Uchaguzi 2020 Polisi, Mgambo, Zimamoto, Uhamiaji kusimamia uchaguzi

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
768
1,959
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amesema majeshi yote yameungana na tayari yamesambazwa kwenye mikoa mbali mbali
ikiwemo Arusha ili kusimamia uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano ijayo Oktoba 28.

Sirro ametaja majeshi hayo kuwa ni Polisi wenyewe, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Mgambo ambao tayari wapo Mkoani Arusha kwa
ajili ya zoezi la kuhakikisha utulivu unakuwepo siku ya kupiga kura.

Akizungumza akiwa mkoani Arusha, Sirro amesema anatambua kuwa kuna vikund ambavyo vimepangwa kwa ajili ya kufanya vurugu siku ya uchaguzi na kuvuruga amani, hata hivyo watavikamata kabla ya siku usiku.

"Kuna vikundi vinataka kuharibu amani katika uchaguzi jijini Arusha vitakamatwa kabla ya siku ya uchaguzi ili kuondoa malengo yao ya kuharibu amani, "amesisitiza na kuongeza" Arusha imekuwa na historia ya vurugu tumeleta polisi wa kutosha kudhibiti wachache wanaotaka kufanya vurugu," amesema.

IGP amesema askari wanatakiwa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa wa amani na kudhibiti changamoto zozote ambazo zitajitokeza za kiusalama. Hata hivyo aliwataka wananchi watoe ushirikiano wanapohisi uvunjifu wa amani ili hatua haraka zichukuliwe.

Chanzo: Habari leo
 
Uchaguzi huu utaishia kwa Amani, Mungu wetu aliye tuvusha kwenye Corona ndiye anayekwenda kutuvusha kwenye uchaguzi.
 
Maneno ya kipuuzi na ya hovyo kabisa kutoka kwa IGP, hii ni aibu kwa jeshi la polisi, kama wanajua kuna hivyo vikundi kwanini wasiwakamate hao wahalifu mapema halafu mambo ya uchaguzi waachiwe raia? Au taasisi za kiraia? unajaza hao watu kwani ni uchaguzi wa jeshini huo?!

Hii ni mbinu ya kuwatisha wapiga kura wasijitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura ili Gambo mwenye hali mbaya ashinde, Sirro amefeli na wale wanaomtumia pia wamefeli, machalii wa chuga hawana mambo ya kisoro kuogopa mandata kiboya, jumatano kura zitapigwa, na Lema atashinda.
 
Anayetaka amani kwa dhamira ya dhati ya moyo, ni lazima asisitize haki na transparency. Vinginevyo huna utofauti na mkulima mjinga anayepambua majani ya mbuyu akiamini utakauka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana IGP na vyombo vyote vya usalama, naamini uchaguzi utapita salama na maisha yataendelea kama kawaida.
Mungu ibariki Tanzania
 
Hivi kwanini hasemi uchaguzi utakuwa wa haki, anarudia rudia tu kusema watahakikisha uchaguzi unakuwa wa amani! Kwanini asiseme watahakikisha uchaguzi unakuwa wa haki na amani

1. Hivi mtu akikaa mita 100 kusubiri majibu kuna ubaya gani? Kwanini unakataza watu kulinda kura zao walizopiga kila kituo kama una hakika hakuna michezo yoyote itakayochezwa. Si uwaache tu wajikalie matokeo yakitangazwa wanaenda makwao

2. Hao magereza mnaowaleta kulinda uchaguzi kule watokako wafungwa wamewaacha na nani?
 
Kuna watu watakamatwa kabla ya Uchaguzi hivyo hawatapiga kura siku ya uchaguzi.

Hii ndiyo kutumia dola ili kubaki madarakani.

Ukidakwa na kikosi Cha Magereza unapigika Kama mfungwa hatari San hii​
 
Wapinzani Waambieni wale mliowaleta toka nje kuja kufanya vurugu waanze kufungasha virago haraka kurudi kwao. Uhamiaji wanawajua wote na wanapolala na kuamka waondoke kabla ya siiku ya uchaguzi kitakachowakuta shauri yao.
 
hivyo vikundi mlivyoleta toka nchi jirani watazikwa wazima wazima kimya kimya

Sirro anawawashia taa nyekundu kuwa tusilaumiane ondokeni rudini kwenye nchi mlizotokea upesi
CCM akili zenu ndogo msipotoa haki tutawabiiri
 
Yafaa kukumbua amani,Bila haki ni ngumu kuwepo, ila haki ikiwepo huambatana na amani.
 
Hivi mtu akikaa mita 100 kusubiri majibu kuna ubaya gani? Kwanini unakataza watu kulinda kura zao walizopiga kila kituo kama una hakika hakuna michezo yoyote itakayochezwa. Si uwaache tu wajikalie matokeo yakitangazwa wanaenda makwao

Mambo ya kuepuka kwa mpiga kura ili usije ingie matatani siku ya kupiga kura​

1. Jambo la kwanza usifanye fujo kituo cha kupigia kura au kupiga makelele,kuzozana nk ile ni sehemu ya kupanga msitari na kupiga kura yako kwa amani na utulivu

2. Kazi ya kujumlisha matokeo ya uchaguzi na kuyatangaza ni kazi ya tume ya uchaguzi tu tena kwenye vituo husika official vya tume.Usije ukakaa guest house au popote na hawara yako mkaanzisha kituo chenu cha kujumlisha matokeo na kuyatangaza kuwa hayo ndio matokeo .Ujumlishaji na utangazaji ni kazi ya tume tu kuanzia mwanzo wa kuzijumlisha hadi mwisho wa kutangaza.Kwenye ofisi zao official ikiwemo kituo cha kupigia kura nk

Mtu yeyote awe mgombea au mpiga kura ,taasisi yeyote au au chama chochote cha siasa au chombo cha habari hakiruhusiwi kutangaza matokeo ambayo tume haijatangaza na kutoa ruksa yatangazwe.Usiende huko na huko ukitangaza matokeo ambayo Tume haijatangaza.

3. Ukipiga kura ondoka nenda zako nyumbani au kwenye biashara zako .Siku hiyo mikusanyiko ya aina yeyote hairuhusiwi popote kwa umbali wowote uwe mfupi au mrefu kiasi gani hata iwe kilomita elfu moja toka kituo cha kupigia kura hiyo ni kwa mujibu wa uamuzi wa mahakamu kuu uliotolewa mwaka 2015.

Nakala ya katazo la mahakama kuu hili hapa
1603430313039.png

1603430373239.png


1603430428314.png
 
Back
Top Bottom