeni yao,” alisema Mkaka na kuongeza:

“Kikubwa ni kwamba wajitokeze tuone namna ya kuingia mkataba, ili wapunguze madeni yao badala ya kukaa kimya, kwa sababu hatua inayofuata ni kuwakatia huduma.”

Mkaka alisema kutokana na wateja kutolipa ankara za umeme kwa wakati wanapeleka, wanaanza kuwapelekea notisi ya kukatiwa huduma.

Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alisema hajui chochote kuhusiana na madeni hayo.

“Hivi kudaiwa kwa Polisi kunakuhusu nini wewe, ebu niache,” alijibu Issah.

Agizo la Rais Magufuli

Juni 6, Rais John Magufuli aliiagiza TANESCO kuwakatia umeme wateja wote wenye madeni makubwa ikiwamo Serikali ya Zanzibar.

Alitoa agizo hilo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye kituo kipya cha TANESCO mkoani Mtwara na kwamba, taasisi zote za umma zinapaswa kulipa madeni la sivyo zitakatiwa umeme.

Rais Magufuli alisema Serikali ya Zanzibar pekee kupitia Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), ina deni la Sh121 bilioni

“Msiogope mnapaswa kukata huduma hii kwa taasisi yoyote ambayo hailipi bili zake.Nataka kumwambia Waziri wa Nishati na Madini, (wakati huo) Profesa Sospeter Muhongo kwamba umeme unapaswa kukatwa hata Ikulu. Nikilala gizani, halafu maofisa wa Ikulu ambao hawajalipa watawajibika siyo wewe. Una hakikisho langu kwa hili.

“Fedha za kulipa bili kawaida hutolewa kwa wizara zetu, lakini badala yake hupelekwa kwingine,” alisema Rais Magufuli na kusisitiza:

“Naambiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haijalipa Sh121 billion. Ninyi (TANESCO) si wanasiasa... mnapaswa kuzingatia majukumu yenu ya kitaaluma... kata huduma ya umeme.”

Nimesema hata kama ni Ikulu , polisi, jeshi ama shule , hakuna mwenye deni anaepaswa kuachwa . Ni kwa njia hii tu tunaweza kuhakikisha kwamba pesa zilizotengewa wizara kwa ajili ya umeme zinatumiwa kama ilivyopangwa ili TANESCO iweze kuendesha kazi zake na kushughulikia matatizo ya uhaba wa umeme. ‘’TANESCO haiwezi kuboresha huduma kwa sababu ya madeni ya serikali yasiyolipwa’’.

Alipozungumza na gazeti la Citizen jana , Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa pili wa rais , Bwana Mohammed Aboud, alisema kuwa mipango inafanyika kwa ajili ya kuliwezesha shirika la Zeco kulipa madeni ya TANESCO .

“Maagizo ya rais Magufuli yako wazi. Madeni lazima yalipwe na yatalipwa. Tumeanza mchakato wa kuhakikishwa suala hili linatatuliwa.Pia tumeiagiza Zeco kuacha kulimbikiza madeni mapya.

Mawaziri hao wawili walifanya mkutano juu ya suala hilo hivi karibuni na kujadili namna deni hilo linavyoweza kulipwa ,” Bwana Aboud aliliambia gazeti la The Citizen.


Muungwana
 
Napenda sana warudie ule mchezo wao wa wakati ule,Polisi wanakamata magari ya Tanesco na Tanesco wanaenda kwenye main line ya umeme ya Polisi wanakata umeme kwa kuondoa fuse kubwa. Ilibidi Waziri wa Nishati na wa Mambo ya ndani wakutane kuweka mambo sawa.
 
Tanesco si wakakamate gwanda zao mpaka watakapo lipa

‍♂️naenda zimbobo.
 
Back
Top Bottom