Polisi Mbeya wameshindwa kudhibiti ujambazi wa nondo

kamili

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
1,213
849
Ni kawaida unapokuwa Mbeya kusikia mtu au watu wamepigwa nondo kichwani na majambazi na kuporwa mali. Na wakati mwingine matukio hayo hutokea hata jirani na police.

Mwaka jana tukio moja liliwakumba police wawili wakiwa wamevaa kiraia na kupelekea moja kufariki kwa kupigwa nondo na hao majambazi.

Matukio hayo yameanza muda mrefu sana, zaidi ya miaka 10 sasa. Wiki ya jana watu wasiopungua watano walilazwa hospitali ya rufaa Mbeya kwa kupigwa vichwani na nondo.

Juzi tumeona kule Songea watu wasiokuwa na silaha wameuwawa na police, lakini pia police wamelaumiwa mara nyingi kwa kuua watu wasiokuwa na hatia katika matukio kadhaa.

Swali langu ni kuwa kwa nini police haitumii maguvu yake kudhibiti vitendo vya kihalifu kama hivi vya ujambazi wa nondo na badala yake huelekeza maguvu hayo kwa watu wasio na hatia wala silaha?

Na tena wasiwasi wangu mkubwa ipo siku wakazi wa Mbeya wataandama kuwasilisha kilio chao hicho na bila ya shaka kama ilivyo kawaida police watawauwa waandamanaji kikatili.

Naomba mjadala kwa wana JF nini kifanyike kuepusha hali hiyo.
 
Arusha wizi ukitokea polisi wanakuja masaa mawili baada ya wezi kuondoka . Tena wanauliza kama wameondoka ndo waje . Teh teh teh kazi kwelikweli.
 
very interesting topic...., ni kweli nguvu (manpower+resources per time) itumikayo kum-undermine raia, ingetumika kuwakamata wapiga nondo(wahalifu in general).., tungekua na imani sana na hiki chombo kinaitwa polisi
 
Polisi wa Bongo huwa hawatafuti wahalifu,wahalifu ni maswahiba zao, wenyewe huwatafuta watenda wema tu.Nasema hivyo kwa sababu wahalifu hawawezi kuandamana hata siku moja.
Cha kufanya ni kulivunja jeshi la Polisi kabisa baada ya miaka kumi ndio tuunde upya maana ile element iliyopo sasa itakuwa imepotea.
Kauli ya chagonja juu ya tukio la Songea ndio inayonifanya kuandika haya niliyo andika leo.
 
Back
Top Bottom